Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 6,956
- 12,409
Habari zenu wanaJF wenzangu
Kwanza natoa pole kwa familia ya mzee wetu hayati Edward Lowasa kwa kuondokewa na kipenzi chao, natoa pole pia kwa watanzania wenzangu kwa kuondokewa na aliewahi kuwa waziri mkuu wetu hayati Edward Lowasa.
Ki ukweli huu msiba umewashtua wengi wakiwemo ndugu zake, marafiki zake na hata maadui zake. Hivyo haishangazi kuona kila mtu anauzungumzia msiba huu.
Lakini pamoja na yote kuna hili jambo la mtu ambae aliwahi kuonesha chuki za wazi kwa hayati Edward Lowasa enzi za uhai wake, eti leo anajifanya ni mwema wake na rafiki yake ambae ameguswa mno na kifo chake 😳😳.
Hivi umeshawahi kuona wapi mtu ambae anakuombea mabaya, siku ukiyapata hayo mabaya eti anakuja tena kusikitika. Huu kama sio unafiki ni nini!!
Sawa inafahamika vizuri kwamba nguzo kuu za siasa ni (1) uongo (2) unafiki (3) na uzushi. Lakini inapotokea pale uliemzushia jambo amefariki, huku ukiwa unajua kuwa ulichomzushia hakina ukweli wowote, basi ni vizuri kuiomba msamaha familia yake ili kuwaondoa ile kumbukumbu mbaya walionayo kichwani mwao kuhusu uzushi uliomzushia ndugu au baba yao.
Kwenda kujing'ang'aniza kutoa machozi ili kuwahadaa baadhi ya watu wasiozijua nguzo za siasa nilizozitaja hapo juu, haitasaidia kuondoa dhana mbaya walizonazo watoto wa marehemu.
Nafikiri toka zamani kiongozi wetu alikuwa anataka Lowasa na yeye achomwe moto kama wanavyochomwa vibaka, ila Mungu hakuruhusu hilo litokee kamwe.
Picha zinaeleza kila kitu, na bahati nzuri mwenyewe anakiri kuwa kuna unafiki unafanyika msibani.
RIP ndugu Edward Lowasa
Mbele yako, nyuma yetu.