Ni onesha au onyesha?

Ntaramuka

Senior Member
May 2, 2008
169
27
Maneno haya ONESHA na ONYESHA hukanganya sana kimatumizi. Baadhi husema sahihi ni ONESHA na wengine husema sahihi ni ONYESHA, mimi nasema yote ni sahihi, wewe unasemaje?
 
Ndugu Salaam

Neno sahihi ni Onesha na si onyesha kama nia yako nikumuonesha mtu kitu ua mahali.

Onyesha hutumika kuonya. Kama mtu kafanua ndivyo sivyo anaonyeshwa.

Wasamu
 
Ndugu Salaam

Neno sahihi ni Onesha na si onyesha kama nia yako nikumuonesha mtu kitu ua mahali.

Onyesha hutumika kuonya. Kama mtu kafanua ndivyo sivyo anaonyeshwa.

Wasamu

Taib .. umeelezea barabara.
 
Kwa mujibu wa BAKITA, yote ni sawa. Ila inasisitizwa kwamba unapoamua kutumia 'onesha' basi endelea hivyo, usitumie 'onyesha'. Na 'onyesha' hali kadhalika, itumike bila kuchanganya na 'onesha'.
Niliyasikia haya kupitia Radio One, kipindi cha Kiswahili kinachorushwa kila siku ya Jumamosi asubuhi. Afisa mmoja wa BAKITA alieleza hivyo.
Asanteni.
 
Binafsi ninasema maneno haya yanafanana kwa sababu neno ONA limefanana sana na neno PONA kiumbo.

Kupona maana yake ni mgojwa kutoka katika ugonjwa,
Dawa anazomeza mgonjwa zinaMPONYA yaani zinamfanya aPONE,
Daktari anayempa mgonjwa dawa anamPONYESHA au anamPONESHA,

Hivyo, kuONA ni kupata taswira ya kitu kwa kutumia macho,
Macho ndiyo humfanya mtu aONE ama sema yanamuONYA,
Kitu ama hali itakayokufanya uweze kupona hukuonyesha.

Hapo mwanzo neno hili lilipoanza kutumika halikumaanisha KUONYA( kutia mtu adabu).

Kuna mtu alimkosea (alimuudhi) mwenzake, sasa kwa vile yule aliyeudhiwa hakuwenza kumuadhibu aliyemuudhi kwa wakati ule, akamwambi ngoja utaONA nitakutia adabu. Baadaye yule aliyeudhiwa akamuadhibu yule aliyemuudhi ( ili aONE kama alivyokuwa amemwambia awali, ngoja utaONA). Watu walioshuhudia akimuadhibu wakasema amemuONYA. Kuanzia wakati huo kuonya likawa linatumia kumaanisha kuONYA(Uliyokuwa ukiijua wewe, kutia mtu adabu) lakini bado neno hili ONA halijapoteza maana yake ya mwanzo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom