Ni wakati gani nyeti ya mwanaume huvunjika wakati wa tendo la ndoa na ipi tiba yake?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,138
.


Kuvunjika kwa uume ni tatizo la kawaida miongoni mwa wanaume, licha ya kwamba tatizo hili halizungumzwi sana.
Kuvunjika kwa uume kuna uwezekano mkubwa wa kutokea pale unapogonga mguu au sehemu ya siri ya mwanamke wakati wa kujamiiana.
Ikiwa tatizo hili halitatibiwa kwa wakati, linaweza kuathiri uwezo wa kimwili na tendo lako la ndoa kwa muda mrefu.
Uwezekano wa kuvunjika kwa uume huongezeka ikiwa mwanamke yuko juu ya mwanamume au mwanamume anashiriki tendo la ndoa lisilo la asili. Kuvunjika kwa uume kunaweza pia kutokea wakati wa kupiga punyeto au wakati uume umeangukiwa na kitu kizito.
Wakati uume uliosisimka kikamilifu unapopigwa au kubanwa na tunica albuginea hupasuka. Kuvunjika kwa kwake pia kunaweza kusababisha matatizo makubwa ya kimwili na kuwa na madhara ya muda mrefu kwa maisha yako ya ngono ikiwa hautatibiwa mara moja.
Utafiti pia uligundua kuwa asilimia 57.2 ya wanaume huvunjika sehemu hiyo nyeti wakati wa ngono.
.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Jeraha kama hilo hutokea miongoni mwa wanaume pekee. Tatizo hili huonekana kwa wanaume wa makamo, hasa katika kundi la umri wa miaka 30 hadi 50. Ni kawaida zaidi kwa wanaume wa jinsia tofauti. Miongoni mwa wanaume walio wapenzi wa jinsia moja, takwimu ni asilimia 1.8.
Kulingana na utafiti, idadi ya matukio kama hayo huongezeka wakati wa siku za kiangazi au wikendi.
Kuvunjika kwa uume husababisha maumivu makali katika eneo la uzazi huku uwezekano huku umbo la sehemu hiyo nyeti huonekana limelegea na kujipinda.
Mtaalamu wa masuala ya jinsia Dkt.Prassan Gadre, akitoa maelezo ya kina kuhusu hili, alisema "Je, uume unaweza kuvunjika licha ya kwamba hauna mffupa? Ndiyo. Inawezekana. Jeraha lolote au ajali inayosababisha sehemu hiyo kulegea inaitwa kuvunjika kwa uume."
"Kusimama kwa sehemu hiyo pia kunaweza kuwa chanzo chake cha kuvunjika. Kuvunjika kwa uume kunaweza pia kutokea ikiwa uume utasimama ghafla wakati umelala. Vilevile uume unaweza kuvunjika unapojaribu kuusukuma ndani wakati wa kupiga punyeto.
"Sehemu ya sira ya mwanamke mara nyingi husinyaa wakati wa kujamiiana. Ikiwa uume utalazimishwa kuingia ndani wakati uke umeshikana, pia unaweza kuvunjika," alisema Dk. Gadre .

Je utajuaje mwanamume amevunjika sehemu yake ya siri ?​

.


Mbinu za kawaida hutumiwa kutambua iwapo uume umevunjika. Tatizo hili pia linaweza kutatuliwa na ultrasound, lakini linahitaji daktari mtaalamu.
Upasuaji ni chaguo zuri sana baada ya kuvunjika.
Akitoa taarifa juu ya hatua gani zichukuliwe mara baada ya kuvunjika kwa uume, Dk Gadre alisema, "Kwa bahati mbaya, jambo kama hili likitokea, jambo la kwanza unapaswa kufanya ni kwenda hospitali, kwa sababu hii pia ni aina ya jeraha."
"Kama sehemu ya huduma ya kwanza, mwathiriwa hafai kuondoka alipo. Mara tu anapopatikana na jeraha , eneo hilo linapaswa kuwekewa barafu kabla ya kumuona daktari.

Nini kinafanyika baada ya upasuaji?​

.


Kwa sababu ya kuvunjika kwa sehemu nyeti ya mwanamume maisha yake ya tendo la ngono huathiriwa vibaya. Wale ambao wamepata jeraha kama hilo wanahisi athari kwa muda mrefu. Watu wengine hupata maumivu kwa muda mfupi baada ya upasuaji, lakini katika hali nyingi madhara ni ya muda mrefu.
Watu wengi hupata unyogovu au shinikizo wakati wa ngono baada ya kuvunjika kwa shemu hiyo nyeti. Hofu ya kuumia pia husababisha tofauti kubwa jinsi unavyoshiriki ngono. Watu wengi wanapaswa kupata ushauri baada ya upasuaji.
Uvimbe mdogo unaweza kusababisha matatizo mengi kama vile, mabadiliko ya umbo la uume, kuishiwa nguvu za kiume, na maumivu hususan wakati wa kukojoa.
Pia kuna uwezekano kwamba umbo la uume litabadilika baada ya upasuaji. Kuna maumivu wakati uume unaposisimka na urefu wake pia hupungua ukilinganisha na ulivyokuwa awali.
Hivyo daktari anapaswa kujadili matatizo haya yote na mgonjwa kabla ya kufanya upasuaji.
Mgonjwa anapaswa kupewa maelezo ya kina kuhusu nini cha kufanya baada ya upasuaji. Mgonjwa anapaswa kuambiwa kwamba kutumia mfuko wa mkojo{ catheter} ni jambo muhimu zaidi baada ya upasuaji. Ni muhimu kutumia catheter kwa angalau wiki nne baada ya upasuaji.
Vivile ni muhimu kuweka eneo lililojeruhiwa safi hata baada ya upasuaji. chanzo. Ni wakati gani ambapo uume huvunjika wakati wa tendo la ndoa na ipi tiba yake? - BBC News Swahili

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom