Ni nani huyu Cool 9 Jamani?

Black Madonna vilikuwa ni vikundi vya watoto wa shule za msingi waliokuwa wakikutana huko Dodoma Mlimani chini ya kiongozi wao Edward Ndomba nakumbuka ni marehemu na kifo chake kilitokea katika purukaushani za namna hiyo hiyo kwa mtu kuchomwa na mshale kichwani. Hawa watoto walikuwa ni wale wa Halaiki za Chipukizi
Wababe wa Dodoma waliodumu kwa muda mrefu ni km kina Abdul Yusuf (kwa sasa km miaka 3 ni marehemu) huyu ndiye tuliyemuogopa kwani akikuona una Demu au kitu km gari atakufuata umlipe asikufanyie fujo anweza kujilengesha kwenye bumper la gari ukiendesha na kudai umemgonga umlipe la sivyo vagi.
Matajiri wa Enzi hizo walipenda kumuweka baunsa milangoni wakati wa filami za kina Bruce-Lee au SHOLAY huko N.K. na PARADISE
Siku za mwishomwisho alitandikwa na watoto wadogo wa vyuo walokuwa hawamjui km ni Baunsa wa Dodoma
Mwingine ni Liondo naye amefariki mwaka huu, naye alikuwa yumo katika list ya wanaoogopewa au kujua Mission town za nani ataibiwa na hivyo kuwafanya Matajiri wa hapa mjini na wenye mabaa kumpa kazi ha za ubaunsa

kuna kikundi cha ngoma za utamaduni kilikuwa kinamilikiwa na MADINI (dodoma) walikuwa na mtu 1 anaitwa juma kombo naye alikuwa balaa
 
daah huyo DAME namkumbuka sana enzi shule ya msingi Mashujaa ya Sinza wakati tupo wadogo tukimwona tu tunamkimbia na alishawahi kula chips na kudai chenji wakati halikuwa hajatoa hela

na puzza je na yule marehemu lintu
 
Huyu Jamaa alikuwa Gumzo mitaa ya Iringa:
Nakumbuka Ilifikia stage mtu akipigwa badala ya kufikiria kwenda kwenye vyombo vya sheria anakwenda kushtaki kwa huyu Mbabe. Na Ole wako akipewa hiyo kesi na vipesa kidogo utakimbia mji.
Kuna vijibabe vingi vya mitaa tulivyokuwa tunavifahamu huko kitanzini,ngome, Ruaha, mwangata wakati ule vilikuwa vinakimbia mji na kwenda kujificha kusikojulikana mara wanapojua kuwa huyu jamaa amepewa Mashtaka na mtu ama kundi jingine kuhusu uonevu vilivyo ufanya kwa wengine. (Na hii ndio mojawapo ya sababukubwa ya yeye kufahamika, maana mtu mnayemuamini kuwa ndio mtemi wa mtaa anapoingia mitini kwa hiari yake mwenyewe kuogopa kukutana na Jamaa inabidi iwe gumzo mji mzima)
Jamaa alikuwa ana kaustaarabu fulani wakati mwingine kwani kuna wakati nimeshuhudia akiwa msuluhishi wa ugomvi, alikuwa ameshajua kuwa yeye ni mbabe.
Nakumbuka mwanafunzi akipigwa ama kuonewa na mwenzie tamko la kwanza atakalotoa nikukuambia kuwa "Utaona naenda mwambia Cool 9 " .. Na watu walikuwa wanafahamu nini kitafuhata.....Na hata ukiwa mgeni inabidi uulize mbona huyu mtu anatajwa saaana.....Ila ukimuona utafahamu kwanini wanamtajataja.
Hata Watoto wakikorofishana utasikia mmoja anamtishia mwenziwe kuwa ataenda mwambia cool 9.... Chezea huyo jamaa....
Haya mambo ya sheria, ustaarabu,haki elimu, haki za binadamu ni miaka ya karibuni jamani. Zamani awareness ilikuwa ndogo saana... Ubabe ubabe tu




 
huyu mshikaji aliolewa ndo kisa cha kupotea kwenye ramani.

teh! teh! teh! teh! teh! teh!!..............kipindi hicho angekuskia na kufahamu ndo wewe umemtusi,du! mkuu nafikiri ungetamani uchukue kamba ushuke porini kitanzini au jiwe mnyororo limeandikwa cocacola ukajinyonge huko,kwi! kwi! kwi! kwi!...mie nalog out
 
nammkumbuka huyu mdau aliwahi kunipiga ngeta miaka hyo pale kitanzini wakati napandisha kwenda mjini akanipora dumu la ulanzi ni kitambo sana

hahahhaha kapalampya wengi wamemwelezea huyu mbabe na visa vyake lakini cha kwake kinafurahisha na kuchekesha sana natamani kama ungetuhadithia mengi zaidi.
 
kulikuwa na ka mtindo flani songea miaka ya themanini. Nilikuwa std three tulipohamia songea nikakuta watoto wagomvi shuleni vibaya mno, ugomvi nje nje mkizipiga ukimdunda utasikia naenda kuagizia, hapo anamaanisha anakwenda kumtafuta mtu au kikundi waje wakudunde. Utashangaa mmetoka maeneo ya shule unakutana na wababe wanakusubiri kitakacho endelea hapo ni kichapo hahaaa

dah unanikumbusha pale songea ttc kulikua na kota mtaa wa chini na mtaa wa juu basi ukionekana mtaa usio wako kichpo chake hko.!uu-siniambie na kwenda kuiba viaz thn unachoma kabumbila..dah zaman raha
 
hahahhaha kapalampya wengi wamemwelezea huyu mbabe na visa vyake lakini cha kwake kinafurahisha na kuchekesha sana natamani kama ungetuhadithia mengi zaidi.

cool 9 alikuwa msumbufu tu na mbabe ila marehemu kipagati ndo alikuwa mwisho wa yote wa miaka ya 80s iringa watakuwa wanakumbuka drama za huyu mtu
 
Tupe basi stori zake je unamjua mdogo wake anayeitwa Van Dame wa magomeni?unasema kwao iringa mi najua kwao ni ubungo kwa baba yake na ndo alikokuwa anakaa na nyumba yao hadi leo ipo.kati ya yeye na ayati nani alikuwa mkubwa nasikia alikuwa na dada yake alikuwa anapiga naye? mkatabafeki usituache hewani tupe stori zake bwana,je jina lake la kuzaliwa ni nani mana hilo kool9 ni la kizungu?.
Ebwana Huyu mchizi R.I.P alikuwa balaa alikuwa ni pande la mtu ukimuona nilazima ukubali mwenyewe nadhani walikuwa na anaasili ya Kiarabu[Handsome fulani vile] alikuwa anaishi Ubungo Kibo alishawahi kuwa Shem wangu, Wadogo zake ni washikaji zangu mpaka leo mmoja anaitwa Salum na Akraby, Jamaa Ubongo mpaka Kibo yote walikuwa wanamtambua Cool 9 kama ngumi jiwe chokoza moto uwone,Nakumbuka siku moja alizinguana na Dada yangu kwny mambo yao ya kimapenzi akamwangaliaaa...huku akisikitika kulikuwa na nguzo ya chuma pembeni kwa hasira aliipiga ngumi moja nzitooo... nikaona kama nyumba inatikisika ilikuwa ni kwa Mzee Kumekucha nyuma ya Msikiti wa Kibo kwa wanaopafahamu mi nilikuwa bado mdogo niliogopa nakutoka mbio nikaona Jamaa kama muaji kwajinsi ile ngumi ilivyotikisa nguzo ya nyumba nilihisi ingetua kwny mwili wa Sister sasa hv angekuwa marehemu,
Kibo ulikuwa ukitaja jina tu Cool 9 kila mtu anatulia nakufunga mdomo kwajinsi mziki wake ulivyokuwa balaa,
Familia yake na Wadogo zake walikuwa wanaheshimika nakuogopwa kwajili ya Ubabe wa Mchizi
Baba yake anaitwa Yahya ni swala 5
Ila na yeye alikuwa anagonga ngumi vibayaaa... alikuwa hapigi Watoto wake zaidi ya kuwafungia ndani nakuanza kuzitwanga
Cool 9 na Bro wake fulani mcheza kareti ndio ilikuwa wakizingua anawaita nakufunga mlango kuanza kuzichapa nao.
Ni long tym ila ilikuwa nifamilia ya kipekee enzi hizooo.. kwa lyf style yao
Huwezi amini Mzee Yahya baba yake Cool 9 bado yupo fit mpaka leo hii na anadrive gari mwenyewe.
 
Back
Top Bottom