Nilivyonusurika kuchunwa ngozi sababu ya bangi

Jerry001

Member
Apr 29, 2020
21
57
Wazee wa jukwaa nawasalimu.

Sitosahau kisa hiki kilichonikuta skonga miaka ya 2003 wakati nipo sekondari moja huko nyanda za juu kusini.

Ilikuwa Ijumaa mishale ya saa 2 usiku, ambapo mimi na jamaa zangu watukutu tulikuwa tunajiandaa na paper za NECTA tukaona sio mbaya twende kijiji jirani kutafuta bangi kama kawaida yetu.

Tulikuwa na kundi letu la watukutu, yaani masela uchwala ila wazee wa kukesha na kupopoa msuli mpaka majogoo.

Sasa hiyo siku tukatoka mimi, wanangu Chino, Buga na Chopa haaoo mpaka karibu na kilabu kimoja cha gongo ambapo ndio pusha wetu ilikuwa maskani yake.

Kufika pale hatukumkuta, tukaelekezwa kuwa atakuwa kwenye disko vumbi ambapo sio mbali sana na pale.

Tukaona fresh ngoja tutimbe mpaka eneo husika, wakati huo Chino na Buga walishanunua sigara kali wakipiga pafu mdogo mdogo.

Kufika disko vumbi, Chopa akatinga ndani kumtafuta pusha, wakati huo mimi na jamaa wengine tupo nje tunasikilizia. Zikapita kama dakika 10 Chopa hajarudi, ikabidi mimi niende kumfuatilia ili kujua nini tatizo.

Kuingia ndani, moja kwa moja nikatimba mpaka kwa msaidizi wa dj nikamuuliza kama amemuona pusha. Yule jamaa akanijibu kifupi kuwa hayupo. Nikamuuliza tena kama alikuwepo pande zile akasema hajamuona. Nikamuona jamaa chenga. Kumcheki vizuri kumbe jicho nyanya, hivyo hatuelewani.

Kurudi nje sikumkuta Chino wala Buga. Nikaanza kuwafuatilia walipoenda, nikajua tu watakuwa wamerudi kule kilabuni kwa mwanzo na Chopa.

Nikachukua njia moja kwa moja mpaka kilabuni. Cha kushangaza sikuwakuta ila nilimkuta Chopa ambaye alidai ametutafuta sana maana baada ya kumpata pusha alidai mzigo kauacha maskani kwake. Tukaona sio shida tukanunua bangi ya mia tano hao tukasepa mdogo mdogo kurudi disko vumbi kuwatafuta Chino na Buga.

Tukiwa njiani tukasokota vijiti viwili vya msuba tukawasha nyasi na kula moshi mdogo mdogo kisha kuucheulia puani kama gari moshi. Basi baada ya kuvuta pafu kama nne za haja nikaanza kusikia kichwa kizito na njaa kiasi. Kadri muda ulivyoenda nikaanza kusikia njaa kali na kichwa kizito kama nimebeba zile ndoo za maji za chuma (wahenga mnazimanya fresh).

Kwa mbali nikawaona Chino na Buga, ila cha ajabu walikuwa wamebadilisha nguo. Chino amevaa koti kama la daktari na Buga koti kama la fundi makenika. Nikafikicha macho kuona kama yananidanganya sababu ya bangi au ndivyo ilivyo. Kuangalia vizuri kumbe Chino kavaa vazi la wauza bucha maana lilikuwa na damu damu kiasi.

Kuwafikia, nikasikia Chopa anawauliza walikuwa wapi, ndipo Buga akajibu walifuata vifaa vya kazi.Wakati huo mdomo wangu umekuwa mzito mbaya siwezi hata kuunyanyua kuongea chochote ukizingatia na ile njaa kali iliyonikumba ghafla.

Sijakaa sawa nikasikia Buga anamuuliza Chopa kama kazi waliyompatia ameshaifanya. Chopa akatikisa kichwa kama kuwapa ishara fulani. Basi tukawa tunaongozana kwenda njia panda ya kuelekea shule. Kufika mbele karibu na vichaka vya mianzi Chopa akawaambia tuingie pori kumalizia Bangi aliyokuwa nayo. Hapo ndio machale yakanicheza

itaendelea...
 
Inaendelea tulipoishia...

Baada ya kuingia kwenye kichaka mwili wangu ulikuwa na ubaridi kiasi, muda huo mbala mwezi inaangaza kiasi na usiku umeshasonga kiaina, jamaa zangu bila kuchelewa wakaandaa misokoto miwili ya haja na kuanza kupuliza. Wakanipasia msokoto mmoja baada ya kupiga pafu mbili kwa uoga uoga na wakati nikiwa bado na wasiwasi ndipo nikaanza kusikia mipango yao.

Kabisa nikasikia wana wanapanga namna gani watanichuna ngozi, maana walikuwa kama wanabishana namna ya kunidhibiti endapo nitawazingua kwa vyovyote, sikutaka kuamini masikio yangu, maana wakati huo najua fika Chino, Chopa na Buga ni masela wenzangu wa skonga. Japo Chino na Buga walikuwa wakubwa kiumri kama miaka 19-21 na mimi wakati huo nilikuwa mdogo mdogo kwa umbo pia.

Maswali dabo dabo yakaanza kunijia kichwani. Ina maana hawa jamaa wa huku yaani Chino, ambaye alikuwa ni mwenyeji wa Mbeya na Buga kutoka Iringa wanataka kunitoa kafara mimi.

Muda ulivyoenda nikaona wanaanza kuongea kwa kunong'onezana na nikasikia kwa mbaaali kama Chopa ananiambia, oya askari wangu naona umeshaanza kuyumba kaa chini utulize ndosi. Hapo ndio nikaona mpango wao wanataka wa utimilize.

Ikabidi nizuge kama naingia kichakani kukata gogo kwanza, wakati huo Chino na Buga siwaelewi maana wanapeana ishara fulani za kutekeleza jambo. Kana kwamba hawakuafiki mimi kwenda faragha kukata gogo na kwa haraka haraka nikajua wanaweka mipango ya kuniweka chini ya ulinzi.

Basi ile wamenipa nafasi kama mita kumi, nikaroka mbio huku nikipiga yowe la kuomba msamaha...."nisaidieni, wachuna ngozi, nisaidieni jamani, wachuna ngozi" . Wakati huo nikaangalia fasta njia ya kuelekea skonga. Jamaa wakaniungia , uzuri kwenye mbio nilikuwa sio haba. Kwa nyuma nikamsikia Chino anasema mkamate huyo kabla mambo hayajaharibika.

Kufika maeneo fulani kwa mbali nikaliona bweni la kwanza la shule. Sasa kutokana na wenge na hofu nikajishauri nikimbilie kwenye uwanja wa shule ambapo itakuwa rahisi kuwaona wachuna ngozi kama bado wananifuatilia kwa nyuma.

Kufika karibu na maeneo ya uwanjani kuna kisiki sikukiona. Nikakigonga kwa nguvu upande wa mguu wa kushoto. Kwa ule mshtuko na maumivu nikajikuta nimezima palepale.

Kuzinduka baada ya dakika kadhaa baadaye nikajikuta nimefungwa kamba kwenye miguu kuanzia magotini na mikono kwa nyuma. Kuhamaki nikaona damu zinanitika mguuni. Hapo nikajua kabisa nimeisha na nipo kwenye himaya ya wachuna ngozi na wameshaanza kazi yao.

Nilianza kulia kwa kububujikwa na machozi huku nikijaribu kuona namna ya kujiokoa kwa kutambaa kama jongoo. Kuhamaki nikawaona wanagu Chino, Buga, Chopa na Msenyere wakiwa pembeni wanasikitika tu. Chopa akaniuliza, oya askari unajisikiaje sa hivi. Nikashangaa sana hawa jamaa walikuwa nananikimbiza ili kunichuna ngozi halafu wanaulizia hali yangu.

Baada ya kumakinika ndio nikaja kuusoma mchezo kumbe hayo yote yalikuwa akilini mwangu tu kwa sababu ya bangi. Maana Chino na Buga hawakuwa na zile nguo nilizoona wakati wa dozi ya bangi pori imenikolea. Mmoja alikuwa amevaa sweta jeupe lenye maua maua mekundu na mwingine kikoti cha Bluu juu ya shati lake. Dah. nilichoka.

Kumbe jamaa walijua nakimbilia shule kuharibu na ingekua msala Jumatatu. Ikabidi wamcheki Msenyere ndiye aliyetoa wazo nifungwe kamba mpaka niwe tumamu kwanza.

Sitosahau mkasa huo. Kiukweli bangi sio sigara.

........mwisho......
 
Back
Top Bottom