Nilijua ni wanawake tu, kumbe kuna wanaume wanatafuta wenza wa maisha na hawapati?

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,678
Zamani nilikua najua wanawake wanapitia mfadhaiko na depression akiona umri unaenda na hajapata Mwenza sahii wa kuishi nae/kuolewa nae, tumeshuhudia makanisani wakikusanyika Kuandika Maombi 12 huku ombi la kwanza ni kupata Mwanaume (kuolewa).

Nilishuhudia kongamano moja la vijana Mchungaji akauliza ambao wanatafuta wachumba wapite mbele kundi kubwa la wanaume wakaenda mbele nikawa najiuliza je ni nyege tu ndio zinawapeleka? Ili kuwadanganya mabinti walioko pale au ni kweli wamekosa wachumba wa kuoa?..

Kumbe haya mambo ni halisi, nilikua na Mchumba wangu tuliyedumu nae miaka mingi kidogo tokea tuko Shule na tuliweka malengo makubwa ya kuoana, tuliachana nae kwa amani hatukugombana, Kuna mistake moja iliyotokea.

Nilikuwa bado najitafuta baada ya kumaliza chuo, nilimpa yule Binti ujauzito nilikubali kuilea na kusisitiza asiitoe hiyo mimba Lakini Mama yake akalazimisha kuitoa mimba yangu kwa kigezo kwamba anataka kumrudisha Binti yake Shule, yule Mama nilimpa option kwamba kama anaona siwezi Lea ujauzito basi aende nyumbani kwa mzee wangu wakajadili, kipindi hicho nilikuwa bado mkoani, Lakini Mama yake akalazimisha kuutoa ujauzito Wangu, basi hiyo ndio sababu iliyonifanya niachane na yule Binti niliejuana nae takribani miaka 7 maana niliona huyo Mama ni chenga, itakuaje atoe ujauzito Wangu then baadae nirudi kwake nitoe tena mahari?

Tokea nimeachana na yule Binti nimeshapitia mahusiano mengi kidogo nikitafuta replacement, nikijiingiza kwenye mahusiano kwa ajili ya uchumba then Ndoa Lakini Kila mwanamke ninaempata naona chenga tu, Naona kama tutavurugana so nakua nasitisha mahusiano. Sijaona Bado ambae anaweza kumkaribia yule Binti kuanzia tabia, usikivu, utii n.k

Nimeamua kujipa likizo Kwenye Mahusiano nione hii game inaendaje, kuoa kipindi hiki imekua ni kipengele sana, mabinti wengi hawaeleweki, ukikutana na Binti age kuanzia 19 unakuta na yeye ana Ex wake, tena waliachana huku wanapendana 😁😁, ukikutana na Mwingine age 25 tena kapita chuo huyu ameshakutana na wajuba wakamiaji so hakuna kipya utakachokitoa 😁.

Mwisho kabisa nimeacha kushangaa Niliona kijana ambae kafikisha miaka 30-35 akisema amekosa Mwanamke wa kuoa, tusiwalaumu vijana ambao hawajaoa tulaumu jamii inayotengeneza hawa mabinti wa Sasa.
 
Back
Top Bottom