NI nani huyu anayepandikiza chuki dhidi ya serikali?

Bwana Macos, umenisikitisha sana kupost vitu vya kidini, hivi nyie watu mtabadilika lini? Nakushauri umuombe sana Mungu wako akuondolee hii dhambi ya ubaguzi. Sisi wote ni watanzania, tumekuja hapa duniani bila kitu chochote na tutaondoka hivyo hivyo. Tumia muda wako mwingi kufikiria namna ya kuiendeleza Tanzania na wewe mwenyewe. Acha udini, haijalishi kama wewe ni ccm, cdm au cuf, wote watapita lakini Tanzania yetu itabaki palepale. Mungu ibariki Tanzania.
 
CIMG2931.JPG
[IN ISLAMIC PASPECTIVE THIS IS NOTE RIGHT
 
Jamani mm Mbona katoa Matipo chuiz sasa wandugu Mbona tunaenda mbali Na kujitungia majibu nje ya Matipo chuiz ya mm..
Nafanya invijileshen tu..
 
Chuki inaletwa na ugumu wa maisha, chukulia mfano mdogo tu wa familia yako, baba anawalisha ugali wa "yanga" na kila siku alafu unamkuta baa anakunywa bia na nyama choma akiwa na machangudoa, je hautamchukia baba yako? kama ni umaskini basi wote tuwe maskini (tule ugali wa yanga). Sasa wenzetu wananunua nyumba za dola 400,000 then wanatuambia nchi yetu ni maskini?
Tunashuhudia wakitupiana maneno pale wanaingiliana kwenye ulaji alafu tuwachekee!!!
 
Wapo wana ccm wanaoipenda Tanzania na wanaimani kuwa vyama vya upinzani vikiingia haviwezi kubadilisha chochote, lakini kwa mfumo waliouweka wa kuwa na viongozi kibao wanaofanya kazi moja (eg DC, DAS, DED, na TD) katika wilaya moja, hata wafanyeje hakutakuwa na mabadiliko kwa kutumia mfumo huu. Haiwezekani nchi kubwa kama hii inakusanya kodi zinazoishia kwenye matumbo ya watu useme kutatokea mabadiliko, haiwezekani nchi ambayo hakuna anayeweza kumsema mwenzake wakati yeye mwenyewe anaogopa asisemwe akakemea rushwa, nchi kama hiyo ikasonga mbele. ccm ikikaa pembeni ikawaachia wapinzani hata miaka mitano (5), itakuja na mikakati mizuri sana kuliko inavyoangaika sasa. Kwa sasa sera zimewaishia ndo maana CHUKI haitakaa ikaisha mpaka siku watakapoondoka ikulu.
 
Back
Top Bottom