Nifanyeje

Fanta Face

Senior Member
Mar 10, 2011
138
21
Niliwahi kuwa na BF miaka kama mitano hivi imepita tulipendana sana lakini ikaja swala la dini tukashindwa kuoana yeye alioa dini yake, baada ya kutaka kuoa nilimwambia sina jinsi wazazi hawataki kusikia hiyo habari, nikamruhusu bila kinyongo hata harusi nilihudhuria, tulikuwa na mawasiliano ya kawaida tu bila kufanya chochote maana sipendi kumkosea mwanamke mwenzangu yaani mkewe, sasa limekuja swala kwamba mkewe kajifungua mtoto wa kike yapata miezi kama minne hivi mimi sikujua kumbe yule mwanaume kampa jina langu yule mtoto na mkewe ananifahamu, sasa yaani nimekaa katika mateso makubwa sana ni msg, simu za matusi kutoka kwa mkewe eti iweje mumewe ampe jina langu mtoto wake, niko njia panda mwenzenu, huyo mwanaume nimemuuliza anasema mimi ndio baba mwenye nyumba nimesema mtoto jina lake ni Fanta Face nimemaliza, nisaidieni ushauri wakubwa nifanyeje
 
badilisha simu,simple!
na ukate mawasiliano na huyo baba waache wajenge ama kuibomoa nyumba yao wenyewe ,
huyo mzee akikutafuta mueleze umeshindwa kuvumilia matusi ya mkewe.:ballchain:
 
badilisha simu,simple!
na ukate mawasiliano na huyo baba waache wajenge ama kuibomoa nyumba yao wenyewe ,
huyo mzee akikutafuta mueleze umeshindwa kuvumilia matusi ya mkewe.:ballchain:

Huyo baba hata simu zake wala msg siku hizi sizijibu kabisa wala sitaki mawasiliano nae tena. kubadilisha simu na hiyo ndo nimeweka kwenye CV natafutia kazi maana nimemaliza chuo tu bado sina kazi
 
Sasa wewe presha ya nini?Ondoa jinsi ya huyo mama kuwasiliana na wewe!
 
Huyo baba hata simu zake wala msg siku hizi sizijibu kabisa wala sitaki mawasiliano nae tena. kubadilisha simu na hiyo ndo nimeweka kwenye CV natafutia kazi maana nimemaliza chuo tu bado sina kazi
Unashindwa nini kublock simu na msg zake?Kama simu yako haina hizo option basi ignore msg na simu usipokee!Hamna kingine unachoweza kufanya!Na huyo mwanamke hanazo kweli...alishindwa nini kukataa hilo jina wakati linatolewa mpaka aje kutukana sasa hivi?
 
Simply ignore sms, dont answer calls, do not react in any way in case you meet (japo ngumu kidogo kibinadamu). Kubadilisha namba ya simu inaweza saidia. Lakini naona kuwa ni ghali sana kubadilisha namba ya simu kwa aijili ya mtu mmoja. Si ughali kipesa, ila kumbuka kuna watu kibao ulio wenye namba yako. kumpa taarifa mmojammoja ni kazi kidogo kwa mfano mi nina contacts za watu around mia saba na 80% ni active.
linganisha kati ya mawili.
 
unatumia cm ya aina gani?kama vp nikuelekeze namna ya kubloock cm zao zisiingie.
 
Unashindwa nini kublock simu na msg zake?Kama simu yako haina hizo option basi ignore msg na simu usipokee!Hamna kingine unachoweza kufanya!Na huyo mwanamke hanazo kweli...alishindwa nini kukataa hilo jina wakati linatolewa mpaka aje kutukana sasa hivi?

Asante kwa ushauri huu nitafanya simu anabadili namba kweli unakuta umepokea sms unakuta tu umesoma anyway let me try to as you said
 
Simply ignore sms, dont answer calls, do not react in any way in case you meet (japo ngumu kidogo kibinadamu). Kubadilisha namba ya simu inaweza saidia. Lakini naona kuwa ni ghali sana kubadilisha namba ya simu kwa aijili ya mtu mmoja. Si ughali kipesa, ila kumbuka kuna watu kibao ulio wenye namba yako. kumpa taarifa mmojammoja ni kazi kidogo kwa mfano mi nina contacts za watu around mia saba na 80% ni active.
linganisha kati ya mawili.

Will try my level best to do as you advice
 
Kama unaweza mwombe huyo mzee kama anakuheshimu kwa kukuondolea kero unayopata kutoka kwa mkewe...abadili jina la mwanawe!

Nimemwambia amekataa anasema yeye ndo baba mwenye nyumba na ameshasema kamaliza
 
Unahangaika na nini mama, kaa kimya tu wala usijibu lolote badae yatatulia, yanini kuyafikiria sana hayo? Just keep yourself busy!
 
Mapenzi mengine yanatia huzuni sana sasa kama alikuwa anakupenda sana kwanini hakukuoa???? Dini sio issue bana na wewe hukumpenda kabisa inaonyesha kuna mambo ya kusikiliza wazazi kweli siku hizi? Mie nimechoka kabisa.

Pole potezea tu jaribu sana kuignore
 
wanaume wengine wanapenda hovyohovyo........
sasa hapo atakuja kumwambia mwanae unajua nilikuwa nina girl friend nilimpenda sana dini ikatuzuia kuoana, nikaamua kukupa jina lake?
hee!!

And for you, hebu mu-ignore bana! au kama vipi mpe na yeye za usom kwani matusi huyajui? NikuPM namba ya DaSophy akupe shule.
 
Ushabiki umeuanza lini wewe???
 
pole sana dada kwa masumbufu yote haya. ndo dunia hii. Umesema ndo umemaliza chuo,na unatafuta kazi.. Kama sikosei sana kuna namna huyu mwanaume anakutoa, na kukusaidia hapa na pale.

Ingawa hujatoa maelezo ya kutosha hapa jamvini, lakini pia umegusia huyo mke wa jamaa kukujua sana. Ana haki kama mke, na inawezekana amesikia mengi kuhusu wewe na mume wake.

kwa sababu wameshafunga ndoa, usijiweke kwenye nafasi ya kuwa sababu ya ndoa ya watu kuwa na matatizo.
Acha kuwasiliana na mwanamume huyo mara moja, hata kama alikuwa BF wako. Fanya hivyo kwa usalama wako na future yako. Mpotezee, na ujitenge na ndoa ya watu. ni ngumu mwanzoni kwa kuwa umemzoea, but you have to do it. Heshima mbele kwenye ndoa za watu. usifupishe maisha yako, bado una future nzuri binti Fanta Face,
 
Back
Top Bottom