Nimeacha damu yangu ughaibuni (Michigan, US) kisa ni ubaguzi wa rangi. Ushauri please

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
526
583
Mnamo mida ya jioni( saa kumi hivi), ikiwa ni majira ya spring katika mji wa Houghton (Michigan) nilikuwa nimetoka kufaidisha kinywa katika mghahawa wa Rodeo Mexican Kitchen, nilipokea simu ya dharula kutoka kwa kiongozi wetu wa tech club, kwamba tunahitajika mara moja kwa dean of students wa College yetu. kwa wakati nikaingia hostel (Douglass Houghton) kuchukua Laptop yangu na kuelekea katika viunga vya ofisi wa mlezi wa wanafunzi (Dean) wa Electrical and Computer Engineering College katika chuo kikuu cha Michigan Technological Univesity.

Kulikuwa na mualiko wa dharula kushiriki mashindano ya uvumbuzi wa kitechnologia katika state nzima ya Michigan. Klabu yetu ilipewa jukumu la kutafiti na kutoa uvumbuzi wa namna ya ku-locate fault za umeme kwa underground cables kwa specifications sahihi kwa maana ya location, dimensions na ukubwa wa tatizo. Lilikuwa jukumu zito sana ukizingatia tulikuwa na week moja tu ya maandalizi, basi kama kikundi kwa pamoja tukapeana majukumu ya kutafiti kwa vipande ili baada ya siku mbili tujumuishe tafiti zetu kwa pamoja.

Naam, Kesho yake nakumbuka ilikuwa ni Ijumaa-asubuhi Jerusalem nilizama katika Library ya Technologia (Van Pelt and John Opie Library) ilikua ndio sehemu niliyo ipenda zaidi wakati wote wa kuchimba madini. Nikiwa nafanya kilichonipeleka, ghafla nikasikia sauti ya kilio kwa mbali upande wa pili wa shelves za vitabu, wakati naifatilia sauti ile, nikagundua ilikua ni ya mwanamke, nilichukua hatua ya kunyanyuka na kwenda upande wa pili wa Shelves.

Mtoto wa kike, mzuri sana, chotara (sikujua ni mixer wa races zipe kwa wakati ule) alikuwa ameinama chini, laptop yake aina ya Mac-book ikiwa imepasuliwa. Kwa haraka nikajiongeza kwamba kilio kile kimetokana na kupasuka kwa Mac yake, kwa rafudhi yangu mbaya ya Kitanzania, nikamuuliza mtoto, "whats wrong", hakunijibu zaidi ya kuendelea kuangua kilio. Basi, nami niliketi chini alipokuwa analia, niliinyanyua Laptop ile na kuanza kuingalia (wakati wote kilio cha binti huyo kinazidi), kwa mbali (kutokana na crakes za kioo) nikaona alikuwa amefungua website ya chuo, site ya matokeo binafsi ya mwanafunzi.

Kwa haraka nikapata mwanga kwamba, hii pisi itakuwa imefeli mitihani na kupelekea kuvunja Laptop yake mwenyewe kwa hasira. Wakati naendelea na udadisi wa nini kilitokea, ghafla nikasikia kama kuna kundi la watu linakuja upande wetu, ndani ya nusu dakika, walinzi wawili( wazungu) na mmama (mweusi) ambaye alikuwa ni Librarian walitufikia, Binti yule alivyowaona akaongeza zaidi kilio huku akiweka mikono yake kifuani, kuashiria kwamba anaumia. Walijaribu kumbembeleza na kumdadisi kinachopelekea kilio chake, kwa kustaajabisha na kushangaza, bila kusema neno lolote akapoint kidole chake kwangu kuashiria mimi "Jerusalem" ndio sababu ya kilio chake.

Wale walinzi waligadhibika sana, huku wakionesha chuki za wazi wazi kwangu, walininyanyua kwa dharau pale chini nilipokuwa na kuanza kunipeleka wanakojua wao, yule mama(Librarian) alijitaidi kuwasihi wanihoji na mimi kujua na story yangu pia. Kwa kuwa nilikua kwenye mshtuko mkubwa, na kwa kuwa kiingereza changu kilikua cha kuungaunga, nilishindwa kujieleza chochote, zaidi ya kubaki nimetoa macho mithiri ya ng'ombe anayekata roho. "This huligan is at fault, we must take him to custody" yalikuwa ni maneno ya wale walinzi wa kizungu wakati wananipeleka kwenye cell ndogo ya chuo kwa kosa la kumjeruhi na kuvunja kifaa cha mwanamke.

Wakati haya yote yanajili, binti yule alikuwa hajaongea chochote, zaidi ya kuonesha ishara iliyonitia hatiani, kuzidi kuangua kilio na kujishika kifuani kuashiria maumivu. Niliondoka na wale mabwana wawili, binti alibaki na Librarian akimbembeleza pamoja na wanafunzi wachache ambao walikuja kushudia lile tukio.

Nilijitambulisha katika cell ndogo ya pale chuoni, kwamba mimi ni "Jerusalem 2006 ", mwanafunzi (international) wa under-graduate, mwaka wa kwanza nilikuwa nasoma Electrical Engineering, katika college ya Electrical and Computer Engineering College, chuoni Michigan Tech University. Walichua ID zangu zote zilizokuwa kwenye wallet yangu na kuthibitisha nilichokuwa nakisema. Zaidi, niliwaambia mimi ni member wa Houghton Technology Club ya pale chuoni, na kilichonipeleka Library ni kufanya utafiti wa task iliyokuwa mbele yetu.

Baada ya kuchukiliwa maelezo, niliwekwa kwenye detention kama ya lisaa limoja hivi, then, nikafatwa na walinzi wengine wawili na kupelekwa "Admistration and Students services Building" ilipo ofisi za mshahuri wa wanafunzi (Dean) wa Chuo kizima. Nilistaajabu na kushangaa nilipomkuta yule binti (chotara) wa Library akiwa mwenye furaha na anacheka pamoja na Librarian (yule mama) wakisubiri kuingia kwa Dean. Sikuongea neno lolote, na nilivyofika moja kwa moja na kwa pamoja tukaitwa ofisini kwa Dean, ( Mimi, binti chotara, Librarian na wale walinzi wa kizungu).

Mahojiano yakaanza kati ya Dean na Binti yule;

Dean; "JIna lako unaitwa nani?"
Binti; "Charlotte Middleton Peters"
Dean;"Uko stage ipi ya elimu na unasoma nini?"
Binti; " Niko Sophomore (mwaka wa pili) na Nasoma Electrical Engineering"
Dean; " Kwa kifupi, tueleze kilichotokea"
Binti; " Matokeo ya Semister iliyopita yametoka na kwa bahati mbaya nimefeli masomo matatu"
Dean; " Uhusiano baina yako na huyu kijana ni upi?"
Binti; " Haupo"
Dean;" Kijana anahusika vipi na kuvunjika kwa Laptop yako"
Binti; "Hakuna, hausiki na chochote"

Baada ya maongezi marefu, ikaonekana nipo innocent, Mwamba mimi, kijana wa mwaka wa kwanza (Freshman) nikawa huru kuendelea na majukumu yangu,huku wale mabeberu wa kizungu (walinzi) wakiniomba msamaha kwa kunidhalilisha na kunipotezea muda.

Siku zikapita, research tukafanya na uvumbuzi ukakamilika, Club yetu ya Houghton Technology ikapata tuzo ya Platnum kama mshindi wa kwanza, huku mimi nikipata tuzo binafsi kama mshiriki bora(nili present vizuri sana mada) wa mashindano yale katika State nzima ya Michigan, Mwaka 2012 mwezi wa Tano.

Baada ya mashindano nikiwa nimebeba tuzo yangu mkononi, begi langu la Laptop mgongoni katika viunga vya "Wadsworth Residence Hall" nikasikia sauti ya kike ikiniita kutokea ndani, nilijaribu kuangaza huku na kule bila mafanikio, ghafla nikamuona Charlote Middleton anakuja kwa kukimbia, alikua amevaa skin tight nyeusi, top off-shoulder nyeupe na in-door ruber mguuni, kwa mavazi yale, nilibahatika kuona uzuri wa binti yule, alikuwa ni mzuri sana wa sura, shep ya kibantu, nywele za kilatino, weupe wa chotara. Mtoto, aliniomba msamaha wa maswahibu ayonisababishia week moja kabla akisema kulitokea misunderstandings tu, akanipongeza kwa presentation nzuri na tuzo nilizopata kwenye mashindano ya ki-techologia.

Baada ya maongezi mafupi, akaniaga anaondoka, mswahili mimi nilipata kiguumizi cha kumuomba mawasiliano, kwani hakuwa level zangu, mimi nilikuwa level za kina mwajuma na chaupele, yeye alikuwa level za beyence huko, yaani ni kama mbingu na ardhi;
Mwamba nilikua mweusi (weusi wa kihaya au msukuma), mrefu na sina hela. Nilibahatika kusoma marekani kwa scholarship(nitaelezea mbele) na uwezo wangu wa akili (nilikuwa kipanga), basi mate yalijaa mdomoni wakati najitutumua kumuomba malaika yule angalau nafasi ya kumuona tena. Nilimuita, "Charlotte", wakati anageuka kurudi kwenye residence yake, "can we meet again"? Nilimuuliza, Mrembo yule alinijibu kwa wepesi sana, " yes sure, do you want my number?" Mwamba nikaona neema imenifuka na paradiso imeshuka duniani, nilichukua mawasiliano yake kwenye kisimu changu cha Samsung (zile za kufunga) na kuahidi kumtafuta yule malkia.

ITAENDELEA WAKUU....Ngoja niende Church kwanza.


 
Wakati tukijipa break kusubiri mwendelezo, tupate kitu cha ku-refresh!




 
Wakati tukijipa break kusubiri mwendelezo, tupate kitu cha ku-refresh!





 
Back
Top Bottom