kt the irreplaceable
JF-Expert Member
- Oct 12, 2017
- 2,363
- 4,851
Wewe bwana mdogo hapa utaandika mengi ukijikita kwenye sheria na utaratibu na wala sio facts. Inawezekana kweli kabisa polis hawachunguzu vya kutosha, lakini kwa hali ilipofikia ilihitajika mbinu ya kupunguza speed ya uhalifu wa panya road.Hoja yangu ipo very clear sitetei na sitawahi kutetea ,Nchi yetu Ina katiba ,sheria za mienendo ya Makosa ya jinai ,PGO,Kanuni za Jumla za Adhabu sheria zote hizi zimeweka utaratibu wa kushughulikia makosa ya uhalifu .
Hakuna sehemu Polisi amepewa mamlaka ya kuuwa mtu kama njia ya kupambana na uhalifu , Polisi wamepewa wajibu wa kuchunguza na kupeleleza sio kuhukumu kwa kupiga mtu Risasi ni Mahakama tuu ndiyo yenye jukumu la kutoa adhabu iwe ni adhabu ya kifo ,kifungo Cha maisha au miaka yeyote hayo hufanywa na Mahakama. Mimi unanishambulia Nina taka Sheria tulizojiwekea tuzifuate na kuziheshimu ,kama hatuzitaki zimepitwa na wakati ktk kupambana na uhalifu tuzibadili, kwanini tuzivunje ???
Ndio maana tuna sheria,katiba , kanuni na taratibu zimeweka utaratibu wa namna ya kupambana na uhalifu .
Ndio maana kuna Mahakama siku zote , ingekuwa Polisi wanaaminika kwa kila Uchunguzi au upelelezi wao kungekuwa hakuna haja ya Mahakama kupima ushahidi na kila siku Polisi wangekuwa wanashinda kesi , ndio maana kuna Mahakama ,ni muhimu sana Ndugu zangu uhalifu ukapambanwa kwa mujibu wa sheria,kama sheria zetu hazifai kupambana na uhalifu tuzibadili ila sio kuzikeuka kwa kumuuwa na kumpiga Risasi Mtuhumiwa.
Hata hao Panya Road wanaofanya uhalifu sheria zipo wakikutwa na hatia wanaadhibiwa sawa na sheria inavyosema kuna kifungo adhabu ya kifo , kifungu cha maisha ,miaka 30 na adhabu zingine . Kwanini wasishtakiwe kwa mujibu wa sheria wajibu wa Polisi ni kufanya upelelezi na uchunguzi kuisaidia Mahakama kufanya maamuzi sio kuuwa watuhumiwa.
Kama tunaona hakuna haja ya kuchunguza na kushtaki Polisi washinikize sheria zibadilishwe ili iwe rahisi wao kufanya wanachokifanya , hakuna mtu anatetea wahalifu ,ninachotaka utaratibu ufuatwe ktk kupambana na uhalifu na kama sheria zetu ni Butu basi tuzibadili na sio Polisi kuchukua hatua ya kuuwa Watuhumiwa bila kuwapeleka mahakamani.
Fuatilia matukio ya panya road, wanakua mpaka vijana 30 kwenda kupora, sasa vikundi vya watu 30 vipo vingapi? Kila kijana akifunguliwa faili la upelelezi itachukua muda gani polis kumaliza kazi? Hao polis hawana shughuli nyingine?
Najua wanasiasa mnapenda sana public attention, ila suala la usalama wa watu ni priority namba moja kwa kila nchi. Leo panya road wanaua watu ambao sio ndugu zako, pengine ipo siku tukio litakugusa moja kwa moja na utajifunza kitu.
Ni lazima tuzungumze uhalisia, nchi hii ni masikini mifumo ya sheria na haki ina matatizo makubwa, upelelezi ni gharama hivyo mahakama huachia watuhumiwa wengi wa uhalifu kwa kukosekana ushahidi wa moja kwa moja, lakini sio kweli kua watuhumiwa ni wasafi. Na hii ni loophole ambayo hadi wahuni wanaijua... polis wakilegeza kamba panya road watashinda hii vita, kama yalivyo makundi ya ulanguzi wa dawa za kulevya pale Mexico.