Nikiwa mkubwa nakata kuwa Rais

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,205
5,334
Kama kawaida ya Baba ukiwa na mwanao lazima utamuuliza maswali juu ya angependa kufanya kazi gani hapo baadaye na wakati huo ukitambua fika kuwa wakati mwingine mtoto huwa na matarajio makubwa mno katika ndoto zake kuliko uhalisia.

Nikiwa kama Baba leo nilikuwa nafanya mazungumzo ya mtu na mwanaye katika kujaribu kumpa nasaha na kumjenga katika ndoto zake hivyo nikaona siyo mbaya kushare na ninyi;

Baba; Mwanangu umeniambia hapo darasani kwenu wamekuchagua leo kuwa kiongozi wao, hivi unahisi wewe ni kiongozi mzuri?

Mtoto: Ndiyo, bila shaka.

Baba: Kwani sifa za kiongozi mwema ni zipi?

Mtoto: Kiongozi mzuri ana sifa kuu nne yaani mwema(benevolence), mnyoofu/mtenda haki (righteousness),mwenye heshima(courtesy) na hekima(wisdom)

Baba: Vyema mwanangu, lakini nina swali moja dogo kwako; Siku ukiwa mkubwa ungependa kuwa nani?

Mtoto: Rais

Baba: Nini maana ya kuwa Rais

Mtoto: Kuwa Rais ina maana ya kuwatawala watu.

Baba: Vipi kuhusu watu?

Mtoto: Watu ndiyo nguvu na msingi wa mtawala.

Baba: Na watu hao hao ndiyo wenye huitaji usiokoma, watahitaji maji, watahitaji zaidi na zaidi.
Watakombeleza mabakuli yao endapo Rais hatotimiza matakwa yao.
Watahigeuza nchi juu chini, watamuua Rais na kumweka Rais mwingine.

Mtoto: Baba nimeanza kuogopa.

Baba: Ndiyo mwanangu, siku zote husiwaamini watu.

Mtoto: Baba! (Kwa kuhamaki)

Baba: Nguvu ya nchi ni CHAKULA na nguvu ya Rais ni DOLA.

Mtoto: Sasa Baba!

Baba: Mamlaka ya Rais utumika dhidi ya maadui zake lakini pia wakati mwingine utumika dhidi ya watu wake.

Mtoto: Hata sielewi eti.

Baba: Ni kitu gani uelewi hapo?

Mtoto: Sasa kwanini Rais awe kinyume na watu wake?

Baba: Je, unataka kuwa mtu mzuri?

Mtoto: Ndiyo

Baba: Basi hutokuja kuwa Rais.

Mtoto: Lakini baba, nataka kuwa Rais mzuri.

Baba: Rais hatakiwi kuwa mzuri au mbaya.

Mtoto: Sasa hilo litawezekana vipi?

Baba: Iwe Rais ni Mzuri au Mbaya kikubwa ni machaguo yake.

Mtoto: Baba sasa kama wewe ndiyo Rais si unachagua tu chochote unachokitaka?

Baba: Kuchagua siyo juu yako wewe au mimi kuamua.

Mtoto: Sasa ikiwa Rais hawezi kuchagua sasa nani ufanya?

Baba: Mazingira au hali ndiyo uhamua ufanye maamuzi gani.

Mtoto: Kwahiyo siasa ndivyo ilivyo baba?

Baba: Je, wajua mwanangu ni jinsi gani siasa ina ukatili?

Mtoto: Hapana!

Baba: Siasa za ulimwengu wa leo ni siasa za jicho kwa jicho, Rais dhaifu uishi mithili ya samaki mdogo ndani ya bwawa kubwa asilojua ukomo wake.

Ndiyo maana mwanangu sitaki uje kuwa kama senene wa msimu wa masika asiyejua kiangazi wala kipupwe, anachojua ni maneno ya kitaalamu na kidini kuhusu maadili.

Mtoto: Kwa kusema hivyo Baba unamaanisha nini?

Baba: Nina maana ya kuwa; Ningependa Mwanangu awe ni Rais mashuhuri, mwenye nguvu na maamuzi.

Mtoto: Sawa Baba, ntabadilika ila sidhani kama nitatenda unyama kama marais wengine.

Baba: Unyama kwa Binadamu, HAUBADILIKI!!!

Mtoto: Sikuamini

Baba: Ni kwa sababu hakuna yeyote kati yetu anayeweza kubadilisha yaliyopita. Ni yajayo tu ndiyo yanaweza kubatilishwa.

Mtoto: Kwa hiyo unamaanisha mabadiliko yanawezekana?

Baba: Ndiyo mwanangu,"Kuishi au Kufa ni matakwa ya mbingu, lakini dhamiri mioyoni mwetu uishi"

*Listen Wisely!
 
Sijasoma Essay ila nimesoma kichwa cha Habari.


Hongera mkuu,Mungu akusimamie utimize ndoto zako ila naomba unikumbuke mimi UMUGHAKA niwe kama mpiga pasi wa nguo za Rais hapo Ikulu.
 
Sijasoma Essay ila nimesoma kichwa cha Habari.


Hongera mkuu,Mungu akusimamie utimize ndoto zako ila naomba unikumbuke mimi UMUGHAKA niwe kama mpiga pasi wa nguo za Rais hapo Ikulu.
Akili ndogo siku zote haiwezi balehe katika upeo mkubwa.
 
Back
Top Bottom