Ni ushuhuda ambao umeniumiza kuusikia.....

Nadhani hili litukumbushe kwamba Mungu ha-operate the way we want or think. Mungu anajua why iwe the way ilivyo. So ni kumwachia yeye (Mungu) afanye kwa kadiri ya mapenzi yake. Kwa nini hujiulizi Mungu alimfanya huyo mtoto apate maambukizi ilhali si yeye alikuwa na makosa pengine wazazi wake? so huwezi muuliza kwa nini asimpe huo uponyaji?
 
Nilikuwa naangalia kipindi cha Mimi na Tanzania kinachoongozwa na Hoyce temu..
Chanel Ten
Ni kuhusu mtoto Shigella William yatima anayeishi Mwanza 14 years old na anayeishi na Virus vya ukimwi..
Na kionekana zaidi ni muumini wa dini ,aliekuwa na imani thabiti juu ya Kikombe cha babu..
kwa imani yake Alienda kunywa Kikombe cha babu Loliondo na aliporudi baada ya siku 21 aliamua kwenda kupima na kujua kama amepona..
Hoyce alimpeleka Clinic kupima na vipimo vyake kuonyeshwa kila hatua lakini majibu yalionyesha bado ameathirika..
Lakini alipopokea majibu hayo alinyong'onyea kidogo na bado aliendelea kumshukuru mungu kwa kila kitu na kisha kusali..
ooh my god ameniliza na ushuhuda huu umeniumiza moyoni na kubaki natafakari kwa huzuni sana ..
Nimeamini kweli Loliondo ni imani ya mtu ..
Nijulisheni wenzangu inakuwaje wengine wanatoa ushuhuda wamepona na wengine hawaponi...
Iweje mtoto mdogo kama Shigella anayeonekana ni mwingi wa imani hakupata uponyaji huu???na ugonjwa wake inavyoonekana alipata maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
Nafedheheka sana wadau.... weekend yangu imekuwa ya mawazo...Muwe na weekend njema yangu si njema tena

hapo kwenye red sikubaliani na wewe, kwa maelezo yako huyo mtoto alipaswa kuwa amepona ikiwa ni imani. Loliondo ni usanii tu hakuna cha imani ya Mungu au ya Mtu. Mliokwenda kule bora mngechuma hata majani ya mwarobaini, mkayachemsha na kuyanywa it could have some difference in your bodies.
nani unamfahamu aliyekwenda huko na amepimwa na ikathibitishwa kuwa amepona.
 
Nasoma nikiwa ofisini na ofisi yangu wateja hawapungui, ila machozi najitahidi kuyazuia yasitoke wasijeniuliza nina shida gani! Kweli inagusa sana na Mungu amsaidie mtoto huyu ili apone. Ushauri wangu ni kwamba mtoto Shegila apelekwe kwenye maombi ili akaombewe kwani hakuna jambo Mungu asiloweza, atapona tu kwa maombi . Mungu alimfufua Lazaro toka kaburini aliyezikwa siku 4, aliponya vipofu, viwete, viziwi na magonjwa mbalimbali,hata ukimwi Mungu anaponya. Naamini atapona tu kwa maombi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom