Ni wapi naweza kupata mkopo usio na RIBA ndani ya Tanzania hii?

Amini nakuambia, tofauti na muislamu mwenzako, hakuna mkopeshaji asiyependa riba. Kwa andiko lako maana yake ni kwamba, hata akikupa sehemu ya pesa yake bila kukutoza riba (asiye muislamu) lazima kuwemo na riba aliyowatoza wengine.

Nachelea kusema, MKOPO NI HARAMU KWAKO
Duh mkopo sio haram ila mkopo wenye riba ndani yake ndio haram...upo?!
 
Amani iwe nanyi.

Moja kwa moja naomba nijitambulishe kwa imani mimi ni muumini wa dini ya Kiislam.Katika maandiko matakatifu ya kitabu cha Quran naona kuwa Suala la RIBA limekemewa sana ,kifupi ni haramu kula au kutumia RIBA!

Principle kuu ni kuwa RIBA ni haramu, yaani ongezeko lolote la pesa juu ya mkopo ni RIBA na haifai kudeal na jambo hilo. Hivyo inaniwia vigumu kukopa katika taasisi za kifedha kama vile benki maana system ya mikopo yao ni RIBA.

Ukikopa mfano shilingi milioni 1 basi utatakiwa kurudisha milioni 1.2 au ukikopa milioni 10 basi utatakiwa kurudisha milioni 12-13. Hilo ongezeko katika pesa ya mkopo ndio RIBA na ni haram.

Naombeni mnijuze ni wapi naweza kupata mkopo usio na riba!!

Asanteni
Benki za kiislam
 
s
Kwanza nikupongeze Kwa kushikilia dini. Jitahidi pia usichepuke, Wala usipige mitungi.
Kuhusu mikopo, Check na NBC, Wana hicho kitengo Cha Islamic banking. Au People's Bank of Zanzibar. Wana hiyo mikopo isiyo na riba.
io kweli,hao amana sijui bpz taratibu zao ni wanakuuliza unataka mkopo wa nini kama ni gari basi wako wanakununulia gari then ndio unalipa huo mkopo ukifatilia kwa undani utakuta wamepata faida kwa kukuuzia hilo gari walilokununulia kwa mkopo ,riba imejifichamo,hupewi cash
 
kuna baadhi ya maandiko yameshapitwa na wakati tuishi kwa uhalisia,nina uhakika ingekua ni kipindi hiki hilo andiko lisingekuwepo
 
Amani iwe nanyi.

Moja kwa moja naomba nijitambulishe kwa imani mimi ni muumini wa dini ya Kiislam.Katika maandiko matakatifu ya kitabu cha Quran naona kuwa Suala la RIBA limekemewa sana ,kifupi ni haramu kula au kutumia RIBA!

Principle kuu ni kuwa RIBA ni haramu, yaani ongezeko lolote la pesa juu ya mkopo ni RIBA na haifai kudeal na jambo hilo. Hivyo inaniwia vigumu kukopa katika taasisi za kifedha kama vile benki maana system ya mikopo yao ni RIBA.

Ukikopa mfano shilingi milioni 1 basi utatakiwa kurudisha milioni 1.2 au ukikopa milioni 10 basi utatakiwa kurudisha milioni 12-13. Hilo ongezeko katika pesa ya mkopo ndio RIBA na ni haram.

Naombeni mnijuze ni wapi naweza kupata mkopo usio na riba!!

Asanteni
Jaribu bank za Kiislam kama Amana. Hawana riba mkuu. Ukikopa milioni 10 unarudisha milioni 10
 
Jaribu bank za Kiislam kama Amana. Hawana riba mkuu. Ukikopa milioni 10 unarudisha milioni 10
Hawatoi pesa taslimu...mikopo yao ni ya vitu tu..mfano una duka wao wanakuja kulithaminisha kisha wanakujazia mzigo wao wanakuwa wamekuuzia
 
Amani iwe nanyi.

Moja kwa moja naomba nijitambulishe kwa imani mimi ni muumini wa dini ya Kiislam.Katika maandiko matakatifu ya kitabu cha Quran naona kuwa Suala la RIBA limekemewa sana ,kifupi ni haramu kula au kutumia RIBA!

Principle kuu ni kuwa RIBA ni haramu, yaani ongezeko lolote la pesa juu ya mkopo ni RIBA na haifai kudeal na jambo hilo. Hivyo inaniwia vigumu kukopa katika taasisi za kifedha kama vile benki maana system ya mikopo yao ni RIBA.

Ukikopa mfano shilingi milioni 1 basi utatakiwa kurudisha milioni 1.2 au ukikopa milioni 10 basi utatakiwa kurudisha milioni 12-13. Hilo ongezeko katika pesa ya mkopo ndio RIBA na ni haram.

Naombeni mnijuze ni wapi naweza kupata mkopo usio na riba!!

Asanteni
Yaani upewe mkopo na mkopeshaji halafu akufaidishe huku yeye hapati choochote..!!!! Nenda tu kaombe kwa wazazi wako au kaka/dada zako
 
Amani iwe nanyi.

Moja kwa moja naomba nijitambulishe kwa imani mimi ni muumini wa dini ya Kiislam.Katika maandiko matakatifu ya kitabu cha Quran naona kuwa Suala la RIBA limekemewa sana ,kifupi ni haramu kula au kutumia RIBA!

Principle kuu ni kuwa RIBA ni haramu, yaani ongezeko lolote la pesa juu ya mkopo ni RIBA na haifai kudeal na jambo hilo. Hivyo inaniwia vigumu kukopa katika taasisi za kifedha kama vile benki maana system ya mikopo yao ni RIBA.

Ukikopa mfano shilingi milioni 1 basi utatakiwa kurudisha milioni 1.2 au ukikopa milioni 10 basi utatakiwa kurudisha milioni 12-13. Hilo ongezeko katika pesa ya mkopo ndio RIBA na ni haram.

Naombeni mnijuze ni wapi naweza kupata mkopo usio na riba!!

Asanteni
Nenda Peoples Bank of Zanzibar wanayo huduma ya Islamic Banking
 
Hawakopeshi fedha , wanakopesha vitu ambapo ni mfumo ule ule wa riba tu sema umezungushwa.

Mfano unataka milioni 10 ununue gari, wao wanasema tunalinunua hilo gari kwa 10m halafu tunakuuzia wewe kwa milioni 13. Then unalipa kidogo kidogo.

Ila ukiwafata wakupe fedha hawatoi.
Hiyo Ni biashara ndugu na baadhi ya ahl Elim wanasema sio riba
 
acha uongo wa kipumbavu,weka ushahidi hapa
Nikiwekee ushahidinwa Nini bwege wewe ...kama hautaki basi... Si nimekwambia uende Kwa Afisa utumishi wako au mkuu wako wa idara!!?? Yaani wabongo bwana ..... Ambacho hautaki ni Nini!!?? We ni MPUMBAVU....
 
Attachments

  • MKOPO KWA WATUMISHI (1).pdf
    423.2 KB · Views: 36
Mkuu unasoma hizo "aya" bila uelewa wake..........ikiwa wataka hivyo ulazimishavyo iwe basi Waislamu wote haitowafaa biashara yoyote

Uislamu juu ya suala la Riba..umetoa njia ambazo waislamu wataweza kuepuka "Riba" hiyo isiyotakiwa

Yasiofaa
1.haifai kuomba riba
2.haifai kuomba mkopo wenye riba

Ifaavyo
3. Musharakah - mwenye pesa na mwenye biashara wanakuwa washirika, wanafanya pamoja na kugawana faida
4.Murabaha-Benki inanuua bidhaa unayotaka,halafu inakuuzia kwa faida (Cost-plus financing)
5..Ijarah-benki inakukodisha kifaa na unanua baada ya muda wa kukodi (Lease)
6.Bay Salam - Mfano, mkulima analipwa kabisa kwa ajili ya mazao yake, na aleta mazao baada ya kuvuna bdae
7.Mudharaba-Benki inawekeza kwako na kuchukua asilimia ya faida ya shughuli husika (e.g 60:40) (Profit n risk sharing)

ziada
Muislam hapaswi kuwekeza (invest) kwenye kitu chochote, kuna utararibu wake na tathmini lazima ifanyike kujua kama maeneo hayo yanakubalika kisheria (sharia compliant).
Tunajua kuwa huwezi ku invest kwenye pombe, kamali, riba, n.k, lakini sio hivyo tu. Kampuni inaweza kuwa kwenye biashara halali, mfano kilimo, lakini ikakosa vigezo vingine vya uwiano wa ki-fedha (financial ratios).
Vigezo hivi vya ki-fedha vinaangalia;
1. Kiasi cha mkopo wa riba kinachangia kiasi gani katika mali zote za kampuni (interest-bearing debt/total assets shuld not exceed 30%)
2. Kiasi cha amana (interest-earning) kampuni ilichoweka benki na mali zote (interest-bearing deposits/total assets) kisizidi 30%
3. Kiasi cha mapato yanayotakana na maeneo yaliyokatazwa yasizidi 5% (non-permissible income)
4. Na “accounts receivables” zisizidi 49% ya mali za kampuni
Kama unataka kununua hisa (shares), kampuni lazima ikidhi vigezo hivyo juu.
Na hii sio kwa waislam tu, ni kwa mtu yoyote, kwa kuwa vigezo hivyo vinaiweka kampuni katika nafasi nzuri ya kuwa na maendeleo makubwa (high growth potential)

Mwisho
Watu wengi wanalalamika kuwa ni ngumu kuepuka riba, baadhi ya sababu wanazotoa ni hizi;
1. Wanatia shaka huduma za kibenki za kiislam na kusema kuwa ni ujanja tu kubadili riba na kuiita faida. Matokeo yake wanaendelea kutumia huduma za kibenki za kawaida (conventional banking)
2. Hawana hufahamu wa utararibu wa huduma za kibenki za kiislam
3. Wanasema benki za kiislam zinatoa masharti magumu ya mikopo, haswa like suala ka kutotoa mikopo ya fedha taslim (cash loans). Hali hii inapelekea thamani ya benki za kiislam (total assets) kuendelea kuwa chini ya assets za conventional banks.
Ukiangalia total assets za 50 top conventional banks only ni USD 69.6 trillion, wakati za islamic banks total globally ni USD 2.2 trillion, ila ukuaji unaendelea vizuri.
JE, NI VIP TWAWEZA KUEPEKANA NA RIBA?
KI-Iman (Religiously)
1. Kuamini kuwa rizki inapangwa na Mwenyezi Mungu, waweza acha riba na Yeye akakupa rizki yako kama kawaida (tawakkul)
2. Kumbuka kuwa kuna adhabu kubwa ya kujihusisha na riba (punishment). Financially
1. Fungua akaunti katika benki zenye utararibu usio na riba
2. Wekeza pesa zako katika mifumo isiyo na riba. Usiweke pesa zako kwenye government bonds, government bills, stocks (hisa) za makampuni yenye kufanya biashara haramu, speculation, n.k
3. Fungua akaunti za akiba (savings) ili uepukana na haja za kuomba mikopo
4. Usiingie mikataba yenye masharti ya kulipa penalties za riba
Socially (ki-jamii)
1. Ishi kwa mujibu wa kipato chako (live below your means) ili kuepuka vishawishi vya kutaka kukopa
2. Jiunge na utaratibu wa vikundi vya kupeana mikopo isiyo na riba, kama vile islamic saccos
Kumbuka kuwa madhara ya riba ni mabaya hapa duniani, na mibaya zaidi kesho akhera.
Surah Al-Baqara, Verse 276:
يَمْحَقُ اللَّهُ الرِّبَا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِ وَاللَّهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ
Allah does not bless usury, and He causes charitable deeds to prosper, and Allah does not love any ungrateful sinner.

Some Credit ziende kwa: Salum Awadh

cc.Partner in business Mshana Jr
Shukrani Sana mkuu umeelezea vema ....namalizia deni langu ntarudi PBZ kupata gari ya ndoto yangu.....Murabaha forever for my life inshaAllah
 
Back
Top Bottom