Ni Zanzibar ipi wanaitaka?

Wakuu.
Nisaidieni hapa...Mwalimu Nyerere alikusudia nini aliposema hivi? JE wakati umefika?

"Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar. Wapendao Utanganyika watakuwa wazalendo zaidi, badala ya kuwa wasaliti, wakiazimia Afrika ya Mashariki iliyoungana kuwa Nchi Moja. kuliko Tanzania iliyotengana ikawa nchi mbili."

Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)

Tunajua kuwa tumeifufua EAC na pia kuna fast track ya kuelekea EA Federation. Leteni mawazo yenu.
Soma uk. 10-12.
 
Wakuu.
Nisaidieni hapa...Mwalimu Nyerere alikusudia nini aliposema hivi? JE wakati umefika?

"Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar. Wapendao Utanganyika watakuwa wazalendo zaidi, badala ya kuwa wasaliti, wakiazimia Afrika ya Mashariki iliyoungana kuwa Nchi Moja. kuliko Tanzania iliyotengana ikawa nchi mbili."

Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)

Tunajua kuwa tumeifufua EAC na pia kuna fast tract ya kuelekea EA Federation. Leteni mawazo yenu.
Soma uk. 10-12.

nafikiri lengo hasa la nyerere nikutaka kufuta kabisa dhana ya muungano wa serikali mbili na kuwa serikali moja. nikosolewe....
 
Wanaitaka nchi "yao" ya Zanzibar; Wanataka kurudia "utukufu wa Zanzibar" kwa kuwa hapa walipo sasa hawaoni manufaa "yoyote" kwa Zanzibar. Wanasema wanaitaka nchi yao waliyonyang'anywa na Wadanganyika (ati Watanganyika). Wanataka warudishiwe nchi yao waliyonyang'anywa na Nyerere na watu wa bara.

Ni Zanzibar ipi hiyo wanayoitaka?

  • Zanzibar ya historia ya kale (Zenj - nchi ya weusi?) ambayo ni zaidi ya visiwa vya Unguja na Pemba bali na mwambao wa Afrika ya Mashariki
  • Zanzibar ya Sultani(ambaye naye utawala wake ulizidi mipaka ya Unguja na Pemba)
  • Zanzibar ya Sultani chini ya Mwingereza
  • Zanzibar ya baada ya Uhuru na Sultani akiwa bado ni Mkuu wa Nchi na serikali ya Mseto
  • Zanzibar ya Mapinduzi kabla ya Muungano
  • Zanzibar "mpya" ambayo haijawahi kuwepo yaani ya baada ya muungano
Ni ipi hasa wanayoitaka? Ni ipi hasa Zanzibar "proper". Isije kuwa ni kama nchi ya ahadi ambayo iko katika fikra za watu tu lakini haijawahi kuwepo; yaani ile nchi imiminikayo maziwa na asali na kwamba watu wa bara na dunia nzima wanataka kuwanyang'anya Wazanzibari. Na labda hapa itabidi tulijibu swali pia kuwa Mzanzibari ni nani hasa?

Nakupongeza sana mwanakijiji kwa kuweka swali lenye akili. Hawa wazanzibar nafikiri hawajui wanachokidai, na hii ni kutokana na ukweli kuwa hawajitambui na hawaelewi tatizo lao hasa. Hali hii iliwahi kufanywa na wayahudi dhidi ya Yesu, wayahudi walihakikisha wanamuua Yesu hata kama hawatapata faida yeyote, ndiyo maana Yesu alipaza sauti na kusema "Baba wasamehe maana hawajui watendalo". Kwa mtu yeyote mwenye utimamu hasa mzanzibar sidhani kama anaweza kudai kitu ambacho kipo!! zanzibar ipo, rais wanaye mawaziri wanao na serikali inayotakiwa kisheria yote ipo. Tanganyika ndiyo haipo. hakuna serikali ya Tanganyika wala wabunge wala chochote kilichowekwa wazi kama cha Tanganyika. Waziri mkuu Pinda alishawaasa kuwa anayetaka kuvunja Muungano auvunje kinyume chake walighadhibishwa na neno hilo wakidai wamekashfiwa ndiyo maana nasema hawa watu ni wakorofi na mbaya zaidi hawajui na hakieleweki wanachokidai. Inawezekana kunawatu wanatumiwa na watu wakorofi ili kuvuruga nchi.

Kwangu mimi ni bahati mbaya sana kuwa na umoja na watu wa namna hii, watu wakulalama na kufukua vijineno kila kukicha. Muda umefika nafikiri viongozi wakae na kuwapa hawa watu hicho wanachokitaka, vinginevyo tutakaribisha alshababu na alkaida kwenye kisiwa chetu cha amani.

Mkuu Anold maneno yako ya mwisho ndio yamebainisha fikra zenu za wazi Watanganyika juu ya Zanzibat. Inakuwaje Zanzibar kuwa ni kisiwa chenu? Hizi ni fikra potofu lakini ndio zinazowapa kiburi, kejeli na dharau.

Hivi kama si kuendeleza ukoloni ni nini? Kwanini kama "muungano" huu ni mzuri, nchi nyengine jirani zaidi zisijiunge nanyi?

Nyinyi ni wavamizi na mnaikalia Zanzibar kwa nguvu kwa msaada wa baadhi ya viongozi wahafidhina wachache na msaada wa nguvu za dola.

Kuwa Zanzibar ni nchi yenye kila chake ni kiini macho tu lakini ukweli nyote mnaujua vizuri.

Wazanzibari hawana haja ya "muungano" wa namna hii na watandelea na jitihada zao za kutafuta ukombozi wa kweli na tunaamini iko siku mtaiacha Zanzibar nyinyi wenyewe.

Chuki zilizopandikizwa miongoni mwetu zinatoweka na sasa tuko tayari kuwakabili.

Zanzibar for Zanzibaris.
 
Tumeandika mara nyingi kuhusu sababu za wznz kutaka muungano uvunjike. Tumekuwa tukipewa sababu nyepesi nyepesi na wengine tumeeleza kuwa kujitenga ni haki yao na wafanye hivyo haraka kuelekea nchi ya kanaani yenye mito ya asali na maziwa.
Nimewahi kuandika kuwa wenzetu wa mzalendo forum sababu yao moja kubwa ni kutaka kufutiwa visa za Oman kwasababu wao wanaamini ni sehemu ya uarabuni, nikazogolewa!
Nimewahi kusema hakuna kisiwa chenye wakazi wa asili bali wote ni wahamiaji, nikajibiwa znz ilikuwepo kabla ya pori la Tanganyika, kwa maana ni nchi pekee iliyowahi kuwepo kabla ya zingine.
Nilisema wznz wapo wa kipilipili na kimanga, nikijabiwa hapana wao ni dugu moja.
Soma hii kitu kutoka raia mwema.

TEMBELEA mji wa Durban nchini Afrika Kusini, utakuta wakazi wanaojulikana kama "Wazanzibari"; kwa maana ile ile ya Uzanzibari wa Visiwa vya Unguja na Pemba, ingawa hawaishi Zanzibar wala si raia wa Tanzania.
Inawezekana usiamini hili na kujiuliza maswali mengi: "Je, Wazanzibari hawa ni wazawa wa masetla wa Kiislam karne zilizopita nchini Afrika Kusini kama walivyo Makaburu nchini humo? Kwanza mji wa Durban wenyewe si mji wa kale kiasi hicho; kwani ulianza mwaka 1834, vipi hii iwe kweli?
Kwa hiyo, Wazanzibari hawa ni kina nani? Walitoka wapi? Walifikaje Durban? Serikali ya Mapinduzi Zanzibar [SMZ] inawafahamu? Ni kina nani? Ni watoro/wakimbizi kutoka Zanzibar au jina hilo ni ngano tu za historia iliyosahaulika? Maswali haya yanataka utafiti makini kuelewa Wazanzibari hawa ni kina nani, na walifikaje huko.
Jamii inayojulikana jijini Durban na Chatsworth kama "Wazanzibari" nchini Afrika Kusini, ilionekana kwa mara ya kwanza katika eneo hilo mwaka 1873. Hawa ni wa vizazi vya watumwa wa kabila la Wamakua waliokombolewa na meli za vita za Waingereza katika Pwani ya Afrika Mashariki na bahari ya Sham; kisha wakapewa makao Zanzibar.
Wakati wakiishi hapo Zanzibar sambamba na Waswahili na Waislamu wa Kiarabu, waliweza kusilimishwa. Hata hivyo, chini ya mpango maalumu uliofikiwa kati ya Serikali ya Uingereza nchini Zanzibar na Gavana wa Jimbo la Natal nchini Afrika Kusini, ilionekana vyema watumwa hao huru wapelekwe Natal badala ya kubakia katika himaya ya Sultan wa Zanzibar kwa kuhofia kukamatwa na wafanyabiashara ya utumwa; licha ya kuwapa mkataba kati ya Uingereza na Sultan huyo mwaka 1873 kupiga marufuku biashara ya utumwa katika himaya yake.
Hiyo ni sababu moja; lakini kubwa zaidi ilikuwa ni upungufu wa nguvu kazi huko Natal kiasi cha kuhitaji wafanyakazi wa mashambani kutoka sehemu zingine. Kwa hiyo, watumwa hao huru walipelekwa huko kupunguza utegemezi wa nguvu kazi mashambani kutoka India ulioanza mwaka 1860.
Walipofika Natal waligundua kuwapo kwa Waislamu wenzao miongoni mwa Wahindi manamba waliofika kabla yao. Mikataba ya kazi ya Wazanzibari na Wahindi ilitofautiana kidogo. Wakati Wahindi walitakiwa kuchukua kitambulisho [kipande] kila waendako, Wazanzibari walikuwa huru kwenda wapendako.
Mikataba ya kazi ilikuwa ya miaka mitano mitano kwa Wahindi; kwa Wazanzibari ilikuwa mitatu. Hata hivyo, makundi yote mawili yalinyanyaswa vikali na watawala weupe.
Kwa hiyo, ni dhahiri kwamba makundi haya mawili yaliyofanyishwa kazi kwa pamoja chini ya msimamizi mmoja, yalijenga udugu na kushabihiana katika kunyanyaswa kwao. Mikataba yao ilipomalizika, Wazanzibari hao walifanya makao ya kudumu Durban na kuishi kama Waswahili.
Katika jamii za Kiswahili, kijiji ndicho kitovu cha jamii na ufuasi wa dini. Hivyo, utamaduni wa Kiswahili na dini ya Uislamu uliwajengea mshikamano wa kijamii kuwawezesha kujenga jamii yao pekee eneo la Kingsrest mjini Durban. Hapa walijishughulisha na kilimo cha bustani na ajira za majumbani kwa matajiri.
Kutokana na asili yao, yaani Zanzibar, iliyokuwa chini ya himaya ya Sultani, "Wazanzibari" hawa waliwekwa katika daraja la kijamii la "Kiasia" [Asiatic], na zaidi ya yote, imani yao ya Kiislamu iliwatofautisha na Wabantu wengine. Juhudi zilikuwa zikifanywa na Serikali ya Durban kutunga sheria watambuliwe kama Wabantu.
Jamii hii ya "Wazanzibari" iliendelea kujitambua kwa dhehebu la Ki-Sunni likizingatia "Shariah", kama njia ya kujichanganya na kujumuika na jamii zingine zilizotupwa nje ya utamaduni asilia.
"Wazanzibari" hawa, hata hivyo, waliendelea kupinga kuwekwa daraja moja na Wabantu kwa madai kwamba nchi yao ya asili - Zanzibar, kilikuwa kisiwa nje ya mpaka wa maji wa bara la Afrika. Na katika mkutano wa 1958 ulioandaliwa na Mfuko wa Juma Masjid Trust, hatimaye ilikubaliwa jamii hiyo ya Wazanzibari ipewe daraja la "Wenye rangi mbali mbali.
Baada ya mazungumzo marefu na Serikali kufuatia Sheria ya Uandikishaji watu Na. 30 ya 1950, mwaka 1961, ilikubaliwa daraja la Wazanzibari hao chini ya "rangi mbalimbali", lifafanuliwe kumaanisha "Waasia wengineo" [Other Asiatics].
Ni muhimu kufahamu kuwa "Wazanzibari" hawa walijitambua zaidi na asili ya Uarabu; licha ya rangi yao nyeusi. Hali hii iliwaepushia adha ya ukandamizaji na unyanyasaji waliofanyiwa Wabantu chini ya Serikali ya ubaguzi wa Makaburu.
Tishio lingine lililowakabili "Wazanzibari" juu ya kuwapo kwao Durban, ni lile kufuatia kutangazwa kwa Sheria ya Maeneo ya Vikundi [Groups Areas Act] ya mwaka 1957 ambapo eneo la Kingsrest walitengewa watu weupe. Hapa tena Mfuko wa Juma Masjid Trust uliingilia kati kuwatetea "Wazanzibari" na juhudi za kutaka wahamishiwe eneo la Zeekoevalleei zilishindwa.
Uhusiano wa mwanzo uliojengeka kati yao na Wahindi ulizidi kuimarika kwa vile waliabudu pamoja, walisherehekea Maulid pamoja, na walijumuika pamoja katika sherehe na vilio, na walitumia makaburi ya pamoja eneo la Kingsrest. Wakati mwingine "Wazanzibari" waliswali kwenye msikiti mkuu mtaa wa Grey, uliojengwa na Waislamu wa Kihindi waliofika hapo miaka ya 1860; na kufikia miaka ya 1880, walikuwa wafanyabiashara mahiri, ndipo wakaanzisha Mfuko wa Juma Masjid Trust.
Mwishoni mwa muongo, Waislamu wenzao wa Kihindi waliwapiga jeki "Wazanzibari" hao kwa kuwapatia mwalimu wa dini, Mustafa Osman, kutoka Visiwa vya Komoro ili akae nao na kuwasaidia kwa mambo ya kiroho.
Mwaka 1899 wafanyabiashara wa jamii ya Kihindi walianzisha mfuko mwingine wa Mohammedan Trust uliowawezesha kuwanunulia "Wazanzibari" hao ardhi eneo la Kingsrest na kuwahakikishia makazi ya kudumu. Mfuko huo uliweza pia kuwalipia kodi zote za serikali, kutunza msikiti, kuendesha madrassa, hivyo kuwahakikishia "Wazanzibari" hali ya usalama wa maisha.
Itakumbukwa pia kwamba jamii ya Kihindi ya Durban ndiyo iliyompokea mwanaharakati mashuhuri wa ukombozi wa India, hayati Mahatma Gandhi alipokimbilia na kukaa huko baada ya kuona India hakukaliki kutokana na harakati zake. Ni kutoka Afrika Kusini Mahatma Gandhi alirejea India akiwa na ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya na akaweza kuleta uhuru wa India.
Hata hivyo, mambo yaliwageuka mwaka 1938 ilipotungwa sheria iliyowatambua kama Waafrika na hivyo kutakiwa kulipa kodi ya kichwa kama Wabantu wengine na kubeba vitambulisho kila walikokwenda. Hata hivyo, kwa msaada wa Mfuko huo, "Wazanzibari" hao waliweza kupatiwa ardhi katika eneo la Wahindi la Chatsworth mwaka 1961, kwa sababu tu makundi haya yalishabihiana kidini.
Wazanzibari hawa walianza kuhamia Chastworth mwaka 1962 ambako wanaishi mpaka sasa. Utawatambua kwa tabia zao za ki-Makua, na wakati huo huo alama yao ya Uzanzibari kwa mivao kama vile kanzu, kikoyi, kofia, kimau, na kanga na kwamba wanazungumza Kiswahili fasaha cha kimwambao.
"Wazanzibari" hawa wanaheshimu swala tano za kila siku, na wanaitukuza na kuisherehekea siku ya Maulid katika nchi ambayo zaidi ya asilimia 90 ya raia wake ni Wakristo wenye mawazo kwamba Uislamu ni dini ya Kiarabu.
"Wazanzibari" wa Durban ni Wazanzibari wa asili ya Visiwa vya Zanzibari, kwa sababu hapo ndipo walipoanzia makazi kama watu huru. Na ndivyo ilivyokuwa kwa Wa-Creole wa Freetown huko Siera Leone waliopewa makao huko baada ya kukombolewa kutoka utumwani kuanzia mwaka 1808.
Idadi ya "Wazanzibari" wa Durban si kubwa sana katika nchi yenye Waislamu wanaounda asilimia moja tu ya wananchi wa Afrika Kusini na idadi ya waumini isiyoongezeka. Wameishi maisha ya kubaguliwa na utawala wa Makaburu [weupe], wakiumia bila uchungu kwa miaka mingi ya sera za kibaguzi wa rangi na ubaguzi wa kidini, kama walivyofanyia Wamarekani wenye asili ya Kiafrika kwa karne nyingi nchini Marekani.
Ubaguzi huu haukufichika miongoni mwa Makaburu. Mapema mwaka 1971, Mkuu wa Kanisa la Makaburu (The Dutch Reformed Church – DRC) Dakta Benjamin Vorster, nduguye aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Vorster, aliulizwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza [BBC], kama kulikuwa na uhalalisho wowote wa ki-Biblia juu ya ubaguzi huo, naye haraka haraka akajibu akisema: "Torati 32:8", inayoeleza kwamba, Mungu alipowagawia mataifa wana wa Israeli, alitaka wajitenge na wasioamini ili kutimiza mpango wake, na kwamba ubaguzi wa rangi kati ya weupe na wasio weupe ndio mfumo bora unaotakiwa na Mungu Afrika Kusini; na zaidi kwamba, Uislamu ni dini batili inayohatarisha Ukristo Afrika Kusini, Afrika na dunia nzima.
Vorster alitaja wazi wazi kuwa, "Wazanzibari" wa Durban ni hatari zaidi kuliko wahamiaji wa Kihindi [Wahindu] nchini Afrika Kusini.
Wazungu hawa [Makaburu] wanafananisha safari yao ndefu kutoka Kusini [Natal], kwa misafara, kuingia ndani ya Afrika Kusini karne ya 19, na safari ndefu [miaka 40] ya Waisraeli kutoka Misri kwenda nchi ya ahadi [Kanaani] yenye mito iliyofurika maziwa na asali.
Kitabu chao kikuu walichosoma kila siku ni Biblia, ni Agano la Kale, na mtazamo wao wa dunia umejengeka kwa misingi ya maandiko hayo. Hotuba zao mara nyingi ni kama unasikiliza manabii wa Agano la Kale. Waliamini kwamba kupinga ubaguzi wa rangi ni kupinga mpango wa Mungu, na hivyo ni kushindana na Mungu.
Msimamo mkali wa kidini wa "Wazanzibari" uliukera utawala wa kibaguzi wakaonekana kuwa watu wasiotakiwa na utawala huo katika nchi yenye idadi kubwa ya Wakristo kama hii. Mpaka sasa "Wazanzibari" wa Afrika Kusini ni watu baridi wanaoishi kwa kukumbuka asili yao daima – "Zanzibar".
Lakini mtu hapotezi asili yake kwa maana kufanya hivyo ni kupoteza utamaduni. Utamaduni ndio unaomfanya mtu aweze kuishi alivyo. Mtu asiyekuwa na utamaduni si kitu, bali ni sawa na mti usio na mizizi.
Huko Ethiopia ilibainika kuwa baadhi ya raia wa nchi hiyo walikuwa wa asili ya Kiyahudi wakijulikana kwa jina la kabila la "Wafalasha", nao hawakupenda kupoteza au kusahau asili yao; licha ya kukaa huko kwa karne nyingi. Na kwa sababu hiyo, Serikali ya Israeli ilichukua hatua za makusudi za kuwarejesha Uyahudi Wayahudi hao, chini ya mpango maalumu uliopewa jina la "Operation Moses", mwishoni mwa miaka ya 1970, na kuungana na Wayahudi wenzao.
Kwa kuwa "Wazanzibari" wa Durban wanainua macho kutazama na kuwakumbuka ndugu zao Wazanzibari wa Unguja na Pemba; na kwa kuwa damu ni nzito kuliko maji, tutarajie "Operesheni Zanzibar", mithili ya ya "Operation Moses" ya Mafalasha kurejea kwao Zanzibar?
Pengine ni vyema ikawa hivyo ili "Wazanzibari" hao wa Afrika Kusini wajumuike na ndugu zao wa Pemba na Unguja katika siasa za "ngangari na ngunguri", Visiwani humo; kwani ardhi yao bado inatosheleza kupokea wageni - "Wazanzibari" kwa "Wazanzibara".
 
Source?
 
Mkuu na wewe soma hili dude tafadhali:

Hii makala ya Joseph Mihangwa ukiisoma kwanza utaona kama inatoa muangaza kuhusu zama za Zanzibar ilipokuwa taifa lenye nguvu, na pengine kuwasifia Wazanzibari kuwa ni watu ambao wanaweza kuishi katika mateso na hatimae kuibuka na ushindi. Lakini mwisho wa makala yake hiyo Mihangwa kaleta taswira ya kama kulazimisha kuwa Wazanzibari hao wa Durban Afrika ya Kusini lazima warudi kuhamia kwao Zanzibar ya leo, yaani hii ya visiwani Unguja na Pemba. Kwa kumnukuu Mihangwa katumia maneno haya ninayomnukuu:

"Pengine ni vyema ikawa hivyo ili "Wazanzibari" hao wa Afrika Kusini wajumuike na ndugu zao wa Pemba na Unguja katika siasa za "ngangari na ngunguri", Visiwani humo; kwani ardhi yao bado inatosheleza kupokea wageni – "Wazanzibari" kwa "Wazanzibara"."

Na hapo ndipo panaposhangaza katika maelezo yake yote Mihangwa. Suala langu kubwa ni kwamba, kwani kila jamii ambayo kizazi chake kitakuwa kimepotea nchi za mbali ni lazima kirudi kwao ambako walihama au kulazimishwa kuhama?

Ikiwa hiyo ndio dhana anayoijenga kwa hao wanaoitwa "Wazanzibari" huko Durban, kwanini hafanyi pia utafiti Fiji pia ambako kuna watu weusi wengi na wanaodai kuwa asili yao walitoka Tanganyika. Jee na wao si itakuwa hivyo hivyo kuwa Watanganyika hao wa Fiji ni lini watarejea kwao?

Lakini si "Watanganyika" wa Fiji tu ni lini watarudi Tanganyika, si watu wanaweza kuuliza pia ni lini Wangoni watarudi kwao kwa asili huko Natal katika nchi ya Afrika ya Kusini ya leo ambako walikotokea na kuja kuhamia kusini ya Tanganyika katika miaka 1800 ambacho ni kipindi hicho hicho "Wazanzibari" aliowazungumza wanakisiwa kuhamia Durban? Au lini makabila mengi ya Tanganyika yatarudi kwao Kongo, Uganda, Msumbiji, Zambia, Afrika ya Kati,, Sudan, Ethiopia na kadhalika na kadhalika. Sijui hii makala kwa asili yake kaifanya utafiti au kaikopia tu kutoka pahala ilipoandikwa na mtu na kuiandika yeye kwa lugha ya Kiswahili, na kwavile na anajuwa kuandika kwa ufasaha na kufanya mtiririko mzuri wa maelezo, imependeza alaipoanza, lakini kaifuja mwishoni, kwani haikuwepo haja yoyote ile ya kufanye dhihaka za kijeuri ("sarcastic") katika kuielezea hadithi hiyo huko mwisho.

Inashangaza sana kufananisha kuwa "Wazanzibari" hao wa Durban wangehitaji waondoshwe huko Durban kuletwa Unguja na Pemba kwa mithili ya dharura kama amabavyo Waethiopia wenye asili ya Kiyahudi (Mafalasha) walipoondoshwa Ethiopia wakati wa njaa ya mwaka 1984 kwa "Operation Moses". Suala kwani hao Wazanzibari walioko Durban wana shida gani? Hawakuondoka wakati huo wa ubaguzi wakaondoke leo? Wakitaka kutembea kwani si wanaweza kuja kutembea wenyewe Zanzibar? Kwani Mihangwa anamjua kila "Mzanzibari" wa Durban hata akisie kuwa hakuna aliyewahi kuja Zanzibar (Unguja na Pemba) kwa kutembea kwa hiari?

Hadithi ni nzuri na inaonyesha mahusiano ya binaadamu na kuashiria matukio mbali mbali katika historia ama yalikuwa mabaya au mazuri yameweza kuwakutanisha wanaadamu na kuwaunganisha kidugu, hilo tu ndio lililokuwa muhimu. Haya ya kusema lini watarudi kwao Zanzibar imehusu nini, kwani wamehamia huko Afrika ya Kusini leo na jana?

Kama wote ambao wazazi wao waliohama makwao makarne mengi yaliyopita, wakitakiwa vizazi vyao vya leo vilazimike kurudi huko makwao kwa asili ambako mababu wa mababu zao walikotoka, jee dunia ya leo katika nchi mbali mbali itakuwa ya namna gani?

Mihangwa huwa namuona mahiri anapochambua sheria za Muungano, lakini ananisikitisha jinsi anavyoshindwa kuelewa ugugmu wa masuala ya uhamiaji, ustawi wa jamii na maamuzi binafsi ya wahamiaji na kuyaandika kwa vipimo vyake. Kwa mbinu hiyo anayoitaka Mihanga ya kuwa watu lazima warudi makwao kwa asili, ni wazi haiendani na wakati huu wa karne ya ishini na moja ya utandawazi na ongezeko la uhamiaji wa hiari wa kimataifa.

Nassor Seif Nassor
 
Tumeandika mara nyingi kuhusu sababu za wznz kutaka muungano uvunjike. Tumekuwa tukipewa sababu nyepesi nyepesi na wengine tumeeleza kuwa kujitenga ni haki yao na wafanye hivyo haraka kuelekea nchi ya kanaani yenye mito ya asali na maziwa.
Nimewahi kuandika kuwa wenzetu wa mzalendo forum sababu yao moja kubwa ni kutaka kufutiwa visa za Oman kwasababu wao wanaamini ni sehemu ya uarabuni, nikazogolewa!
Nimewahi kusema hakuna kisiwa chenye wakazi wa asili bali wote ni wahamiaji, nikajibiwa znz ilikuwepo kabla ya pori la Tanganyika, kwa maana ni nchi pekee iliyowahi kuwepo kabla ya zingine.
Nilisema wznz wapo wa kipilipili na kimanga, nikijabiwa hapana wao ni dugu moja.
Soma hii kitu kutoka raia mwema.

TEMBELEA mji wa Durban nchini Afrika Kusini, utakuta wakazi wanaojulikana kama “Wazanzibari”; kwa maana ile ile ya Uzanzibari wa Visiwa vya Unguja na Pemba, ingawa hawaishi Zanzibar wala si raia wa Tanzania.
Inawezekana usiamini hili na kujiuliza maswali mengi: “Je, Wazanzibari hawa ni wazawa wa masetla wa Kiislam karne zilizopita nchini Afrika Kusini kama walivyo Makaburu nchini humo? Kwanza mji wa Durban wenyewe si mji wa kale kiasi hicho; kwani ulianza mwaka 1834, vipi hii iwe kweli?
Kwa hiyo, Wazanzibari hawa ni kina nani? Walitoka wapi? Walifikaje Durban? Serikali ya Mapinduzi Zanzibar [SMZ] inawafahamu? Ni kina nani? Ni watoro/wakimbizi kutoka Zanzibar au jina hilo ni ngano tu za historia iliyosahaulika? Maswali haya yanataka utafiti makini kuelewa Wazanzibari hawa ni kina nani, na walifikaje huko.
Jamii inayojulikana jijini Durban na Chatsworth kama “Wazanzibari” nchini Afrika Kusini, ilionekana kwa mara ya kwanza katika eneo hilo mwaka 1873. Hawa ni wa vizazi vya watumwa wa kabila la Wamakua waliokombolewa na meli za vita za Waingereza katika Pwani ya Afrika Mashariki na bahari ya Sham; kisha wakapewa makao Zanzibar.
Wakati wakiishi hapo Zanzibar sambamba na Waswahili na Waislamu wa Kiarabu, waliweza kusilimishwa. Hata hivyo, chini ya mpango maalumu uliofikiwa kati ya Serikali ya Uingereza nchini Zanzibar na Gavana wa Jimbo la Natal nchini Afrika Kusini, ilionekana vyema watumwa hao huru wapelekwe Natal badala ya kubakia katika himaya ya Sultan wa Zanzibar kwa kuhofia kukamatwa na wafanyabiashara ya utumwa; licha ya kuwapa mkataba kati ya Uingereza na Sultan huyo mwaka 1873 kupiga marufuku biashara ya utumwa katika himaya yake.
Hiyo ni sababu moja; lakini kubwa zaidi ilikuwa ni upungufu wa nguvu kazi huko Natal kiasi cha kuhitaji wafanyakazi wa mashambani kutoka sehemu zingine. Kwa hiyo, watumwa hao huru walipelekwa huko kupunguza utegemezi wa nguvu kazi mashambani kutoka India ulioanza mwaka 1860.
Walipofika Natal waligundua kuwapo kwa Waislamu wenzao miongoni mwa Wahindi manamba waliofika kabla yao. Mikataba ya kazi ya Wazanzibari na Wahindi ilitofautiana kidogo. Wakati Wahindi walitakiwa kuchukua kitambulisho [kipande] kila waendako, Wazanzibari walikuwa huru kwenda wapendako.
Mikataba ya kazi ilikuwa ya miaka mitano mitano kwa Wahindi; kwa Wazanzibari ilikuwa mitatu. Hata hivyo, makundi yote mawili yalinyanyaswa vikali na watawala weupe.
Kwa hiyo, ni dhahiri kwamba makundi haya mawili yaliyofanyishwa kazi kwa pamoja chini ya msimamizi mmoja, yalijenga udugu na kushabihiana katika kunyanyaswa kwao. Mikataba yao ilipomalizika, Wazanzibari hao walifanya makao ya kudumu Durban na kuishi kama Waswahili.
Katika jamii za Kiswahili, kijiji ndicho kitovu cha jamii na ufuasi wa dini. Hivyo, utamaduni wa Kiswahili na dini ya Uislamu uliwajengea mshikamano wa kijamii kuwawezesha kujenga jamii yao pekee eneo la Kingsrest mjini Durban. Hapa walijishughulisha na kilimo cha bustani na ajira za majumbani kwa matajiri.
Kutokana na asili yao, yaani Zanzibar, iliyokuwa chini ya himaya ya Sultani, “Wazanzibari” hawa waliwekwa katika daraja la kijamii la “Kiasia” [Asiatic], na zaidi ya yote, imani yao ya Kiislamu iliwatofautisha na Wabantu wengine. Juhudi zilikuwa zikifanywa na Serikali ya Durban kutunga sheria watambuliwe kama Wabantu.
Jamii hii ya “Wazanzibari” iliendelea kujitambua kwa dhehebu la Ki-Sunni likizingatia “Shariah”, kama njia ya kujichanganya na kujumuika na jamii zingine zilizotupwa nje ya utamaduni asilia.
“Wazanzibari” hawa, hata hivyo, waliendelea kupinga kuwekwa daraja moja na Wabantu kwa madai kwamba nchi yao ya asili - Zanzibar, kilikuwa kisiwa nje ya mpaka wa maji wa bara la Afrika. Na katika mkutano wa 1958 ulioandaliwa na Mfuko wa Juma Masjid Trust, hatimaye ilikubaliwa jamii hiyo ya Wazanzibari ipewe daraja la “Wenye rangi mbali mbali.
Baada ya mazungumzo marefu na Serikali kufuatia Sheria ya Uandikishaji watu Na. 30 ya 1950, mwaka 1961, ilikubaliwa daraja la Wazanzibari hao chini ya “rangi mbalimbali”, lifafanuliwe kumaanisha “Waasia wengineo” [Other Asiatics].
Ni muhimu kufahamu kuwa “Wazanzibari” hawa walijitambua zaidi na asili ya Uarabu; licha ya rangi yao nyeusi. Hali hii iliwaepushia adha ya ukandamizaji na unyanyasaji waliofanyiwa Wabantu chini ya Serikali ya ubaguzi wa Makaburu.
Tishio lingine lililowakabili “Wazanzibari” juu ya kuwapo kwao Durban, ni lile kufuatia kutangazwa kwa Sheria ya Maeneo ya Vikundi [Groups Areas Act] ya mwaka 1957 ambapo eneo la Kingsrest walitengewa watu weupe. Hapa tena Mfuko wa Juma Masjid Trust uliingilia kati kuwatetea “Wazanzibari” na juhudi za kutaka wahamishiwe eneo la Zeekoevalleei zilishindwa.
Uhusiano wa mwanzo uliojengeka kati yao na Wahindi ulizidi kuimarika kwa vile waliabudu pamoja, walisherehekea Maulid pamoja, na walijumuika pamoja katika sherehe na vilio, na walitumia makaburi ya pamoja eneo la Kingsrest. Wakati mwingine “Wazanzibari” waliswali kwenye msikiti mkuu mtaa wa Grey, uliojengwa na Waislamu wa Kihindi waliofika hapo miaka ya 1860; na kufikia miaka ya 1880, walikuwa wafanyabiashara mahiri, ndipo wakaanzisha Mfuko wa Juma Masjid Trust.
Mwishoni mwa muongo, Waislamu wenzao wa Kihindi waliwapiga jeki “Wazanzibari” hao kwa kuwapatia mwalimu wa dini, Mustafa Osman, kutoka Visiwa vya Komoro ili akae nao na kuwasaidia kwa mambo ya kiroho.
Mwaka 1899 wafanyabiashara wa jamii ya Kihindi walianzisha mfuko mwingine wa Mohammedan Trust uliowawezesha kuwanunulia “Wazanzibari” hao ardhi eneo la Kingsrest na kuwahakikishia makazi ya kudumu. Mfuko huo uliweza pia kuwalipia kodi zote za serikali, kutunza msikiti, kuendesha madrassa, hivyo kuwahakikishia “Wazanzibari” hali ya usalama wa maisha.
Itakumbukwa pia kwamba jamii ya Kihindi ya Durban ndiyo iliyompokea mwanaharakati mashuhuri wa ukombozi wa India, hayati Mahatma Gandhi alipokimbilia na kukaa huko baada ya kuona India hakukaliki kutokana na harakati zake. Ni kutoka Afrika Kusini Mahatma Gandhi alirejea India akiwa na ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya na akaweza kuleta uhuru wa India.
Hata hivyo, mambo yaliwageuka mwaka 1938 ilipotungwa sheria iliyowatambua kama Waafrika na hivyo kutakiwa kulipa kodi ya kichwa kama Wabantu wengine na kubeba vitambulisho kila walikokwenda. Hata hivyo, kwa msaada wa Mfuko huo, “Wazanzibari” hao waliweza kupatiwa ardhi katika eneo la Wahindi la Chatsworth mwaka 1961, kwa sababu tu makundi haya yalishabihiana kidini.
Wazanzibari hawa walianza kuhamia Chastworth mwaka 1962 ambako wanaishi mpaka sasa. Utawatambua kwa tabia zao za ki-Makua, na wakati huo huo alama yao ya Uzanzibari kwa mivao kama vile kanzu, kikoyi, kofia, kimau, na kanga na kwamba wanazungumza Kiswahili fasaha cha kimwambao.
“Wazanzibari” hawa wanaheshimu swala tano za kila siku, na wanaitukuza na kuisherehekea siku ya Maulid katika nchi ambayo zaidi ya asilimia 90 ya raia wake ni Wakristo wenye mawazo kwamba Uislamu ni dini ya Kiarabu.
“Wazanzibari” wa Durban ni Wazanzibari wa asili ya Visiwa vya Zanzibari, kwa sababu hapo ndipo walipoanzia makazi kama watu huru. Na ndivyo ilivyokuwa kwa Wa-Creole wa Freetown huko Siera Leone waliopewa makao huko baada ya kukombolewa kutoka utumwani kuanzia mwaka 1808.
Idadi ya “Wazanzibari” wa Durban si kubwa sana katika nchi yenye Waislamu wanaounda asilimia moja tu ya wananchi wa Afrika Kusini na idadi ya waumini isiyoongezeka. Wameishi maisha ya kubaguliwa na utawala wa Makaburu [weupe], wakiumia bila uchungu kwa miaka mingi ya sera za kibaguzi wa rangi na ubaguzi wa kidini, kama walivyofanyia Wamarekani wenye asili ya Kiafrika kwa karne nyingi nchini Marekani.
Ubaguzi huu haukufichika miongoni mwa Makaburu. Mapema mwaka 1971, Mkuu wa Kanisa la Makaburu (The Dutch Reformed Church – DRC) Dakta Benjamin Vorster, nduguye aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Vorster, aliulizwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza [BBC], kama kulikuwa na uhalalisho wowote wa ki-Biblia juu ya ubaguzi huo, naye haraka haraka akajibu akisema: “Torati 32:8”, inayoeleza kwamba, Mungu alipowagawia mataifa wana wa Israeli, alitaka wajitenge na wasioamini ili kutimiza mpango wake, na kwamba ubaguzi wa rangi kati ya weupe na wasio weupe ndio mfumo bora unaotakiwa na Mungu Afrika Kusini; na zaidi kwamba, Uislamu ni dini batili inayohatarisha Ukristo Afrika Kusini, Afrika na dunia nzima.
Vorster alitaja wazi wazi kuwa, “Wazanzibari” wa Durban ni hatari zaidi kuliko wahamiaji wa Kihindi [Wahindu] nchini Afrika Kusini.
Wazungu hawa [Makaburu] wanafananisha safari yao ndefu kutoka Kusini [Natal], kwa misafara, kuingia ndani ya Afrika Kusini karne ya 19, na safari ndefu [miaka 40] ya Waisraeli kutoka Misri kwenda nchi ya ahadi [Kanaani] yenye mito iliyofurika maziwa na asali.
Kitabu chao kikuu walichosoma kila siku ni Biblia, ni Agano la Kale, na mtazamo wao wa dunia umejengeka kwa misingi ya maandiko hayo. Hotuba zao mara nyingi ni kama unasikiliza manabii wa Agano la Kale. Waliamini kwamba kupinga ubaguzi wa rangi ni kupinga mpango wa Mungu, na hivyo ni kushindana na Mungu.
Msimamo mkali wa kidini wa “Wazanzibari” uliukera utawala wa kibaguzi wakaonekana kuwa watu wasiotakiwa na utawala huo katika nchi yenye idadi kubwa ya Wakristo kama hii. Mpaka sasa “Wazanzibari” wa Afrika Kusini ni watu baridi wanaoishi kwa kukumbuka asili yao daima – “Zanzibar”.
Lakini mtu hapotezi asili yake kwa maana kufanya hivyo ni kupoteza utamaduni. Utamaduni ndio unaomfanya mtu aweze kuishi alivyo. Mtu asiyekuwa na utamaduni si kitu, bali ni sawa na mti usio na mizizi.
Huko Ethiopia ilibainika kuwa baadhi ya raia wa nchi hiyo walikuwa wa asili ya Kiyahudi wakijulikana kwa jina la kabila la “Wafalasha”, nao hawakupenda kupoteza au kusahau asili yao; licha ya kukaa huko kwa karne nyingi. Na kwa sababu hiyo, Serikali ya Israeli ilichukua hatua za makusudi za kuwarejesha Uyahudi Wayahudi hao, chini ya mpango maalumu uliopewa jina la “Operation Moses”, mwishoni mwa miaka ya 1970, na kuungana na Wayahudi wenzao.
Kwa kuwa “Wazanzibari” wa Durban wanainua macho kutazama na kuwakumbuka ndugu zao Wazanzibari wa Unguja na Pemba; na kwa kuwa damu ni nzito kuliko maji, tutarajie “Operesheni Zanzibar”, mithili ya ya “Operation Moses” ya Mafalasha kurejea kwao Zanzibar?
Pengine ni vyema ikawa hivyo ili “Wazanzibari” hao wa Afrika Kusini wajumuike na ndugu zao wa Pemba na Unguja katika siasa za “ngangari na ngunguri”, Visiwani humo; kwani ardhi yao bado inatosheleza kupokea wageni - “Wazanzibari” kwa “Wazanzibara”.

JIBU HILO:

Prof.Ibrahim Noor 07/05/2011 kwa 7:15 mu · Jibu
Waalaykum salaam,
Kweli Joseph Mihangwa ni mwandishi mzuri akiandika juu ya maudhui fulani kama hayo ya katiba ya muungano, lakini katika makala haya kajikanyaga mara nyingi katika hoja na mantiki. Kwa mfano, ametuelezea kuwa hao “Wazanzibari” ambao hawasemi Kiswahili na ni watu wenye asili ya Kimakua. Jee, chimbuko la Wamakua ni Zanzibar?
Pili, Waingereza walipoyateka majahazi ya waharamia yaliyopakia watumwa dhidi ya mkataba baina ya Sultani wa Zanzibar na Waingereza kuanzia 1822 — ambao wenye chuki zao dhidi ya Waislamu hawautaji — na mikataba ya baadaye, watumwa hao waliachwa huru na kutafutiwa mahala wakae na kuendesha maisha yao. Wakati huohuo, wamishinari wa Kiingereza waliwavama na kuwatia katika Ukristo. Hivyo ndivyo walivyofanyiwa watumwa walioachwa huru na kupewa ardhi, kwa mfano ile ya Frere Town, Kenya, kama akina Mbotela na wengineo. James Juma Mbotela aliwatumikia vizuri sana Wamishinari hadi kuandika kitabu kiitwacho “Uhuru wa Watumwa” ambacho hakina lengo jingine ila kuonesha kuwa Duniani hakuna watu makhabithi na wabaya zaidi ya Waswahili-Waislamu. Kwa hivyo kuwa hao Wamakuwa walikuwa ni watumwa walioachiwa huru Zanzibar kwa muda mfupi waliokaa Zanzibar na katika muda huo wakawa Waislamu ni la hadithi ya paukwa pakawa. Hii madda ya utumwa ili walaumiwe Waislamu milele, ni katika hizo propaganda za wamishinari ambazo mpaka leo zinaendelezwa na kila kukicha huongezwa achari na sukari kuliko katika michezo ya Kihindi. Rafiki yangu mmoja wa Kiafrika aliyeniletea makala haya yanayofuata kukhusu Bi Khole, ameniandikia kuwa “If this is true, then this story about Bi Khole is awfully more powerful than Mandingo!” Sasa tafuteni mchezo wenye jina la “Mandingo” muuangalie wenyewe vipi binadamu wanavyopanga kichwani mwao wayapendayo.
Inaingia akilini zaidi kuwa hao Wamakuwa wanaojulikana kama ni “Wazanzibari” walipelekwa Afrika ya kusini kama walivyopelekwa huko Wahindi, Wamaley na wengineo kutiwa katika utumwa mambo leo wa kufanyishwa kazi kama watumwa kwa jina la vibarua. Zanzibar ilikuwa ipigwe vita na Mfaransa wakati wa Sayyid Said kwa sababu iliwakatalia kuchukua “vibarua” wa aina hiyo kuwapeleka katika mashamba yao yalioko katika koloni zao Wafaransa.
Kwa hivi sasa someni moja katika hadithi nyingi za kipaukwa pakawa zenye lengo la kuwapumbaza wataalii na kuwala pesa zao. Kwa wasiojua Kiingereza na kwa mukhtasari, hadithi inatuelezea kuwa Bi. Khola eti alikuwa hatoshelezeki ila aingiliwe na idadi kubwa ya watumwa ndipo uchu wake umtoke! Na hakutosheka! Na ikisha kila mtumwa aliyemuingilia hum-uwa. Jee amelipenda ndude na mikato ya mtumwa, hiyo si itakuwa khasara kubwa kwake! Mradi hawa magaidi na njaa zao hawana kikomo katika kupanga hadithi zao za kiwehu na Zanzibar imekaa kimyaa haina khabari ya athari za mambo haya katika mustaqbal wake! Khasara ilioje!

souce:mzalendo.net.
 
Kwanza nikumbushe kuw nimeweka Source: Gazeti la Raia mwema, na J . Mihangwa.

Pili, Mihangwa ameandika kama ilivyo kawaida yake ya kuweka wazi kile alichokifanyia utafiti wa kitaaluma. Nashangaa wznz wanamuona hafai lakini wakati akiandika yale wanayopenda kuyasikia anafaa! Kigeugeu!!

Tatu, ameweka kichwa cha habari chenye kutamananisha kama sehemu ya uandishi, na hilo amefanikiwa. Sidhani kuwa alikuwa na maana halisi ya kurudi akijua kuwa wapo south Africa kwa karne. Hoja yake kubwa ambayo ninyi wachangiaji wznz mnataka kuikwepa ni ukweli kuwa wznz hawajitambulishi kama waafrika, hata inapotokea hivyo kwao ni unyonge. Wao wanadhani ni sehemu ya wanadamu bora wa Uarabuni, na hili hawalisemi hadharani bali nyuma ya mgongo wa muungano.
Mihangwa ametoa ushadhidi wa vitambulisho kuwa wao walikuwa bora zaidi kuitwa 'Asiatic' kuliko wamatumbi. Ni dhana hiyo bado inawasumbua wenzetu na kwahiyo muungano ni bangusilo tu, kinachotafutwa ni nasaba iwe ya kweli au kupandikiza lakini itoke sehemu bora hata kama rangi na nywele zitakuwa na mushkeli, bora nusu ya shari kuliko shari kamili..

Article ya Mihangwa pia imeonyesha kuwa hakuna mtu anayeweza kusema asili yake ni znz!! hakuna watu wa kisiwa wenye asili ya kisiwa hicho, wote ni wahamiaji kwa hiyo dhana ya kuwa znz ilikuwepo kabla ya nchi zingine ni aina ya uelewa wenye matatizo.
Hoja si Mihangwa kama mwandishi bali yale aliyoandika, kama kuna mtu anajua jingine kuhusu wznz walowezi (ukiita watumwa utakuwa unatukana) kule S.A weka hapa.
 
Kwanza nikumbushe kuw nimeweka Source: Gazeti la Raia mwema, na J . Mihangwa.

Pili, Mihangwa ameandika kama ilivyo kawaida yake ya kuweka wazi kile alichokifanyia utafiti wa kitaaluma. Nashangaa wznz wanamuona hafai lakini wakati akiandika yale wanayopenda kuyasikia anafaa! Kigeugeu!!

Tatu, ameweka kichwa cha habari chenye kutamananisha kama sehemu ya uandishi, na hilo amefanikiwa. Sidhani kuwa alikuwa na maana halisi ya kurudi akijua kuwa wapo south Africa kwa karne. Hoja yake kubwa ambayo ninyi wachangiaji wznz mnataka kuikwepa ni ukweli kuwa wznz hawajitambulishi kama waafrika, hata inapotokea hivyo kwao ni uonyonge. Waoa wanadhani ni sehemu ya wanadamu bora wa Uarabuni, na hili hawalisemi hadharani bali nyuma ya mgongo wa muungano.
Mihangwa ametoa ushadhidi wa vitambulisho kuwa wao walikuwa bora zaidi kuitwa 'Asiatic' kuliko wamatumbi. Ni dhana hiyo bado inawasumbua wenzetu na kwahiyo muungano ni bangusilo tu, kinachotafutwa ni nasaba iwe ya kweli au kupandikiza lakini itoke sehemu bora hata kama rangi na nywele zitakuwa na mushkeli, bora nusu ya shari kuliko shari kamili..

Article ya Mihangwa pia imeonyesha kuwa hakuna mtu anayeweza kusema asili yake ni znz!! hakuna watu wa kisiwa wenye asili ya kisiwa hicho, wote ni wahamiaji kwa hiyo dhana ya kuwa znz ilikuwepo kabla ya nchi zingine ni aina ya uelewa wenye matatizo.
Hoja si Mihangwa kama mwandishi bali yale aliyoandika, kama kuna mtu anajua jingine kuhusu wznz walowezi (ukiita watumwa utakuwa unatukana) kule S.A weka hapa.

Mkuu Zanzibar ni Kisiwa na kina kila aina ya watu kutoka Mataifa mbali mbali. Kuna wenye asili ya Kiafrika, Kiarabu, Kishirazi, Kihindi, Kigoa, Kichina na kadhalika na wamekuwa wakiishi kwa amani tu mpaka nyinyi mlipokuja na fitna zenu kutugawa ili mtutawale na mmefanikiwa sana.

Lakini nakwambia, Wazanzibari sasa wameshamjua "adui" wao na hawakubali tena kugaiwa mtakavyo.

Zanzibar for Zanzibaris.

View attachment 29559
 
JIBU HILO:

Prof.Ibrahim Noor 07/05/2011 kwa 7:15 mu · Jibu
Waalaykum salaam,
Kweli Joseph Mihangwa ni mwandishi mzuri akiandika juu ya maudhui fulani kama hayo ya katiba ya muungano, lakini katika makala haya kajikanyaga mara nyingi katika hoja na mantiki. Kwa mfano, ametuelezea kuwa hao "Wazanzibari" ambao hawasemi Kiswahili na ni watu wenye asili ya Kimakua. Jee, chimbuko la Wamakua ni Zanzibar?
Pili, Waingereza walipoyateka majahazi ya waharamia yaliyopakia watumwa dhidi ya mkataba baina ya Sultani wa Zanzibar na Waingereza kuanzia 1822 - ambao wenye chuki zao dhidi ya Waislamu hawautaji - na mikataba ya baadaye, watumwa hao waliachwa huru na kutafutiwa mahala wakae na kuendesha maisha yao. Wakati huohuo, wamishinari wa Kiingereza waliwavama na kuwatia katika Ukristo. Hivyo ndivyo walivyofanyiwa watumwa walioachwa huru na kupewa ardhi, kwa mfano ile ya Frere Town, Kenya, kama akina Mbotela na wengineo. James Juma Mbotela aliwatumikia vizuri sana Wamishinari hadi kuandika kitabu kiitwacho "Uhuru wa Watumwa" ambacho hakina lengo jingine ila kuonesha kuwa Duniani hakuna watu makhabithi na wabaya zaidi ya Waswahili-Waislamu. Kwa hivyo kuwa hao Wamakuwa walikuwa ni watumwa walioachiwa huru Zanzibar kwa muda mfupi waliokaa Zanzibar na katika muda huo wakawa Waislamu ni la hadithi ya paukwa pakawa. Hii madda ya utumwa ili walaumiwe Waislamu milele, ni katika hizo propaganda za wamishinari ambazo mpaka leo zinaendelezwa na kila kukicha huongezwa achari na sukari kuliko katika michezo ya Kihindi. Rafiki yangu mmoja wa Kiafrika aliyeniletea makala haya yanayofuata kukhusu Bi Khole, ameniandikia kuwa "If this is true, then this story about Bi Khole is awfully more powerful than Mandingo!" Sasa tafuteni mchezo wenye jina la "Mandingo" muuangalie wenyewe vipi binadamu wanavyopanga kichwani mwao wayapendayo.
Inaingia akilini zaidi kuwa hao Wamakuwa wanaojulikana kama ni "Wazanzibari" walipelekwa Afrika ya kusini kama walivyopelekwa huko Wahindi, Wamaley na wengineo kutiwa katika utumwa mambo leo wa kufanyishwa kazi kama watumwa kwa jina la vibarua. Zanzibar ilikuwa ipigwe vita na Mfaransa wakati wa Sayyid Said kwa sababu iliwakatalia kuchukua "vibarua" wa aina hiyo kuwapeleka katika mashamba yao yalioko katika koloni zao Wafaransa.
Kwa hivi sasa someni moja katika hadithi nyingi za kipaukwa pakawa zenye lengo la kuwapumbaza wataalii na kuwala pesa zao. Kwa wasiojua Kiingereza na kwa mukhtasari, hadithi inatuelezea kuwa Bi. Khola eti alikuwa hatoshelezeki ila aingiliwe na idadi kubwa ya watumwa ndipo uchu wake umtoke! Na hakutosheka! Na ikisha kila mtumwa aliyemuingilia hum-uwa. Jee amelipenda ndude na mikato ya mtumwa, hiyo si itakuwa khasara kubwa kwake! Mradi hawa magaidi na njaa zao hawana kikomo katika kupanga hadithi zao za kiwehu na Zanzibar imekaa kimyaa haina khabari ya athari za mambo haya katika mustaqbal wake! Khasara ilioje!

souce:mzalendo.net.
To:ibrahimnoors@hotmail.com
Subject: RE: Lini Wazanzibari wa Afrika Kusini watarejea kwao?
Date: Sat, 7 May 2011 18:34:10 +0000

Profesa, umeandika: "[FONT=Tahoma,sans-serif]Mradi hawa magaidi na njaa zao hawana kikomo katika kupanga hadithi zao za kiwehu[/FONT][FONT=Tahoma,sans-serif]" [/FONT]

[FONT=Tahoma,sans-serif]Laiti hadithi hizi zingekuwa za kiwehu kwani mwehu ana udhru hata kidini hapati dhambi. Hadithi hizi ni za upumbavu na ujinga! Na anaye sadiqi vitu kama hivi ni ngo'mbe; si mtu aliyekuwa anatumia aqili yake!![/FONT]
[FONT=Tahoma,sans-serif]Vipi Sayyida Khole atafanya mambo kama haya na ndugu zake wasijue? Kwani zina ni haram na aibu kubwa sana kwa aila yake. Ingalikuwa vitendo hivo ni kweli basi haqiqa angaliuawa. Ikiwa Sayyida Salma ilibidi akimbizwe ilipojulikan kuwa anatoka na bwana wa kijerumani [/FONT][FONT=Tahoma,sans-serif]Heinrich Ruete. Viti watakubali wafalme dada yao afanye ukahba wa kiwazimu kama huo?[/FONT]
[FONT=Tahoma,sans-serif]Na vipi huyo bibi, alikuwa mjinga sana hadi akapoteza mali yake kwa kuwaua watumwa waliokuwa ndio mali makubwa na vilevile wale waliokuwa wakimkidhi haja zake za kinafsi kwa kumburudisha kwa ya anasa? Mpaka lini watu watukubali kudanganywa kama waliokuwa hawana aqili za kupima mambo?[/FONT]
 
Zanzibar ndio wanaoigeza bara wanavyotaka, bara haimui chochote kwa zanzibar, angalia serikali yao ni 100 percent zanzibaris, ya Tanganyika wao wamejaa na wanatuamulia kila kitu, wameinyonya Tanganyika na wametosheka, sasa tunawapa ghasia tu! na wote wana moja, hata hao walioko serikalini kwetu wanatucheka tu...sawa wakubwa
 
Mkuu unatucheka lakini iko siku tutakomboka tu Mungu akipenda.

Kweli Zanzibar inaitawala Tanganyika, hebu angalia serikali ya Zanzibar, wapo watanganyika? angalia ya watanganyika, angalia mabalozi wa Tanzania nje, wanaotoka Tanganyika wanaiwakilisha Tanzania yote, wanaotoka Zanzibar wanawakilisha Zanzibar tu, mfano mmoja tu Balozi Ali Karume... malizia mwenyewe, mimi sipo
 
Mkuu Zanzibar ni Kisiwa na kina kila aina ya watu kutoka Mataifa mbali mbali. Kuna wenye asili ya Kiafrika, Kiarabu, Kishirazi, Kihindi, Kigoa, Kichina na kadhalika na wamekuwa wakiishi kwa amani tu mpaka nyinyi mlipokuja na fitna zenu kutugawa ili mtutawale na mmefanikiwa sana.

Lakini nakwambia, Wazanzibari sasa wameshamjua "adui" wao na hawakubali tena kugaiwa mtakavyo.
Zanzibar for Zanzibaris.

Sasa wale wanaojiita 'Asiatic' ili kujitenga na wenzao wamatumbi au wahindi wakiwa wote watumwa waligawanywa na Tanganyika!!!
Hakuna anayewagawa kwa sababu wote mnajinasibu mu wznz, jambo jema kabisa. Lakini jiulize mtakapokuwa mnakwenda ujombani Oman mtaangaliwa kwa mtazamo huo?
Hoja usioijibu ni kuwa kujitambulisha kuwa ni 'Asiatic' kulikuwa na maana gani?
 
Njoo Zanzibar umuone huyo anaejiita "Asiatic".

Huko waliko hao Wamakuwa wenzenu ndio kwenye au kulikokuwa na classes kwa sababu ya apartheid, Zanzibar hatuna habari hizo.

Wewe nadhani umefika Ukererwe tu, Zanzibar hukujui wala hatuna haja na watu wa aina yako.

Afterall, mambo ya Zanzibar yanakuhusuni vipi?
 
Na ya Tanganyika usiwe ukayazungumzia bac!
 
Njoo Zanzibar umuone huyo anaejiita "Asiatic".
Huko waliko hao Wamakuwa wenzenu ndio kwenye au kulikokuwa na classes kwa sababu ya apartheid, Zanzibar hatuna habari hizo.
Wewe nadhani umefika Ukererwe tu, Zanzibar hukujui wala hatuna haja na watu wa aina yako.
Afterall, mambo ya Zanzibar yanakuhusuni vipi?

Lahaullah! busara ituongenze katika majadiliano inshallah.

Suala lililopo mbele yetu ni kuwa wznz waliopo South Africa wanajinasibu hivyo. Hata kama ni wamakuwa bado ni wznz kwasababu wapo wanyasa na wameongoza znz wakiwa na hadhi ya uzanzibar. Ukianza kusema wamakuwa basi hakutakuwa na Znz kwasababu hakuna anayeweza kusema yeye ana asili ya znz, mathalani wapo wenye asili ya Oman, Yemen, Saudia, India n.k

Hao Waznz wa South Africa walitaka wawe na vitambulisho vya 'Asiatic' ndipo swali linazuka, je ina maana gani wao kunasibishwa na waasia kuliko wabantu na wakabaki kubeba vitambulisho hivyo vifua mbele!

Je, si kweli kuwa asili hufuata asili na haya tunayoyaona yanashabihiana na kile kilichotokea South Africa? Nikimaanisha wznz kutaka kubaki Tanganyika lakini wakiwa na vitambulisho vya uznz a.k.a 'asiatic'

Je, kutamani kufutiwa visa za Oman (mzalendo forum) sio aina nyingine ya 'modern Asiatic'?

Hizi ndizo hoja za kujadili na kutufikirisha.

Pili, mambo ya znz yananihusu kwasababu nimeishi znz nina marafiki, ndugu n.k. Hapa bara naishi na wznz ni ndugu na marafiki. Muhimu zaidi mambo ya kisiasa mengi ni sehemu ya ushirikiano na znz. Ni kweli znz inaweza kuwa hainihitaji kwa nywele zangu za kipipili, lakini inanihitaji kwa kodi yangu. Zaidi ya yote nchi yangu Tanzania inahitaji mchango wangu wa hali na mali pamoja na fikra.

Inshallah, tumuombe mwenyezi Mungu S.W.T atujaze hekima na busara katika ilm na mulankasha ili tunapohitilafiana kwa hoja, jazba iwe mbali nasi, nasi tuwe mbali nayo.
 
Tunaitaka zanzibar iliohuru katika maamuzi ya mambo ya kimaendeleo na na uongozi wa nchi na uhusiano wa nchi nyengine bila ya kupitia katika jina Tanzania(Tanganyika iliojificha).

Najua suali hili litakuja:si mutangaze tu kujitenga na muungano?

Musisahau kua viongozi wa juu wa Zanzibar wamechaguliwa kutoka Tanganyika kwa maslahi ya kuulinda muungano.

Naomba kama liko suali uliza moja au mawili tutumie utaratibu huu kutokana na kua muda sina wakutosha.

maswali yaweke wazi bila ya kuyazungusha ili yafahamike kirahisi.

Ahsante.
 
Back
Top Bottom