Elia
JF-Expert Member
- Dec 30, 2009
- 3,425
- 567
amekuwa anapeku sana simu yangu
anapekua mikoba yangu
anapekua nguo zangu
kila anachotaka najitahidi kumpatia hata nikishindwa huwa nimejitahidi sana
hapendi kusikia nimemsaidia mtu.. anadai sisi wanaume hatujui kutunza hela...
KILICHONIFANYA niandike hii thread leo ni hiki:
MOJA ya masharti au msimamo wangu ni kwamba sitaki kusikia jambo la ndani ya nyumba (tatizo) limepelekwa sehemu nyingine yeyote, tukishindwa kulitatua sisi wawili huko itakuwa ni kujichoresha tu. Hili nililiweka clear kwake naye akaliafiki na kuunga mkono..
MBILI sipendi kufichana fichana kama kunakitu kinafichwa basi sio kizuri, nalo lilikuwa clear na lilieleweka
Wiki iliyopita katika kupitia pitia simu yangu amekuta meseji alizoona zinautata akanipigia simu. akihitaji maelezo alikuwa MKALI sana...nilimpa maelezo ilikuwa ni hizi meseji za utani ambazo huwa tunatumiana. nilimueleza undani wa hizo meseji... niliona tatizo kwake ilikuwa imeandikwa na mwanamke.. nilimfafanulia ikiwa ni pamoja na kumpigia simu huyo muhusika mwisho nilimsifu kwa kitendo chake cha kuuliza kwangu ili apate ufafanuzi, nikimsihi asije peleka matatizo yake nje alinithibitishia kwamba hawezi kupeleka jambo kama hilo nje ovyo ilhali yeye ni mtu mzima sasa...
siku moja ikapita nikaitwa na mama mchungaji nikaona siwezi kwenda peke yangu nika mwambia anisindikize maana alikuwepo tu nyumbani. tulifika kwa mchungaji tukaongea sana baadae tukaishia kula chakula na juisi then nikaaga nikitegemea ataanzisha alichoniitia lakini sikupata kitu.. nikamuuliza una neno ulilo niitia? akasema basi tu niliwamiss,
tukaondoka nyumbani nika mwambie mwenzangu kwakweli mimi sijaipenda hii safari yetu nimeacha mambo yangu mengine nikidhani kuna la muhimu kama nilivyo itwa kumbe kuuza sura tu... akaniambia usichukie hata kusalimia ni jambo jema yakaishia hapo..
jana nilitumia simu yake kutuma meseji kwa mdogo wangu ikafeli na kujisevu(auto) kwenye draft.. nilipoweka vocha nikaenda kuitafuta kwenye draft ndipo nika kuta meseji mbili zilizo nikosesha usingizi usiku wa leo
1. .....naomba usimwambie habari ya zile meseji maana naona hali huku sio nzuri nitarekebisha mwenyewe.
2.......hiyo hela iliyobaki nitakumalizia mwezi wa kumi na moja
Nilipo angalia ile meseji ya kwanza ilikuwa ni siku nilipoitwa kwa mchungaji na ilitumwa kwa mama mchungaji.
Hii ya pili sikuielewa ikanibidi nizame kwenye mkoba wake (sio kawaida yangu) nikakuta mkataba wa manunuzi kwa jina lake akiwa amelipa milioni sita na laki nne zimebaki milioni moja na laki sita, nilishituka sana maana hana kipato kingine zaidi ya kunitegemea mimi
MWISHO nilihisi haniamini nikawa najitahidi kumfanyia kila anacho taka ikiwa ni pamoja na kumpeleka shule na kumpa nafasi ya kusimamia vibiashara ninavyofungua 80% vilikuwa vinakufa.. kwakweli nimekosa imani naye kabisa na usiku nimewaza mambo mengi sana