Ni Shule Nzuri Sana

popiexo

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
742
182
Jana TBC walionyesha uzinduzi wa shule mpya ya Msoga, kwakweli ni shule nzuri yenye majengo bora sana. Na JK ndio alienda kukabidhiwa shule hiyo, shule hiyo imejengwa kwa msaada wa serikali ya China kwa thamani ya shilingi za Tz 1bln, Asante.

Kilicho nifurahisha ni ubora wa miundombini ya shule hiyo, lakini kwa upande mwingi nilijiuliza hivi tutategemea misaada kama hii mpaka lini wakati kama nchi uwezo tunao wa kujenga shule nzuri kama hiyo bila kutegeme wachina, ni kuamua tu kama hela ya kuwalipa DOWANS ((94bln) ipo tusiwalipe ili tujenge shule 94 zenye hadhi kama shule hii ya Msoga na hapo ndio at least tutakumbuka tumetoka hapa na tumeelekea pale.

Chakushangaza na kukera ni pale katika lisala yake Dr Shukuru Kawambwa, Waziri alipoomba wachina waongeze madarasa mawili kwa ajili ya chekechea katika shule hiyo, kwa kweli ni utegemezi wa hali ya juu. Inamaana wizara yake imeshindwa kushukuru msaada wa wachina kwa kutenga bajeti ndogo ta hayo madarasa mawili? Kodi zetu zinatafunwa na watu wachache na za wenzetu ndio zije kufanya maendeleo ya watanzania.

Iko siku itafika mwiso
 
Mkuu wakwere na wazaramo ni watu wanaopata faraja kwa kuomba, ni sawa na watani wangu wa Idodomya. Kwa hiyo ukishangaa, shangaa polepole utachekwa!
 
Back
Top Bottom