Ni nani huyu Cool 9 Jamani?

baada ya cool9 kuna kajamaa kalikuwa kanaitwa SHETANI ALIYEBARIKIWA naye alikuwa noma sana ingawa alikuwa hana mwili ni mwembamba na sio mrefu,yeye ngumi sio sana ila mateke na sarakasi anaweza kukuua lakini mpaka umkute sehemu zenye ukuta ndo anakubamizia,sehemu za wazi unaweza kumpiga,kutokana na ukorofi wake polisi walimwambia awe anaripoti kituon kila ifikapo jion,alikuwa mchafu chafu na akipendelea kushona vitenge shati na bukta,nilikuwa namfahamu sana huyu jamaa kipindi naishi iringa
 
Hivi shetani bado yupo hai maana alikuwa mtemi akienda dukani anawambia wampe bidhaa yeyote anayotaka bila fedha. Then anatimua zake
 
umenikumbusha miaka ya cool9 iringa nilikuwa niko primary sabasaba,cool9 alikuwa noma pale pote iringa town,nakumbuka mwaka 1994 mdogo wangu aligongwa na gari pale uhindini kwa sadrus na kufa papo hapo,cool9 alikuwepo karibu siku hiyo basi alimchomoa dereva na kumpa kichapo kitakatifu,pia alishawahi kumtemea traffic mate usoni na wala hakufanywa chochote,nimekumbuka mbali sana ingawa naumia sana

Pole sana kaka yangu namanyele najua jinsi gani unavyoumia.
 
huyo dame wa sinza anaitwa Ayubu mkobo alishachezea miaka yake mi 3 jela sasa yupo nasikia yupo kinondoni,alipotoka kakuta dingi kandei tayari halafu ndugu zake washauza nyummba yao kila mtu kasepa na chake hivyo akabaki anaganga njaa tu kinondoni,kuhusu yeye na kool9 nadhani dame mwenyewe anamjua vizuri huyu jamaa,tatizo la dame ngumi hawezi ila yeye ana nguvu tu hivyo anapigwa na watoto wadogo kila mara,kool9 alikuwa mwili nyumba halafu hadi kata alikuwa anaziweza yote anayoyafanya dame miaka ya karibuni alikuwa anamwiga huyu jamaa mana Dar nzima uliza hakuna asiyemjua huyu KOOL9.Halafu Dame alikuwa ni mwizi tu wa kukaba ngeta
huyu bwana alikuwa na nguvu na alikuwa ni jambazi mkubwa sana polisi wote walikuwa wanamwogopa,siku moja polisi walienda kwao kumkamata wakamkuta anapiga nondo walipomwona tu wakaanza kumbwela akatoka nje akaenda kuwaambia waondoke wakaondoka Dame naye alikuja kuiga tukio hili baadae ukiangalia matukio yote ya dame yalimwiga huyu jamaa.

daah huyo DAME namkumbuka sana enzi shule ya msingi Mashujaa ya Sinza wakati tupo wadogo tukimwona tu tunamkimbia na alishawahi kula chips na kudai chenji wakati halikuwa hajatoa hela
 
Hao ndo walikuwa wanaitwa "MAGANGWE" AU?

Iringa jamaa alikuwa anaogopeka kishenzi, ndo ilikuwa inadaiwa jamaa anachapa iringa nzima. Vijana wa leo kwa taarifa yenu enzi za mwalimu kulikuwa na mbabe wa darasa, shule, mtaa mkoa. Hao jamaa walikuwa balaa tupu usiombe ukanyage reli zao. Wanakudunda mbaya, siku hizi maisha yamekuwa peace sana, hakuna tena yale mambo ya ubabe
 
alikuwa ni mbabe wa dar na iringa pia,ana mdogo wake anaitwa van dame naye alikuwa mbabe wa magomeni pia,hawa jamaa ukoo wao ni noma!!
 
Mmmh mie Iringa nilienda kusoma tu nadhani ilikuwa baada ya hilo gharika la kina cul9 mana nakumbuka njia ya kitanzini tulikuwa tunaiogopa ilikuwa na sifa ambazo mie mpaka nimemaliza shule sikuwai kusikia tena ila paliendea kuogopwa sana na tulipita kwa tahadhari!

Mleta mada naona watu wamefunguka bado unataka zaidi nadhani kuna vitu bado unataka kusikia funguka basi. . i guess unataka kujua kilichopelekea kifo chake! kwa style hii ya maisha yake inaonyesha alikufa kwa the famous juliana enzi hizo mana umeme ulikuwepo ati!! kunyanyua tu mabinti utakavyo sidhani kama alipona. .
 
Haya, na ninyi wa Mbeya tuleteeni mikasa ya JOMBI

Lol. . jombi hakuwa mtemi nadhani wapo watemi enzi hizo wengine tulikuwa wadogo lakini nakumbuka madisko ya mby sifa yake kubwa ilikuwa ni vurugu za wanaojiona watemi labda watu wafunguke walete majina yao hapa! jombi sifa kubwa alikuwa mtu na heshima zake tu kumbe alikuwa nyuma ya ujambazi sugu mkubwa uliokua ukiendelea sijui alishatoka jela na kuokoka!
 
Mmmh mie Iringa nilienda kusoma tu nadhani ilikuwa baada ya hilo gharika la kina cul9 mana nakumbuka njia ya kitanzini tulikuwa tunaiogopa ilikuwa na sifa ambazo mie mpaka nimemaliza shule sikuwai kusikia tena ila paliendea kuogopwa sana na tulipita kwa tahadhari!

Mleta mada naona watu wamefunguka bado unataka zaidi nadhani kuna vitu bado unataka kusikia funguka basi. . i guess unataka kujua kilichopelekea kifo chake! kwa style hii ya maisha yake inaonyesha alikufa kwa the famous juliana enzi hizo mana umeme ulikuwepo ati!! kunyanyua tu mabinti utakavyo sidhani kama alipona. .

Naomba na mimi nijulishwe alikufa kwa ugonjwa gani kweli na ilikuwa mwaka gani??
 
umenikumbusha miaka ya cool9 iringa nilikuwa niko primary sabasaba,cool9 alikuwa noma pale pote iringa town,nakumbuka mwaka 1994 mdogo wangu aligongwa na gari pale uhindini kwa sadrus na kufa papo hapo,cool9 alikuwepo karibu siku hiyo basi alimchomoa dereva na kumpa kichapo kitakatifu,pia alishawahi kumtemea traffic mate usoni na wala hakufanywa chochote,nimekumbuka mbali sana ingawa naumia sana

mkuu tumesoma wote sababa miaka hiyo ya 1994 nilikuwepo enzi za mwl kisunda
 
ahsante ndugu ni thread hii imenipeleka mbali sana,jamaa mwenye thread cjui aliwaza nini ingawa kwa wengine inaonekana ya kizushi
Huyu dame mwaka 94 kuna siku nilienda kumwona rafiki yangu pale ubungo national housing nyuma ya bus terminal kuna primary school na secondary walikuwa wanaingia evening basi jamaa alikuwa na ugomvi na mwanafunzi mmoja wa secondary hapo shuleni zikaanza vurugu hadi walimu ikabidi wawaruhusu wanafunzi waondoke maana palikuwa hakushikiki hapo ndipo nilipoanza kumfahamu
 
kumbe na wewe unamjua dame mdogo wake kul9 tupe zaidi visa kaka.
 
umenikumbusha miaka ya cool9 iringa nilikuwa niko primary sabasaba,cool9 alikuwa noma pale pote iringa town,nakumbuka mwaka 1994 mdogo wangu aligongwa na gari pale uhindini kwa sadrus na kufa papo hapo,cool9 alikuwepo karibu siku hiyo basi alimchomoa dereva na kumpa kichapo kitakatifu,pia alishawahi kumtemea traffic mate usoni na wala hakufanywa chochote,nimekumbuka mbali sana ingawa naumia sana

Duh Namanyele, hata mimi nimesoma Sabasaba shule ya Msingi enzi hizo.....! Tulihamishwa toke shabaha Agh Khan pale Lugalo.... Baada ya muda kuna wanafunzi waliletwa tokea Azimio nakumbuka kukawa na mikondo miwili A na B.... Pale ndani ya uwanja wa sbasaba kulikuwa na ukumbi wa disco unaitwa Soweto.... Ndo nilipoanzia kumfahamu huyu jamaa anaitwa Kool nine... Kulikuwa na DISCO karibu kila J'mosi kuanzia saa 8 mchana. Na nakumbuka shule tulikuwa tunasoma hata J'mosi mpaka saa 6 mchana.
Na hii group ya wanafunzi iliyohamia tokea Azimio/Ama chemchem ndio iliyoleta mabadiliko ya ajabu pale sabasaba... Nidhamu yoote ikashuka, ikawa mara yangu ya kwanza kuona mwanafunzi anabishana na Mwl na kumkunjia ngumi duh, kukawa na makundi ya kupigana sana kuanzia pale shuleni... Dah umenifanya nivute kumbukumbu za enzi hizo...
Kuna jamaa alikuwa ana mkanda mweusi alikuwa anakaa Gangilonga alikuwa anaitwa Sempaya ..Wengi tulisubiri kuona kama itatokea atapambana na huyu mbabe mwenye nguvu nyingi -Kool nine..... Tulisubiri kwa hamu sana lakini sidhani kama ilitokea..Maana naye ingawa alikuwa mstaarabu alikuwa anaogopewa sana pia - Alikuwa anafundisha makaratee pale Kleruu pia na Mwalimu wa masarakasi Kundya - Pale chuo cha Kreluu.

Huyu Kool nine kufahamika Iringa na sehemu zingine haikuwa kazi rahisi... alipitia vipindi vigumu vya kuwachakaza viongozi wa magroup (Gangstars) mbalimbali pale Iringa... Aliwapa hard blasts mbaya na wakamjua...

Kulikuwa kuna notorious groups maeneo ya kihesa kuna jamaa alikuwa anaitwa Midaku, John Shura, Gerad Njanga, Laiton na kaka yake Juli na wengine wengi sikujui kama wapo hai...Kool nine aliwachakaza woote hawa na wafuasi wao kwa wakati tofauti... na wakamkubali na wakawa wana report kwake....
Huko Kitanzini kulikuwa na akina Sungu na gang lake nao hakuwaacha ..aliwapa mkong'oto wakainua mikono na kuwa wapole kwake....na kuwa marafiki pia bila kupenda.
Kulikuwa kuna mapolisi wakuogopewa enzi hizo .... akina Msangalufu na Mfalingundi (Sijui kama wapo hai) walimjua huyu jamaa wa miraba minne ....Kool nine.....Maana alikuwa anakwenda kuonyesha ubabe wake bar moja ilikuwa inaitwa Mwafrika Kichangani - pale opposite na FFU....

Namanyele nadhani iko siku tutaweka thread ya Iringa sabasaba , gangilonga, kichangani, wilolesi, chemchem kukumbuka enzi hizo.... Nimekumbuka mbaaaali sana sana rafiki yangu..Nimewakumbuka mpaka akina Fire, akina JB Kaduma, Kodo, Mkandawile, hawa jamaa majirani zetu pale Highlands secondary...
Pia nimewakumbuka na baadhi ya waalimu pale sabasaba.. Mh Komba, Mwl Mfiringe, Kasuga, Lupola, Mwinyi kidekeo hilo ni AKA alikuwa nachapa mboko sana, Mgina, sitaki, Mwaitebele, Seme, Simoko, Mandari, Mwl Said, Kuna mwl alikuwa anakunja ndita saaana Mwl Mohamed ha ha ha ha ha ha ha ... Jamani ya kale dhahabu .... (Sijui kama wote wapo hai)

Ila woote hawa walikuwa wanamjua huyu Kool nine .... Alikuwa anakatiza kote bila kizuizi....hata kumbi za starehe walimfahamu na hawakutia neno kwake.

Enzi hizo nilikuwa napita mitaa mbalimbali pale Iringa unakuta watoto wadogo wanajiita Kool nine... Wakimwigiza mambo yake!!! Alikuwa mtu maharufu sana wa wakati wake... (Kama akina Bruce lee, Van dame, Anord...etc)

Huyu jamaa ingekuwa nchi za wenzetu kama USA, UK, France wangemchukua kuwa Actor katika filamu za ubabe, Kwetu hapa Bongo ilikuwa si rahisi kuona vipaji vya watu wa aina yake enzi hizo... Ukweli alikuwa anapendeza sana kuwa ACTOR.
Mungu amurehemu na wengine....waliotangulia kwenye haki..... Duh nimekumbuka mbaaaaliii sana sana. Thanks!
 
duh huyu mdau 'Bengal Snake' salute sana kwa kumbukumbu mkuu

this is incredible
 
Back
Top Bottom