Nikijiuzulu hamtapata waziri kama mimi - Nchimbi

Alipokuwa anatangaza tume ya kuchunguza mauaji ya Marehemu D. Mwangosi, Nchimbi aliulizwa endapo yuko tayari kujiuzulu kama itabainika kwamba polisi ndio wanahusika na mauaji haya, akasema tena kwa kejeli 'nani ajiuzulu, nikijiuzulu mtapata wapi waziri kama mimi'.

My Take:
hizi ni dharau na kejeli kubwa sana kwa watanzania, sijui anaweza kutuambia lolote la maana alilofanya toka amewekwa kusimamia wizara hii, ninachokiona kwake ni kuratibu mauaji yanayoendeshwa na Polisi akishirikiana na Mwema. Nchimbi please swallow your pride and step down.

[JFMP3]Ni kweli kabisa akijiuzulu Dr. Nchimbi hatutapata waziri irresponsible kama yeye, tutampata waziri mweledi zaidi anayejua kusimamia haki!!!!!!![/JFMP3]
 
Tangu nchi hii ipate uhuru hakuna waziri kama MREMA enzi zake sasa mchimbi ni nani?
 
hii ina maanaisha kwamba nchi hii ni wajinga hakuna wasomi na ndio maana anpata kiburi cha kusema maneno kama haya.Ni kweli kwamba hatutapata waziri jasiri mwenye kuficha na kupotosha haki kama yeye hapa Tanzania kwa sababau zama za waongo na wapotoshaji zimekwisha.
 
Nakumbuka wakati wa awamu ya kwanza,Mwl. Nyerere akitambua umuhimu wa wizara hii na ile ya Ulinzi na JKT,alikua anawateua watu makini na wakati mwingine maafisa wa juu wa jeshi kuwa mawaziri! Mambo yameanza kuharibika awamu zilizofuata baada ya wanasiasa uchwara kama alivyo Nchimbi kuwa mawaziri. Nidhamu ya usimamizi ngazi ya Wizara imeshuka sana,maafisa wa juu Polisi wanateuliwa kwa ukada,siyo uwezo na matokeo nidhamu ya askari hakuna! Ukiziangalia picha zile Mwangosi akishambuliwa,huku afisa mmoja akijaribu kumkinga asiumizwe zaidi,lakini anaendelea kuadhibiwa mpaka kuuwawa mbele ya RPC inatosha kuchora picha kwamba kuanzia polisi wa ngazi ya chini mpaka juu hakuna nidhamu!

Unaweza tu ukaona tu udhaifu wa huyu bwana katika kufanya maamuzi. Juzi kati hapa kaenda Jangwani wakati wa maandamano ya waandishi wa habari kupinga mauaji ya Marehemu Mwangosi. Angekuwa vizuri above the shoulders angejiuliza haya:

a) Je maandamano yalikuwa dhidi ya nani? Wizara yake?? Serikali au kikundi kingine?
b) Kama alikuwa anaunga mkono maandamano mbona asishiriki maandamano na badala yake anataka kuyapokea na kuhutubia.
c) Hivi kweli alikuwa hajui ushiriki wa Police (wizara yake) ktk sakata zima? Je alitaka kujitenga na Police?
c)
 
Yeyote ajionaye bora kuliko wenzake; huyo ndo mbovu kuliko wote! Ujumbe huu umfikie mhusika!
 
Unaweza tu ukaona tu udhaifu wa huyu bwana katika kufanya maamuzi. Juzi kati hapa kaenda Jangwani wakati wa maandamano ya waandishi wa habari kupinga mauaji ya Marehemu Mwangosi. Angekuwa vizuri above the shoulders angejiuliza haya:

a) Je maandamano yalikuwa dhidi ya nani? Wizara yake?? Serikali au kikundi kingine?
b) Kama alikuwa anaunga mkono maandamano mbona asishiriki maandamano na badala yake anataka kuyapokea na kuhutubia.
c) Hivi kweli alikuwa hajui ushiriki wa Police (wizara yake) ktk sakata zima? Je alitaka kujitenga na Police?
c)

Awazalo mjinga kwamwe huwa halitokei! Ujumbe umfikie mhusika mkuu wa mauaji ya Mwanaharakati wetu - Mwandishi wa habari!
 
Back
Top Bottom