Ni sahihi kufanya maendeleo ya Kiuchumi na mpenzi wako?

"
nyinyi wanaume ni vinara wa kugoma kuwekeza kwa mwanamke asiye mkeo,
Leo iweje rahisi kwa mwanamke
?"

Kweli unacho kizungumza?

Hivi wakina nani wanaongoza kusomesha wachumba zao vyuoni?

Akina nani wanaongoza kuwapa mitaji ya biashara na kuwapangia nyumba na wengine kuwajengea nyumba wachumba zao?

Kumbuka hao wachumba wanafanyiwa hivyo,sio wake.

Ndoa yoyote huanzia na stage ya uchumba,matendo na tabia zenu za kwenye uchumba ,ndizo hizo hizo mtaingia nazo kwenye ndoa.Kama ulikuwa mbinafsi hata kwenye ndoa utakuwa mbinafsi tu.
Sasa hayo matendo mema yanayoanziwa kwenye uchumba ni lazima yawepo na uyaangalia kabila hujaoa au hujaolewa. Tabia njema, upendo wa kweli, , heshima, kuthaminiana na mengineyo lkn sio ktk swala la kuwekeza pamoja, kwani ata nisipowekeza naye ndiyo kigezo cha yeye cha kutonioa?, Eti kuwa ni mbinafsi kisa sijawekeza naye?.

Na tambua kuwa sio wote ambao wamewekeza pmj alafu hawaoana, wapo walioona lkn ktk 30 bs ni mmoja ndiye aliyefanikiwa kutimiza hilo jambo kihaki, lkn walioathirika na hili swala ni wengi Sana mkuu, watu wanatendwa, hujawah kushuhudia eti eh?
 
Safi Sana, Asante kwa kuelewa swali langu mana naona wengi hawajaelewa namaanisha nini. Moe nimeulizia kuwekeza kwa mpenzi ambaye hatambuliki kwenu wala hutambuliki kwao. Je unaweza kuwekeza kwake?
Sio kwamba hawajaelewa bali hawa watu hawajui wanachokitaka.

Eti namimi najikuta niko bize nawekeza na mpenzi tu dahaisee haiwezekani kila mmoja awekeze kivyake mpaka tuoane.
 
Wanasemaga mchumba anasomeshwa cherehani tu
Halafu wao wanataka tuingie kwenye hiyo betting..wallah siwezi.
cherehani yenyewe siku hizi Haina ata soko Sana. Kwa kweli ata sie hatuwezi kuwekeza kwao katu. Mi nimeshindwa eti.
 
Sio kwamba hawajaelewa bali hawa watu hawajui wanachokitaka.

Eti namimi najikuta niko bize nawekeza na mpenzi tu dahaisee haiwezekani kila mmoja awekeze kivyake mpaka tuoane.
apo Sasa na mkopo unakopa kabisa milioni 20 za kujenga nyumba ya pmj na hati ya nyumba umeandika jina lake eti.
 
Siku hizi mambo yanakwenda kisheria... Hakuna kuzurumika.. Kwa kila kitu mwaandika majina mawili na kila mtu anabakia na kopi. Kama unahisi uko na mtu kwa ajili ya kumchuna tu yaan hauna upendo naye. Unapita tu. Bora upite tu. Ila kama mpo kimaisha, hiyo yaweza ongeza thaman kwako
Najiuliza hapa.... Mambo yakikaa vizuri kisheria.... Upande wa uwekezaji na shares zikawa clear kwa Kila mmoja katika mradi ule.... Shida IPO wapi??

Unaacha kufanya maendeleo unasubiria Mume wa kukuoa.... Hao waoaji wapo Foleni.... Mpaka wakufukie... Miaka 5 mingine ijayo. We must take CALCULATED RISK 😂😂
 
Kizuri ni kwamba .. umeuliza na ukaji-jibu

Sema kuna-vijana huwa wanavimba na kucheza michezo atarisha kwa afya za akili zao na wanajitoa kwa moyo wote kwa wapenzi wao na huwa wanajaribu michezo ya kuwalipia Ada wachumba zao , kawaida wakiachana utakuta kijana anachoka kuanzia mwili mpaka akili na makunyanzi juu ..

Hata mke kuandika jina lake kwenye ardhi niliyonunua kwa Pesa yangu ni kosa kubwa , nasisitiza ni kosa kubwa na sitafanya
 
duh we nomaaa.
 
Back
Top Bottom