Ni nani aliyeleta na aliyetengeneza uchawi hapa duniani?

Kaka naona umeamua kunibana zaidi,kiukweli jina halisi la mtu huyu unaemtaka wewe silifahamu ila historia ya uchawi ndo iko hvo.

Ha ha ha ha ha ha! kila la kheri mkuu! Watu wa mungu munatakiwa kuyajua haya!!

Maana mimi naelewa mungu hayupo kwa sababu nyingi,.
 
Ha ha ha ha ha ha! kila la kheri mkuu! Watu wa mungu munatakiwa kuyajua haya!!

Maana mimi naelewa mungu hayupo kwa sababu nyingi,.

Kaka naona umefurahi sana ila habari za uchawi ni ndefu sana na ziko wazi ila nimekujibu kitaalam na kwa kifupi ili maswali yapungue, Sasa hilo la kutokuepo kwa mungu nalo jipya ila mi nataka unipe sababu moja tu inayokufanya usiamini uwepo wa mungu
 
Mungu hayupo kwa misingi ya mafundisho na mambo yanayoelezwa kwenye vitabu vyake, ukilinganisha na historia yetu pamoja na maisha tunayoishi.

maana haiwezakani mungu aliyetuumba sote mwengine waendelee kumjua, wengine wapelekewa taarifa kwamba kuna mungu aliyetuumba.?

haiwezakani kabisa mungu mwenye maarifa, upendo na nguvu za ajabu kuumba mtu na dunia yenye uchawi, njaa, vita, magojwa wakati uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauna majanga yote hayo inawezekana?
 
Kaka acha kulalamika toa sababu iliyoshiba inayokufanya usiamini kua mungu yupo sio kusema njaa,vifo, magonjwa ndo iwe sababu hizo ni athar za kimazingira,kwa mfano mi naamini mungu yupo kwasababu sina ujanja wa kupata kila nachokitaka
 
Huyu mungu wenye upendo na maarifa mengi kwa nini? aumbe kiumbe tena aanze kukipima? wakati uwezo wa kuumba kiumbe ambacho hakifanyi maovu kama anavyotaka inawezekana? Huyu mungu yupo? kweli. wiseboy saidia kujibu hili swali.

Basi na wanafunzi vyuoni wawe wanapewa vyeti tu

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Chanzo cha uchawi ni Nimrod wakat anajenga mji wa Babeli.

Baadae ntashusha nondo kwa ushahidi zaidi.
 
Wenyewe wachawi wanapitia hiz post zenu wanawacheka mnavyohangaika kujua uchawi,kumbuka nasikia uchawi una miiko yake na mwiko namba moja ni sili, mkeo,ndugu,mtoto,mzazi wako anaweza kuwa mchawi na ukuishi nae usijue kama ni mchawi
 
Uchawi ni elimu kama zilivo elimu nyingine ambazo watu husoma na kujifunza na elimu zote ni zake mwenyezimungu,amini ya kwamba heri na shari zote zinatoka kwa mungu kama mtihani kwa mwanadamu . mungu akitaka jambo huwa na asipotaka jambo basi haliwi.
Sasa Uchawi kama Uchawi ni elimu ambayo ilishushwa duniani na malaika wawili wakijulikana kama Haruta na Maaruta katika mji wa babel enzi hizo na watu walijifunza kama elimu nyingine ya kawaida kwa matumizi ya kawaida, Sasa binadam wa enzi hizo walienda mbali sana juu ya elimu hiyo na kuanza kumuasi mungu kwa kuitumia elimu hyo vibaya kwa kuwadhuru wengine na hata kufikia hatua ya kumuona mungu si chochote ndipo mungu alipoamuru malaika waende duniani kuchukua nyaraka za elimu hyo ila tayar baadhi ya watu walikua washakua na ujuzi kidogo juu ya elimu hyo na ndo leo hadi Sasa watu wanarithishana.
Kwa hiyo kaka uchawi ni elimu kutoka kwa mungu kama vile biology na chemistry na wala hakuna kiumbe yoyote alienzisha wala kumiliki elimu hii na ndo mana hao wachawi wenyewe wanapata shida sana kumdhuru mtu na wengine hushindwa kabisa na kutulia tulii.

Kwanza kabisa mungu wa waislamu ni tofauti kabisa na Mungu wa Wakristo. Sina nafasi leo ya kufafanua hili ila kwa kifupi tu Mungu anayehubiriwa na Wakristo wa kweli ndiye muumba wa vyote ilhali yule anayehubiriwa na waislamu ni kiumbe tu ambacho kilikuwa malaika wa mwanga na kuasi na kuwa malaika wa giza.

Ukishajua hilo, ndio sasa unaweza kuona kwamba Mungu wa kweli hahusiki na wala hakuumba uovu au uchawi kama unavyosema, bali kile kiumbe chake kilichoasi ndicho kilileta uovu wote ikiwa pamoja na uchawi.

Uchawi sio kitu kingine bali ni kutumia uwezo wa binadamu wa kuamua kwa kushirikiana na roho chafu (shetani na malaika zake) kufanya uovu.

Kamwe Mungu wa kweli hakuumba uchawi, uchawi ni tokeo la kuanguka kwa Luciferi na wanadamu kutoka katika utukufu wa Mungu.

Kama unataka kuushinda uchawi, basi ishi kama mtoto wa Mungu Mwenyezi (Yesu Kristo) nawe hao wachawi watakuwa chini ya miguu yako.
 
Maneno yako muafaka sana ni kweli elimu hiyo ililetwa duniani iwe kama test kwa mwanadamu,na kuongezea zaidi hao wachawi pia hushirikiana na mwalimu wao mkubwa ambaye ndio shaitwaani yule tunayemjua siku zote.Lakini kwa kuongezea tuu,hiyo elimu sisi waafrika tumeshindwa kuitumia vizuri,na kama tungeliweza fanya hivyo basi naamini leo hii dunia ingetuheshimu sana kwa jinsi tungelikuwa na uwezo wa kutatua matatizo mengi yanayoikumba hii dunia ya sasa.Kwa mfano uganga ambao huwa unashabihiana na uchawi siku zote labda leo hii ungechanganywa pamoja na uchawi waafrica tungeweza solve problems nyingi za kiafya hapa duniani.Huku maulaya tungekuwa tunaingia bila kutumia usafiri wa anga tungekuwa na uwezo wa kufika kwao through kusafiri kwa ungo na hata immigration prwa moderators,yaani ocess tusingekuwa tunapitia lakini kwa ubinafsi wetu sisi waafrika tumeshindwa kuufanya uchawi kuwa ni alimu ambayo inayoweza ikafundishwa darasani kama vile wakati unapofundisha physics au masomo mengine,hili lingelikuwa nalo liwe somo maalum Africa.Nimesoma malalamiko ya mtoa hii thread ya kufutiwa topic zake hata mimi ninamuunga mkono kwa hilo maana watu ka mimi tumegeuzwa weeping boy wa hawa sijui wanaojiita moderators,wanachagua baadhi ya watu humu na kuwafanyia ushenzi wa ,mara huruhusiwi changia kitu au mara nyingine topic kupotezwa bila hata ya notification yeyote ile.Mimi hapa nimeamuaga kupageuza sehemu ya kupita tuu na in fact i am no longer very serious like before with this forum na ninawashangaa sana sijui ni kwa nini paranoia imewaingia hawa moderators kwa baadhi ya watu humu,hapa tupo kila mtu kutoa mawazo na mchango wake kwa lugha ya wageni wanasema frredom of expression but inavyoonekana wanajaribu kutaka tufikiri jinsi wanavyofikiria wao,tamati.Mr Murage Msherwampamba.

"Maneno yako muafaka sana ni kweli elimu hiyo ililetwa duniani iwe kama test kwa mwanadamu,na kuongezea zaidi hao wachawi pia hushirikiana na mwalimu wao mkubwa ambaye ndio shaitwaani yule tunayemjua siku zote"

Kwa maneno yako hapo juu unapotosha ukweli kwani unasema Mungu alileta uchawi kama test halafu unasema mwalimu wa wachawi ni shetani. Manake unasema Mungu ameshirikiana na shetani katika kuleta na kueneza uchawi, hili ni uzushi mbaya sana ndugu yabidi kubadilisha usemi wako na kutubu na pia anza kujifunza ukweli halisi kupitia YESU KRISTO aliye njia, ukweli na uzima.
 
Uchawi ni elimu kama zilivo elimu nyingine ambazo watu husoma na kujifunza na elimu zote ni zake mwenyezimungu,amini ya kwamba heri na shari zote zinatoka kwa mungu kama mtihani kwa mwanadamu . mungu akitaka jambo huwa na asipotaka jambo basi haliwi.
Sasa Uchawi kama Uchawi ni elimu ambayo ilishushwa duniani na malaika wawili wakijulikana kama Haruta na Maaruta katika mji wa babel enzi hizo na watu walijifunza kama elimu nyingine ya kawaida kwa matumizi ya kawaida, Sasa binadam wa enzi hizo walienda mbali sana juu ya elimu hiyo na kuanza kumuasi mungu kwa kuitumia elimu hyo vibaya kwa kuwadhuru wengine na hata kufikia hatua ya kumuona mungu si chochote ndipo mungu alipoamuru malaika waende duniani kuchukua nyaraka za elimu hyo ila tayar baadhi ya watu walikua washakua na ujuzi kidogo juu ya elimu hyo na ndo leo hadi Sasa watu wanarithishana.
Kwa hiyo kaka uchawi ni elimu kutoka kwa mungu kama vile biology na chemistry na wala hakuna kiumbe yoyote alienzisha wala kumiliki elimu hii na ndo mana hao wachawi wenyewe wanapata shida sana kumdhuru mtu na wengine hushindwa kabisa na kutulia tulii.
elimu murua kabisa, pata kitabu udadadvue vizuri
 
Attachments

  • Witchcraft_Free_Book.pdf
    806 KB · Views: 116
wiseboy utafiti na wadau wengine mnaoamini kwamba watu tumeubwa na Mungu naomba mnijuze aliyeumba uchawi ni nani? na mtu wa kwanza kueneza uchawi hapa duniani ni nani?

Kama ni sheteni anahusika katika maswala ya uchawi,! shule za shetani za kufundisha uchawi ziko wapi? kwa nini wachawi wananguvu kubwa kiasi kwamba Mungu ameshidwa kuwaagamiza.?
Bush land unakumbuka vizuri mti wa kati wa ujuzi wa mema na mabaya? Mambo yote yalianza pale Eva alipolila lile tunda na kishapo kumpa Adam!
Kumbuka ule mti unaitwa MTI WA UJUZI WA MEMA NA MABAYA

Wachawi hawana nguvu kubwa kuliko Mungu wangekuwa nayo dunia ingeshaangamia, anachokifanya Mungu ni kuangalia na kuweka vizuri hesabu ya kila mmoja mpaka siku ya kiama
 
Last edited by a moderator:
Kwanza kabisa mungu wa waislamu ni tofauti kabisa na Mungu wa Wakristo. Sina nafasi leo ya kufafanua hili ila kwa kifupi tu Mungu anayehubiriwa na Wakristo wa kweli ndiye muumba wa vyote ilhali yule anayehubiriwa na waislamu ni kiumbe tu ambacho kilikuwa malaika wa mwanga na kuasi na kuwa malaika wa giza.

Ukishajua hilo, ndio sasa unaweza kuona kwamba Mungu wa kweli hahusiki na wala hakuumba uovu au uchawi kama unavyosema, bali kile kiumbe chake kilichoasi ndicho kilileta uovu wote ikiwa pamoja na uchawi.

Uchawi sio kitu kingine bali ni kutumia uwezo wa binadamu wa kuamua kwa kushirikiana na roho chafu (shetani na malaika zake) kufanya uovu.

Kamwe Mungu wa kweli hakuumba uchawi, uchawi ni tokeo la kuanguka kwa Luciferi na wanadamu kutoka katika utukufu wa Mungu.

Kama unataka kuushinda uchawi, basi ishi kama mtoto wa Mungu Mwenyezi (Yesu Kristo) nawe hao wachawi watakuwa chini ya miguu yako.

Nikweli kabisa kaka hilo liko wazi kua mungu wa waislam na mungu wa wakristo ni vitu viwili tofauti,labda nisaidie kitu kimoja kaka, mungu wa waislam anaitwa nani na yule wa wakristo anaitwa nani?pia unasema uchawi ni matokeo ya binadam kutumia uwezo wake wa kuamua kwa kushirikiana na shetani na malaika zake, swali
1 ) unaamini kabisa ktk dini yako binadam ana uwezo wa kuamua jambo na likawa?
2) mungu wenu ninyi ndo alowafundisha kua shetani nae ana malaika zake?au huwajui malaika ni viumbe wa aina gn na wameumbwa kwa kazi gn?
 
Bush land unakumbuka vizuri mti wa kati wa ujuzi wa mema na mabaya? Mambo yote yalianza pale Eva alipolila lile tunda na kishapo kumpa Adam!
Kumbuka ule mti unaitwa MTI WA UJUZI WA MEMA NA MABAYA

Wachawi hawana nguvu kubwa kuliko Mungu wangekuwa nayo dunia ingeshaangamia, anachokifanya Mungu ni kuangalia na kuweka vizuri hesabu ya kila mmoja mpaka siku ya kiama

Tafadhili ya huo mti ni kufanya ngono, unakubaliana na mimi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom