NI nani huyu anayepandikiza chuki dhidi ya serikali?

Yataisha haya..wala hotosikia tena baada ya 2015..ccm watam weka mkatoliki basi yataisha hata akiuza nchi sooote kimya...hata akiiuza madini yoooote media yote ita freeze...
Hata akibinafsisha banki kuu "( nbc) sotekimyaaaaa
hata akiuu kama ilivotokea pemba 2001..watasema saw
hata tukinunua tena rada bomu...mapadre kimyaaaaaa
basi hapo choko choko zitaisha
na kwa jamaa zangu chadema upepo utabadilika....kanisa sasa lita msa pot wa ccm jitayarasheni..kwani naamini hapo utaona upepo una badilika na cuf kuchukua nafasi ya 2 na cdm ya 3

huu ndio ukweli .na utabiri
 
Serikali yenyewe, kwa kutokuwajibika. Imeshindwa kudeliver social services,wizi wa viongozi, rasilimali tunazo kwanini hatuendelei? Hii imefanya wananchi kuchoka na kuwa na chuki.

Majibu kama haya na watu wakiangalia tofauti kubwa ya masikini na matajiri, na hao matajiri wakiwa ni viongozi wa serikali na familia au marafiki zao ndio yameleta chuki hizi.

Muulizaji: Mheshimiwa hivi unadhani ni kwanini pamoja na rasilimali zote nchi yako bado ni masikini?
Mwenyenji: Kwa kweli hata mimi sijui

NB: Jibu hili linatolewa mwenyenji akiwa na tabasamu pana la kidwanzi!! unategemea nini kama sio chuki kali kutoka kwa wadanganyika.
Baadhi ya majibu mengine maarufu na ya ujanja ujanja yako hapa

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/285214-jibu-maarufu-la-serikali-bungeni.html
 
dont talk to shit.....
mbona hii nichuki ya kiamani sana,mimi binafisi kungekua ha jinsi nyingene ya kuondooa serelikali hii ya sasa tz...ingekua bora,lakini kama kuna muozo wowote tunyamaze?kwani serekali dhaifu,yakibinafsi,nyanyasaji,onevu yakipuuzi na fisadi haifai kabisa kuongoza nchi yenye amani na utari mkubwa...hii chuki inayo pandikizwa havyombo hivi nivizuri na ndiyo jukumu lake kufaya hayo mambo kwa wananchi wanyonge wanao kandamizwa na serekali ya kinguvu,yakiuukandamizaji na yakibinafsi hii serekali haina tofauti na ile ya Saadamu Hussen ambayo iliona raia hawana haki bali wao ndiyo wenye haki ya kila kitu .
tuko kwenye harakati za ukombozi wa nchi yetu ......vyombo vya habari,wanaharakati na wengine tuko nyuma siku moja tutasimama tu...
 
Mzee Mwanakijiji swali lako ni gumu ila tutajitutumua hivohivo kujibu,ukiangali haraka haraka unaweza kusema ni vyama vya siasa pamoja na waandishi wa habari lakini pia ukiangalia kwa undani hasa utagundua ni serikali yenyewe japo hujaweka katika sehemu ya uchaguzi.Nikianza na vyama vya siasa (hasa chadema) hivi vimekuwa vikipita kila pembe ya nchi hii vikinadi sera zake na kufanya kazi zao za kisiasa katika kutaka kujiweka karibu na wananchi, bahati mbaya sana vyama vya upinzani haviwezi kupita vikifanya mikutano na kusifia mazuri ya serikali, hivi vyama vinapita kutangaza uzaifu wa ccm na serikali yake ndio kazi yao wala huwezi kuvilaumu kwani na vyenyewe vinataka kwenda magogoni ati!
Waandishi wa habari: Hawa wapo kazini, watavifuata vyama vya upinzani popote vinapoenda ili kukusanya habari, huwezi kuvilaumu kwani ndio kazi yao, wataripoti yale yanayosemwa majukwaani,watayapamba kuvutia wasomaji nasi wasomaji tutavutiwa na kuona kumbe hivi vyama vya siasa vinafanya kazi ya kufichua maovu ya serikali, na kwavile CCM hawajibu mashambulizi zidi ya serikali yake tunaona kumbe kweli Serikali inatuhadaa na mifano ipo, kumbuka List of shame pale Mwembe yanga na nyingine nyingi ambazo mpaka leo hatujasikia CCM wakikanusha kwa ufasaha na vikaeleweka kwa Wananchi, tazama vikao vya bunge vinavyoendelea huko Dodoma unaweza kusema CCM ndio wapinzani mapovu yawatoka kutetea vitu ambavyo hata bibi yangu kule shamba asingevitetea, mfano mtu anatetea fungu la kilimo na kuunga mkono lakini wakati huo analalamika kwamba fungu la bajeti iliyopita hakupata kitu, sasa hapa utasema vyombo vya habari visiandike, vitaandika na mimi nikisoma nitaona kweli Serikali inatudanganya, wapinzani wakisimama na kufafanua ndio kabisa nitaona hii serikali hainifai.
 
Wewe tume ya Katiba kwa kuwa umevimbiwa na kwa kuwa unafaidika kwa namna moja ama nyingine ya uozo na ufisadi wa viongozi wa CCM lazima useme hivo..
Unaona kama wananchi wanavokuwa na uelewa wa mambo yanavoenda wewe kwako sio habari njema.
unategemea watanzania watakuwa ni walewale wa zidumu fikra za mwenyekiti..
Pole sana..


1) Vyombo vya habari,kupitia waandishi wenye malengo hasi kama wewe
2) Chadema
3) viongozi wa kidini
 
nuksi zote alisababisha huyu

42314-004-677D1E59.jpg

Wenye ubongo mdogo kama wewe hujaribu kuelezea failures na mapungufu yao kwa kuwabebesha wengine responsibility au kusingizia historia kama ilivyo kwa nchi zetu za Afrika. Hatushangai kusikia ukitoa sababu za kushindwa kufanya kazi reli ya kati kuwa wajerumani hawakuijenga vizuri. Nyerere aliachia ngazi miaka 28 iliyopita na hayuko duniani 14 yrs bado unaota anaongoza nchi. unafikiri kinyumenyume mkuu. Rwanda wametoka kwenye genocide only 19 yrs lakini wanaondoka. Acha mawazo mgando we dont work for the past but present and future
 
Kwa mtizamo wangu pamoja na jitihada nzuri za kufichua ufisadi unaofanywa na CDM, bado pia wao na wafuasi wao ndani ya serikali wanatumia mbinu chafu za kufitinisha wananchi na serikali yao. Kwa mfano suala la Dr. Ulli, kwa kiasi kikubwa wafuasi wa CDM pamoja kuoonekana kama wanasikitishwa na masahibu yaliyompata lakini pia wanatumia suala hilo kama ngazi ya kupata umaarufu. Sasa tunapata mashaka kutoamini kwamba ni wafaidika wa madhila yaliyompata Dr. Nalisema hili kwa vile pale Chacha Wangwe alipotofautiana kimsimamo na viongozi wa chama chake alifariki, hatuwezi kusema moja kwa moja aliuwawa lakini kuna utata mwingi hapo. Hata kwa suala la Dr. mgomo ulianza kupoa ndipo alipotekwa na kuteswa. Swali ambalo najiuliza kwa nini Serikali imteke wakati huu ambapo mgomo ulikuwa hauna nguvu kama wafuasi wa CDM wanavyo "propagate" . Ndipo tunapata mashaka kwamba yawezekana hii ni moja ya njia chafu ya kupandikiza chuki kwa Serikali.
 
The Boss,

You have suggested the right answer. Kwa kuongezea Mzee Mwanakijiji - hakuna anayechochea ila utawala wa CCM hauna tena ile popular mandate na kwa kukosa itikadi pamoja na Dira upepo kidogo tu unawasumbua. Watahangaika sana kumtafuta mchawi but for this collapsing monster hizi ndizo alama na ishara za kuanguka au Mwisho wa CCM.

Hata Kama watatumia nguvu vipi it has just weathered and outlived its purpose. Anguko limeanzishwa na CCM wenyewe mwaka 1992 walipofuta bila mjadala Azimio la Arusha which was the central pillar. They are just revolving around the vicious circle. Let me ask you ni nchi gani duniani iliyowahi kupata maendeleo kwa kutumia wawekezaji. A simple ABC in economics you simply create capital fight actually is just imperialism through the back door.

The old Soviet Union did the same mistake and KGB couldn't stop the disintegration , Russia has come back after kicking the Multinational oil companies sasa mwache JK adanganywe na what the call investors and the bogust PPP they are trying to embrace. Very soon CCM will follow the route of KANU and it's coming very fast !! Keep on scratching you heads Watz,?.?
 
Wenye ubongo mdogo kama wewe hujaribu kuelezea failures na mapungufu yao kwa kuwabebesha wengine responsibility au kusingizia historia kama ilivyo kwa nchi zetu za Afrika. Hatushangai kusikia ukitoa sababu za kushindwa kufanya kazi reli ya kati kuwa wajerumani hawakuijenga vizuri. Nyerere aliachia ngazi miaka 28 iliyopita na hayuko duniani 14 yrs bado unaota anaongoza nchi. unafikiri kinyumenyume mkuu. Rwanda wametoka kwenye genocide only 19 yrs lakini wanaondoka. Acha mawazo mgando we dont work for the past but present and future


Nimeipenda sana hapa!
 
Ni wale wanaoona kabisa kuwa kuwa mfalme yuko uchi lakini kwa unafiki wao wanamsifia alivyojisetiri...kumbe anachekwa hadi na watoto wadogo anapopita barabarani na kuonekana kama chizi!
 
Muda !
Kuna chuki imepandikizwa dhidi ya serikali yetu; chuki ambayo inawafanya watu wawe na hamu ya kuona serikali iliyoko madarrakani inaangushwa au kuanguka (collapse). Chuki hii inawafanya baadhi ya watu kufanya kila wawezalo kufichua uozo na uovu mbalimbali serikalini. Ni chuki hii inayowafanya watu hata kuamua kubadili uanachama kutoka chama tawala kwenda vyama vingine. Ni chuki ambayo inaonekana kuzidi kukua na kuongezeka kila siku ijayo.

Swali langu ni NANI HASA (mwenye wajibu wa kwanza kabisa) ANAYESABABISHA AU KUPANDIKIZA CHUKI HII?

a. Waandishi wa habari
b. Vyama vya Upinzani (wanasiasa wa upinzani)
c. Wanaharakati wa kisiasa (political activists)
d. Mitandao ya Kijamii
e. Serikali yenyewe
f. Vyote hapo juu!

Lakini swali la msingi ni jinsi gani mhusika huyo anapandikiza chuki hiyo?


Tukijua ni nani anapandikiza chuki tutatarajia hatua dhidi yake....
 
Back
Top Bottom