Mkuu, nakileta kwako kilio Cha sisi wazazi WALALAHOI tunaosomesha watoto katika shule ya Msingi JUHUDI, kata ya Lukobe.
Mheshimiwa, sina uhakika kama Una taarifa zozote kwamba ndani ya kama kilomita 10 kutoka ofisini kwako ktk kata ya Lukobe Kuna shule ya watu maskini KABISA KABISAA TENA MASKINI WAKUTUPWA!! HAWA NI WALALA HOI KABISA ktk nchi hii ambao Mheshimiwa Rais wao Mama Samia anawatambua na ANAWATHAMINI kabisa na kawajengea shule iwe jirani yao ili watoto wao waelimike, na kwa jinsi Mama anavyowathamini hao walalahoi akakuteua wewe Mheshimiwa kuwa mlezi wa hao masikini wasio na UWEZO wa kusomesha watoto wao ktk shule za hadhi ya juu. Lakini sijui kama na wewe hao unaowasimamia chini yako sijui kama WALISHAKUELEZA ni nini kinachoendelea ktk shule ya Msingi JUHUDI!
Na kama WALISHAKUELEZA, basi walikudanganya Hali halisi ya hapo. Na kama unayo taarifa basi Wahenga walinene " Tusiandikie mate na wino upo" funga safari dakika yoyote usomapo waraka huu nenda mwenyewe kajionee, tuache masikhara kwenye uhai wa watoto wetu. No research no Comment!
Waswahili tunasema "Jihadhari kabla ya Hatari" Mheshimiwa kwani YALIYOTOKEA HANANG tena majuzi tu, Ina maana hatujajifunza kitu tu? Au ni mwendo ule ule tu, yaani tunasubiria majanga yatokee ndio Mnajifanya mnasikitika na kutoa pole!
Mkuu, shule ya JUHUDI ni HATARI KABISA KWA AFYA ZA WATOTO WETU! Mazingira ni Hatarishi Kwa watoto, magogo, michanga,tope, mawe na matakataka yanayoletwa na Mvua yamejaa Uwanja wa shule. Imekuwa sio shule kwani mkondo wa maji unapita katikati ya shule na imekuwa mikondo zaidi ya mmoja. Maji yanaingia madarasani, vyoo vimezingirwa na tope na mchanga, sijui watoto wanajisaidiaje. Maji yamechimba baadhi ya majengo na Msingi kubomoka.
Inasemekana Viongozi kadhaa walishafika hapo shuleni na Hali halisi wamejionea, lakini hakuna wanachokifanya.
Kwa yaliyotokea HANANG Liwe ni somo Kwa sisi binadamu; kwanini iwe ni somo? sababu kabla ya Hilo janga hakuna MTanzania ambae aliamini kuwa mlima unaweza KUMUNG'UNYUKA wote na kuleta maafa.
Mkuu pia Kuna suala la KIPINDUPINDU.
Hayo maji yanayopita hapo ndani ya shule yanakotoka yanapita katika nyumba za watu ambao wengine wanatumia fursa hii ya Mvua kutiririsha maji taka ya vyoo kuingia miferejini na hatimae yanapita hapo shuleni na watoto hao wadogo wanachezea.
Hili suala naona tunaWATESA sana walimu kwani tunawapa kazi za ziada kudhibiti watoto wasicheze kwenye matope, hivi kweli hao walimu wataweza kweli kuandaa masomo, kufundisha na Sasa kulinda AFYA za watoto it's not fair!
Hii naifananisha na mahafa ya Hanang Kwa kuwa iwapo kutatokea KIPINDUPINDU itakuwa ni HATARI sana, kwani tusiseme haiwezekani, kwani magonjwa yanasababishwaje? Shule Ina mamia ya watoto tena hapa ni wadogo wa darasa la 5 kurudi chini.
Na kama Manispaa Ina Bwana AFYA basi Kwa hii Hali halisi ya JUHUDI primary inabidi ajitathmini!
Wanakauli za kebehi eti kama hapakufai HAMISHA mwanao, sisi walalahoi uwezo wetu ndio hapo hapo ambapo Mama Samia anapathamini.
Mkuu, nakuomba fika mwenyewe hapo shuleni ujionene mwenyewe usitume mtu.
Na iyo shule kama ingelikuwa ya mtu binafsi Kwa mazingira halisi ya uchafu uliopo pale basi mmiliki angelikuwa muda huu yupo Magereza.
Hii shule ni ya Walalahoi ORIGINAL maana kama mtu una uwezo japo kidogo HUWEZI kumwacha mwanao ktk mazingira Hatarishi kivile.