voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,553
- 11,885
Ninasema hivyo kutokana na mtazamo wangu binafsi.siwakilishi chama chochote cha kisiasa nchini.
Mbinu za ufanyaji siasa za chadema kwa sasa zimepitwa na wakati au zimechokwa!
Ninaposema hivyo nina maanisha kwamba ...wananchi wanahitaji tofauti.
Wakati Chadema pia mnalo hitaji lenu tofauti.
Jaribuni kukaa na kupata watunga sera mahiri ili wawasaidie kutunga sera zinazowagusa wananchi kwa 100%.
Badala ya Sera hizi za matukio na kutafuta Sympathy kwa watanzania.
Maana hata watanzania pia wanaihitaji hiyo hiyo Sympathy toka kwenu wanasiasa.Badala yake nyinyi mnawatumia wananvhi kama ngao ya kujikingia ili mjinufaishe binafsi
Kwa Dunia hii yenye utandawazi uliokithiri,kuwa mpinzani kunahitaji uwe mkweli na muwazi.uwe kweli unaakisi uhalisia na wananchi waweze kuweka imani kwako
Maana uelewa wa wananchi ni mkubwa kwa sasa tofauti na hapo awali.Pia mawasiliano na mifumo yake imebadilika kwa kiasi kwamba wananchi kwa asilimia kubwa wanapata na kuelewa habari nyingi nchini kwa wakati husika na kusha kuzifanyia upembuzi makini.
Ila wanasiasa mmeeendelea kuwachukulia wananchi kama watu wasiojielewa elewa ki- viile!
Lakini kumbe unakuta wananchi ndio wamewapuuza wanasiasa baada ya kuchoka na ngonjera zao zisizo na ukomo wala ukweli.
Sasa siasa imegeka kuwa sehemu ya ajira na kipato cha utajiri, na sio kipawa cha uongozi na maadili mema!
Hili ni tatizo kubwa kwa wanasiasa wa Tanzania..kote kabisaa!
Sio CCM wala Chadema pekee,bali vyama vyote!
Tukisema Chadema mnapenda kick za matukio kupata Political Mileage mnasema tunakosea?
Mfano wa hili ni juzi huko Katesh.
Chadema jipimeni kwa kina maana kwa uhalisia ni kwamba mnahitaji uongozi mpya wenye kuweza kufanya mabadiliko makubwa na ubunifu wa sera na mbinu za ufanyaji siasa kuendana na wakati uliopo ili muweze kwenda sambamba na upepo halisi wa kisiasa nchini.
Viongozi waliopo kwa sasa pumzi yao inaonekana rasmi, ndio inaelekea imefikia ukomo kisiasa.
Hawana mbinu mpya za kukabiliana na CCM wanaobadilishana vijiti kila baada ya miaka kumi(10).
Kama ni riadha ya kisiasa!
Mbowe ameishazunguka uwanja mpaka amepitiliza na vijiti nje ya uwanja. na sasa anakimbia peku kwenye lami.
Msaidieni......
Kwa kuwa matusi ni sehemu ya seraza baadhi yenu!sintawashangaa mkianza kuyaporomosha hapa
Ila mimi nimemaliza kutoa langu la Moyoni.
Niwatakie SABHATHO njema!