Ni nani anaemiliki kiwanda cha ARV feki?

Idimi inawezekana kuna "disagreement" maana ninavyofahamu kile kiwanda walipata mbia nadhani toka Ujermani kwa ajili ya kutengeneza hizo dawa na lazima zilihakikiwa kabla ya kuanza kusambazwa
Uwezekano huo upo, kwani kwenye kila dili migongano haikosekani. Suala kubwa ni namna bora ya kutatua migongano hiyo. Lakini all in all, watawalipaje hawa waathirika waliokunywa dawa feki?
 

Nimesoma mahali hapa hapa JF, kwamba kiwanda kile ni mali ya familia ya akina Madabida. Ni makada maarufu wa magamba kwa mkoa wa Dar. Tutajibeba mwaka huu

Ni kweli kiwanda kilichositishwa kutengeneza ARVs ni mali ya ukoo wa Ramadhani Madabida na mkewe ambae ni mbunge wa CCM!! Hii familia iliingia kwenye ulingo wa siasa kama njia ya kukwepa deni kubwa la serikali wanalodaiwa baada ya kununua kiwanda toka PSRC.

Bwana madabida ni mjumbe wa NEC ya ccm na sasa hivi yuko kwenye kuwania uenyekiti wa ccm mkoa wa Dar. wakati mkewe amebwagwa kwenye kugombea uenyekiti wa UWT mkoa huo huo. Hawa jamaa ni rafiki wa karibu wa mkweree na ndio maana wanataka kufanya kama alivyofanya swahiba wao yaani kufanya chama mkoa wa Dar ni cha familia yao!!!
 

Nimesoma mahali hapa hapa JF, kwamba kiwanda kile ni mali ya familia ya akina Madabida. Ni makada maarufu wa magamba kwa mkoa wa Dar. Tutajibeba mwaka huu

Huo ndio ukweli.Niliwahi kufanya field hapo TPI,zamani kidogo. kipindi hicho kiwanda cha kutengeneza ARV kikiwa bado kwenye makaratasi.Kulingana na maelezo ya meneja,serikali ilikuwa ina hisa katika kile kiwanda(wewe haujiulizi waziri amepata wapi nguvu za kumsimamisha mkuu wa kitengo cha quality assurance wa kiwanda),hii inamaanisha kuna uwezekano serikali ndio yenye hisa nyingi zaidi hivyo kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi.Pia kulikuwa na tetesi mama Ndomondo (yule mama aliyekuwa director wa TFDA) anahusika na kiwanda cha TPI.Hapa hakuna cha dawa feki,TPI watakuwa walichemsha wakati wa production wakaamua kufunika kombe mwaharamu apite.
 
ukifikiria wangapi watakuwa wameathirika na wangapi watakuwa wamepoteza maisha kwa kutumia dawa hizo inasikitisha.......adhabu ya kufungia kiwanda haitoshi wanastahili kunyongwa mara moja jamani tufanyeje hawa watu hawastaili kuishi
 
Huo ndio ukweli.Niliwahi kufanya field hapo TPI,zamani kidogo. kipindi hicho kiwanda cha kutengeneza ARV kikiwa bado kwenye makaratasi.Kulingana na maelezo ya meneja,serikali ilikuwa ina hisa katika kile kiwanda(wewe haujiulizi waziri amepata wapi nguvu za kumsimamisha mkuu wa kitengo cha quality assurance wa kiwanda),hii inamaanisha kuna uwezekano serikali ndio yenye hisa nyingi zaidi hivyo kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi.Pia kulikuwa na tetesi mama Ndomondo (yule mama aliyekuwa director wa TFDA) anahusika na kiwanda cha TPI.Hapa hakuna cha dawa feki,TPI watakuwa walichemsha wakati wa production wakaamua kufunika kombe mwaharamu apite.

wamiliki ni Watanzania ngozi nyeusi wakiongozwa na Rama Madabida. wamefanya kazi kubwa kufikia hapo kutokana na ushindani toka makampuni ya watanzania wenye asili ya India! kuna uwezekano wa uzembe wakati wa kuzalisha hizo dawa ama hujuma! ushauri ni kwa bodi ya wakurugenzi na menejimenti kuwa makini sana ktk uzalishaji wa madawa yenye viwango!
 
[h=2]Member of Parliament CV[/h]
GENERAL
SalutationHonourableMember picture
1593.jpg
First Name: Zarina
Middle Name: Shamte
Last Name:Madabida
Member Type:Special Seat
Constituent: No Constituency
Political Party: CCM
Office Location: Box 3850, Dar Es Salaam
Office Phone: +255 754 400804
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail: zmadabida@parliament.go.tz
Member Status: Current Member
Date of Birth 30 April 1953
EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start DateEnd DateLevel
Wailes Primary SchoolPrimary Education19611967PRIMARY
Jangwani Secondary SchoolO-Level Education19681971SECONDARY
University of Dar Es SalaamBSc. (Pharmacy)19761979GRADUATE
University of Ghent, BelgiumPharmacist19811981CERTIFICATE
Government Chemist Technical SchoolDiploma (Chemical Analyst)19721974DIPLOMA
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From DateTo Date
The Parliament of TanzaniaMember - Special Seat20102015
Tanzania Pharmaceutical IndustryDirector1997Todate
Mpewani PharmacyDirector19941997
NAPCOMarketing Manager19811993
Government ChemistsChemical Technician19741975
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position FromTo
Chama Cha Mapinduzi, CCMChairperson - UWT (Dar Es Salaam Region)2008
Chama Cha Mapinduzi, CCMChairperson (Ward Economics)2006
Chama Cha Mapinduzi, CCMGuardian (NAPCO Branch)1983
Government ChemistsChemical Technician19741975
 
[h=2]ednesday, September 21, 2011[/h] [h=3]Mbunge Bi Zarina Madabida Awacharukia Wanaharakati[/h]
Mbunge wa Viti Maalum Bi.Zarina Madabida akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Mikocherni Dar es Salaam jana .Pamoja na mambo mengine pia aliwataka wana harakati kumwekea wakili Mkuu wa wilaya ya Igunga Bi.Fatuma Kimario katika kesi aliyoifungua wilayani humo kupinga udhalilishaji aliofanyiwa na wanachama wa Chadema hivi Karibuni.
MBUNGE wa Viti Maalum (CCM),Bi. Zarina Madabida amedai kushangazwa na ukimya uliofanywa na wanasheria na wanaharakati wanawake kutojitokeza kumtetea Mkuu wa Wilaya ya Igunga Bi. Fatuma Kimario ambaye alidhalilishwa na wafuasi wa CHADEMA kama wanavyofanya kwa wanawake wengine ambao wamefanyiwa vitendo hivyo.

"Nashindwa kuelewa TAWLA,TGNP,TAMWA na wanaharakati wengine wanaotetea haki za wanawake wamekaa kimya bila kutolea maamuzi suala tuwaeleweje. Hii inanipa mashaka makubwa,"alisema.

Bi. Madabida alisema kuwa wanaharakati hao siku zote wapo mstari wa mbele kutetea wanawake na watoto ikiwemo jamii, lakini anashangazwa na ukimya kuhusu utetezi wa Bi. Kimario.

Alisema mbona wanawake wakiwa wananyanyaswa wanakuwa mstari wa mbele kutetea lakini iweje leo hii aliyefanyiwa hivi ni mwanamke tena kiongozi lakini wamekaa kimya tuwaeleweje?.

"Hawa tuwaeleweje ni wanawaharakati au wao wanavyama vingine vya siasa, utetezi wao huko wapi inanipa mashaka,"alisisitiza

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Chama Cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA)Bi.Analelia Nkya alipoulizwa juu ya kimya walichonacho kuhusu kudhalilishwa na Bi. Kimario alishindwa kutoa tamko kuhusu udhalilishaji huo kwa madai kuwa wao wanashughulikia masuala ya jamii na wala siyo ya mtu mmoja.

"Sisi tumekuwa tukizungumzia masuala ya jamii na sio suala la mtu mmoja sasa wewe kama mwandishi ukiniuliza tumekaa kimya kuhusu kudhalilishwa kwa mwamamke mwenzetu nakushangaa sana,"alisema Bi. Nkya.

Hivi karibuni wafuasi wa CHADEMA walimkamata Mkuu huyo wa Wilaya na Kumdhalilisha kwa madai kuwa alikuwa anapanga njama za kuupatia ushindi CCM katika uchaguzi mdogo unaoendelea jimboni humo,wakati alipokuwa akizungumza na watendaji wa wilaya hiyo.​
 
wamiliki ni Watanzania ngozi nyeusi wakiongozwa na Rama Madabida. wamefanya kazi kubwa kufikia hapo kutokana na ushindani toka makampuni ya watanzania wenye asili ya India! kuna uwezekano wa uzembe wakati wa kuzalisha hizo dawa ama hujuma! ushauri ni kwa bodi ya wakurugenzi na menejimenti kuwa makini sana ktk uzalishaji wa madawa yenye viwango!

Ushindani sio mkubwa kama unavyofikiria ndugu yangu,asilimia kubwa ya dawa za TPI zinauzwa MSD na kwa maneno yake mwenyewe Madabida kwa miaka kadhaa walikuwa hawajawahi kukidhi mahitaji ya soko.Tatizo kubwa liko hapo kwenye kutengeneza dawa zenye ubora na mbaya zaidi makosa yanapotokea wakati wa kutengeneza dawa au wakajua kabisa kwamba wametengeneza dawa zisizokuwa na ubora wa kutosha,bado wanaziingiza sokoni.TFDA nao hawafanyi ukaguzi wa mara kwa mara katika hivi viwanda vyetu,nao wanajisahau wakijua hakuna anefuatilia.
 
Ramadhan Madabida aligombea ubunge kilwa na kushindwa na mgombea wa cuf bwn Bungala aka b.wege,ni mmiliki wa hiki kiwanda na mkewe Zarina mwenyekiti wa uwt wa Dsm aliyepita.
Ofisi zake zipo pale mikocheni opposite na talk of the town,kwa warioba
 
Inaweza kuchukua muda lakini tushuru Mungu maana na Ritz kaanza kuuona mwanga sasa, bravo.
 
Dawa ya binadamu ni kumuwekea sheria kali kwenye mali ya umma.
 
Back
Top Bottom