Nilivyoingiza 17.6M ndani ya mwaka mmoja na nusu, kwa biashara ya Mgahawa kwa mtaji wa kawaida kabisa

Mac Alpho

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
13,677
26,999
Habari zenu humu ndani?

si muandishi mzuri sana wa nyuzi humu jf ila leo nimejisikia kushare kitu kidogo na nyinyi juu ya biashara, nikiamini kwamba naweza kubadili fikira za baadhi ya vijana na wazee humu juu ya biashara.

Kwa taaluma mimi ni Civil Engineer na huwa napata vikazikazi ambavyo husukuma maisha yangu kwa kipato cha kawaida tu ila mwaka 2021 nilienda na jamaa yangu mmoja kama msindikizaji (kupoteza muda na kujifunza kitu kuhusu biashara ya dhahabu) sehemu moja inaitwa Dutwa ambako machimbo ya dhahabu yalizuka, kwa watu wa dhahabu watakuwa wanapajua vizuri. Sasa ile kufika kule nikakuta pilika za watu wengi balaa na huduma za jamii zinatolewa kwa bei ya juu kabisa, kwamfano watu walikuwa wanalala kwenye tugest tudogo twa mabati kwa 10K pre day so ukikuta mtu anavyumba 20 anakunja 200K yake kwa siku vizuri kabisa tena kwa kugombaniwa.

Nilivyorudi nyumbani Mwanza nikaa na kujiuliza sana mwisho wa siku nikaamua kuja na wazo la kwenda kuuza chakula kule, nilipojaribu kukusanya mawazo kutoka kwa watu nilikatishwa sana tamaa maana wengi walisema biashara kwenye migodi ya kulipuka huwa sio za kudumu kwana watu huhama mara kwa mara. Nilifikiria sana baadae nikaamua kujitoa mhanga, nikaandaa 2M kwaajili ya kujenga guesthouse za mabati na mgawaha na vyote nilivipa jina la CALFONIA HOLEL & CALFONIA GUEST (kwa wale waliowahi kufika dutwa namba moja watakuwa wanazijua), hazikuwa za kisasa sana ila kwa kiasi fulani niliset standards ukilinganisha na vimigahawa vingine vidogovidogo na guest za pale kihuduma.

MWANZO WA BIASHARA:
Nilinunua kila kitu kinachotakiwa kuanzisha mgahawa na ilinigharimu kama 1M nyingine, nilidhamiria kuuza kila kitu tofauti na wengine ambao walikariri chapati na chai, wali maharage nyama. Mimi nilitafuta mpishi mzuri kwaajili ya bites tu(chapati, Af cakes, na vitumbua na chai) ambae nilimlipa 10K siku, kisha nikatafuta pishi wa ugali na wengine wawili kwajili ya vitu vingine (Nyama, Samaki, wali, kuku, mbogamboga, maharage, maini...nk). Wahudumu nilitafuta wanne ambao niliwashonea sare kabisa.

Nilivyoanza sikutaka kucheka na nyani kwakua vitu vilikuwa standard nilikuja na bei ambazo hazikuwako kabisa. Kwamfano:-

Chapati 500Tsh (wao 300)
Andazi 500Tsh (wao 200)
Kitumbua 250Tsh (wao 200)
Wali nyama 3500Tsh (wao 2000)
Wali roast 4000Tsh (wao 3000)
Supu 2000Tsh (wao 1000)
Kipande kimoja cha nyama ya kuku ilikuwa ni 6000.
Samaki mzima nilikuwa nauza 10K hadi 12 wakati mimi nilikuwa nawachukulia 5k hadi 7K pale Ramadi, yani ni kwamba nilinunua vitu kwa bei ndogo na kuuza mara mbili yake. Nilizingatia usafi wa eneo langu na wahudumu wangu muda wote.

Siku ya kwanza hadi ya nne mauzo hayakuwa mazuri sana ila yalienda yanaongezeka,nadhani walikuwa wanapeana habari. Wiki ya pili nilianza kuuza hadi nilishangaa maana watu wa kule wakikaa kula hakuna kujibana, kwenye mgahawa wangu watu walipishana wengi sana ambao kwa mjini ili uwapate unahitaji uwe na mtaji mkubwa sana, nilipata tenda hadi kwenye ofisi za shamba ambako walikaa wale makota wa dhahabu. Mauzo ya chai na supu(7Kg) yalifika hadi 120K-140K kutokana na siku, mchana hadi usiku kwa pamoja nilikuwa nakusanya mauzo si chini ya 350K-400K (watu mtashangaa ila uhalisia ulinishangaza hata mimi)

Baada ya hesabu na kuwalipa wafanyakazi kukunja 60k-70k kama faida ilikuwa ni swala la kawaida kabisa. Nikikaa pale kama cashier kwa wiki tatu kisha baada nikaleta ndugu asimamie ili nirudi mwanza kuendelea na issue nyiingine ila akaanza kuniletea habari za faida 20K wakati mimi nishapiga hesabu za mbali kabisa, nilimtoa nirudi mwenyewe mzigoni(sikutaka kumpeleka wife kule mgodini) na mambo yakaendelea kuwa mzuri na mpaka mwisho wa mwezi ule nilikunja kama 1.2M benki. Biashara ya Guest Ilianza kuzorota maana ilifikia hatua chumba ikaw ni 3k baada ya guest kuwa nyingi.

CHANGAMOTO KUBWA:

Baada ya kama miezi miwili mambo yalianza kwenda kombo yani nikawa nauza msosi kwa raia wengi ila usiku wakati wa mahesabu hakuna hela hadi naanza kubembelezana na wafanyakazi kuwalipa hela, nikaanza kuchukua hela nje ya biashara ili kuinusuru, niliwaza labda naibiwa na wafanyazi ila kwakua mimi ndo nilikuwa mshika hela sikufikiria hivyo sana. Mimi huwa ni si muumini wa wa mambo ya tiba asilia na nilikuwa na msimamo sana ila baada ya kuona vyakula vinaisha ila hela haionekani jioni nikaamua kuomba ushauri, kila mtu akawa anadai bariadi wachawi sana na kwamba sitatoka na kitu nikizubaa. Nikaamua kumshirikisha mjomba wangu mmoja aliyekuwa anafanya kazi GGML ambaye alikuwa ni tajiri sana kutokana na biashara zake nyingi( RIP), alinisisitiza sana swala la kwenda kwa mganga nilikataa sana ila baadae niliingia kwenye line kisha akaniunganisha na mzee fulani hivi (sitaki maswali PM) nikaenda kuaguliwa japo kishingo upande, niliambiwa kuwa kulikuwa na chuma ulete kwenye biashara yangu na kwamba hela zikikuwa hazikai.

Niliporudi ofisini mambo yalichachamaa kaisi kwamba ikanilazimu kuongeza wahudumu kutoka wanne hadi 9 ili kuendana na kasi ya wateja, watu walitoka mbali (namba 2 na 7 kuja kula Calfonia ambayo ipo namba 1), kikuweli niliuza sana kisha baadae niliongeza biashara ya chips na nyama choma ambayo nayo ilinipa faida sana, swala la kuweka 90K- 120K kama faida likawa la kawaida sana au la lazima kabisa na kila mwisho wa mwezi benki ilibaki 900K- 1.4M (haikuwa constant kwasababu ya matumizi ya kijinga ikiwemo betting)

Hili swala la betting nilishashindwa kabisa kuliacha, na hata humu Jf mimi ni member mzuri tu wa jukwaa la mikeka😄.

Maisha yalikuwa mazuri sikuwa na hitaji kufanya kingine kabisa tofauti na mgahawa wangu, Mwanza nikawa naingia weekend (ijumaa- jpili) na nikifika na kula bata na marafiki na jamaa na kila aliyeuliza mishe yangu mpya nilimwambia nipo mgodini😄.

Baada ya mwaka mmoja mgodi ulienda unapunguza idadi ya watu walihamia Kakola na sikuwa na mpango wa kukimbizana nao hasa nikiangalia faida niliyoipata ndani ya muda huo, taratibu mauzo yalipungua mpaka ilipofikia mwezi wa tatu nikaamua kuibomoa nili nirudi kutulia nyumbani.

Mpaka nafunga biashara benki nilikuwa na 17.6M achilia mbali zile ambazo nilikuwa na kula au zile ambazo nilikuwa naliwa kwenyr betting.

NILICHOJIFUNZA

👉🏽Biashara ni location, huo mgahawa ukiuleta Mwanza mjini ungeonekana local kabisa na pengine nisingepata haya mauzo kabisa.

👉🏽Kwenye biashara utajikuta tu unaingia kwenye ushirikina kutokana na nature ya wateja ambao utawapokea (wapo wasio na nia nzuri ) unless uwe mcha Mungu thabiti kitu ambacho wengi hatuwezi.

👉🏽Ningekuja kuomba ushauri humu jf kwa mtaji ambao nilianza nao pale basi ningekata tamaa, maana humu nilishawahi kuona jamaa anasema hata mtaji wa 12M hauwezi kukupa faida ya 2M daaah😄.

👉🏽Kuna mishe zinaonekana za kijishusha viwango sana ila kiuhalisia ni zinalipa sana kama utaamua kuweka aibu pembeni.

NB; Sijaeleza yote, mengine nitakuwa naeleza huko chini kutokana na maswali ya wadau.
 
Mgahawa huwa naufikiria sana,kuna siku nitajaribu
Kikubwa ni location tu mkuu, kwasababu wali unaouzwa 1000 hapa ndo huohuo unaoenda kuuzwa 3000 sehemu nyingine na watu watakula bila kuhoji.

Kingine ukipata chimbo la kununua vitu kwa bei ya chini (jumla), unakuta samaki umemnunua 5000 halafu mwingine kamnunnua 7000 kisha wote mnenda kumuuza 12K huyu aliyenunua bei ndogo ni lazima apae tu, au wakati mwingine wewe unaamua kuuza 11k kwajili ya ushindani wa biashara na bado unabaki na faida kuliko anaeuza bei kubwa.

Biashara ni jinsi unavyonunua na sio jinsi unavyouza.
 
Back
Top Bottom