Ni nini solution la tatizo la internet kama hili?

little finger

JF-Expert Member
Oct 13, 2018
384
986
Habari za saa hii wakuu.

Nimepata changamoto kwenye swala la speed ya internet, natumia simu (4G) speed ni ndogo sana.

Minara inaishia bars 3 kama inavyoonekana kwenye picha. Nipo maeneo ya mbezi ya kimara, nyumba ipo kwa chini.

Swali langu ni jinsi gani naweza kutatua changamoto hii, nimeshajaribu line zote tatu (Airtel, voda, tigo) zote minara ipo chini.

Je kuna kifaa au namna ambayo naweza boost hii internet?

Natanguliza shukrani.
Screenshot_20231007_081938.jpg
 
signal nyingi zinazuiwa na kuta or milima,ukiwa bondeni jaribu kuweka meza yako unayotumia karibu na dirisha huku Mara nyingi signal zinapita vzr tu.
 
Back
Top Bottom