Nilikosea kumlipa?

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
7,638
4,522
Kuna siku nilitokewa na ndoto nzuri na ya kupendeza.Usiku huo niliota nipo na msichana mrembo wa kuvutia ambaye kila kijana pale mtaani alikuwa akitamani kuwa naye.Na mimi katika ndoto hiyo nilimfaidi barabara,maana ilikuwa nikiamka na kujisafisha narudi tena kulala, naye anakuja tena na ndoto inaendelea na tuna do tena,hali hiyo ilijirudia mara tatu mpaka kulipokucha.Asubuhi yake nikajiona kuwa sitamtendea haki dada wa watu endapo sitamlipa ujira wake kwa kazi aliyonitendea ukizingatia kuwa mimi pia sipendi vya bure.Basi mtoto wa kiume nikatoka mpaka anapoishi yule dada na kutoa kitita cha noti na kumkabidhi,akaniuliza unanipa pesa ya nini?Nikamsimulia ndoto yangu,We!Nilikoma jinsi alivyonitoa mbio siku hiyo mpaka nikajiuliza kosa langu lilikuwa lipi?Kumlipa ujira wake?Kuota ninado naye?Au ujasiri wangu wa kwenda kumsimulia ndoto yangu.
 
Watu wengine bwana...kwahiyo kwa akili zako zote unaona ulifanya kitu cha maana??Back to logic...uliyemtamani ni wewe...uliyeota ni wewe bila msaada kutoka kwake sasa unamlipa kwa lipi??
 
Watu wengine bwana...kwahiyo kwa akili zako zote unaona ulifanya kitu cha maana??Back to logic...uliyemtamani ni wewe...uliyeota ni wewe bila msaada kutoka kwake sasa unamlipa kwa lipi??

Hahahahahahahahah,umeniacha hoi kwa kicheko maana umekuwa mkali kama yule mdada alivyokuwa siku ile....
 
Hahahahaaah utakuwa uli do na jini mahaba lililokujia kwa sura ya huyo mrembo jirani yako. Pole kwa mkasa uliokukumba!!
 
Hahahahahahahahah,umeniacha hoi kwa kicheko maana umekuwa mkali kama yule mdada alivyokuwa siku ile....

Mhhu baki huko huko hoi mpaka nije kukuchukua!Alafu wewe si ajabu ulitegemea kwakujipeleka ndo atajilengesha!
 
mwanangu kama kawa na mahoka yako, hadithi ya leo ni kali ya kufungia mwaka! Heri ya mwaka mpya mkuu...
 
mwanangu kama kawa na mahoka yako, hadithi ya leo ni kali ya kufungia mwaka! Heri ya mwaka mpya mkuu...

Nimekuambia unitafutie ajira mkuu,maana niliyopitia katika haya mambo yanatosha kuandika best selling movie..........
 
oyaa black cat eeh mbona hii kimitego babuu
kwahiyo mchizi ulikuwa unajishindilia mibao kivyako duh
kizushi zushi lazima godoro lilikuwa na mitundu kibwena
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom