Ni sawa kwa Mtendaji Kata ya Boma Morogoro (Kada wa CCM) kujirekodi na kusambaza picha zinazooesha uchafu wa Shule ya Morogoro Sekondari?

T2020

Senior Member
Jul 15, 2020
131
328
Serikali inapaswa kuwa makini na ajira hizi za upendeleo zinazokuwa zinatolewa kwa makada wake hasa vijana wa CCM au katika nafasi zozote hasa inapotokea fursa yoyote.

Huyu Mtendaji wa kata ni mmoja kati wa vijana wa CCM aliyeajiriwa akitokea katika vyeo vya UVCCM na kupata ajira serikali.

Picha zinazosambaa katika mitandao ya kijamii na magroup mbalimbali ya Whatsapp wakionesha akifokea wanafunzi wa kike na nyingine akionesha uchafu maeneo ya jikoni, vyooni na mabweni yanayotumiwa na watoto wa kike.

Chanzo kinadaiwa ni picha alizopiga na kujirekodi na kuzisambaza katika group ya wafanyakazi wa kata ya Boma. Taarifa zinaeleza kuwa alijirekodi alipokwenda kusimamia usafi shuleni hapo. Aidha amefanya hivyo kwa kutafuta sifa au kuchafua uongozi wa shule hiyo.

Kama lengo lake ni kufanya usafi Kuna sababu gani kusambaza picha hizo. Idhini ya kufanya hivyo kapewa na nani?

Sheria ya elimu zinasemaje juu ya kusambaza taarifa za shule au taasisi nyingine za serikali. Hii haiwezi kuleta taharuki kwa wazazi juu ya usalama wa afya za watoto wao?
 
Prisca Mawallah huyu, Katibu UVCCM wilaya Morogoro enzi hizo. Ni Mdada smart sana.
 
Prisca Mawallah huyu, Katibu UVCCM wilaya Morogoro enzi hizo. Ni Mdada smart sana
Mmeanza kuteteana. Kosa la mtandao hilo kurusha picha na habari bila idhini. Na tabia za maCCM hizi. Ukisikia kazi za sensa, kusimamia mitihani, uchaguzi eti nafasi kadha za vijana wa chama. Chafuaneni tu.
 
Serikali inapaswa kuwa makini na ajira hizi za upendeleo zinazokuwa zinatolewa kwa makada wake hasa vijana wa CCM au katika nafasi zozote hasa inapotokea fursa yoyote...
Umesha sema ni wa ccm ulitegemea nini? KWANZA Palamagamba na Bashiru walikuwa hivyo enzi wako UDSM? Au Pole pole wa mchakato wa katiba ya wananchi( katiba ya WARIOBA) ndo yule yule baada ya kuwa mwenezi wa ccm?

Leo hii unawezaje kumtofautisha Palamagamba na Lusinde na Bashite na Msukuma na Kitenge na WAITARA?
 
Kwani umesahau ile ahadi kuu ya mwanaccm "Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko"

Kwahiyo yuko sawa kabisa , huyo bibi wa Unguja anapotezwa na machawa wanaopigania maslahi yao kwenye uteuzi.

Aione kwenye jalada :Lucas Mbwa Wa Shamba
 
Back
Top Bottom