Shine
JF-Expert Member
- Feb 5, 2011
- 11,481
- 1,364
Katika hali isiyo ya kawaida huko Zanzibar watu wengi wamefurika na wamehudhuria mhadhara ya kupinga muungano uliofanyika viwanja vya Lumuba mjini Zanzibar na hivyo kupelekea mpaka Polisi nao kushiriki katika uchukuaji picha za video katika mhadhara huo.
Kwa kweli Wazenji wamevunja ukimya na kuiweka SMZ katk hali ngumu ya mchakato wa katiba mpya licha ya kuwa kuna polisi wengi waliopelekwa kutoka Tanganyika kwa hofu ya kutokea fujo.
Si wawape uhuru wao jama isitoshe hati ya muungano haipo na wasiwalazimeshe wasilolipenda walipende!