Nifanye nini ili kuzuia kutapika mara kwa mara

mangulumbwisi

Member
Apr 19, 2012
77
22
JF Dr
Nina ujauzito wa miezi mitatu, tatizo ninatapika mara kwa mara, nilienda hospital nikapewa dawa (NOSIC) nilimeza kwa muda wa wiki 1 zilisaidia kidogo ila tatizo linaendelea, pamoja kuwa nameza dawa lakini bado narudisha chenji ile mbaya mpaka hata kwenye daladala.Je nile nini matunda gani nizuie hii hali nateseka sana,NB nimepima Malaria nipo sawa, nimepima mkojo nipo sawa.nisaidieni nataseka jamani mwenzenu, kweli kazi ya uumbaji ni kubwa sana.
 
Kula sana,kula vyakula vibaya(asivyotaka mtoto),aleji husababisha kutapika.Kwa maelezo yako,pata chai iliyotiwa tangawiz
 
itaisha yenyewe vumilia tu ila kama its too much mimi nakumbuka nilipewa dawa flani sizikumbuki jina zilipunguza kutapika jaribu kuwaona madokta wa wanawake watakusaidia
 
Nosi ndiyo yenyewe na pia ondoa mawazo ! hiyo unaweza kunywa muda wote hadi utakapojifungua!

pia acha mawazo wewe kila ukiwaza kutapika lazima itakuwa hivyo.na pia uhutakiwi kula sana kula kiwango kidogo kidogo kwa interval fulani
 
Back
Top Bottom