Ni muda Sasa wa serikali kutoa muongozo kuhusu uhamisho wa Mbarali

fullcup

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
806
2,182
Ndugu wana jamvi nisicheleweshe muda.

Mwaka Jana mwezi Novemba serikali ilitoa katazo la kufanya shughuli za kilimo Kwa maeneo kadhaa na kuidhinisha uhamisho wa baadhi ya vijiji. Mwezi Disemba waziri mkuu alifuta GN 28 na kufanya marekebisho ya maeneo ya kuhama na kufanya shughuli za kilimo lakini Madibira phase two na Mnazi yakabaki kwenye katazo.

Wananchi hawakulima maeneo hayo Kwa kuamini kuwa kiangazi watalipwa fidia na kuhamia maeneo mengine Kama alivyosema mtaalamu wa tathimini katika mikoutano ya maeno hayo. Wakati wa uchaguzi mdogo baadhi ya makada wakitumia majukwaa kutangaza kuwa wakiichagua CCM wataendelea na shughuli za kilimo katika maeneo hayo lakini mpaka Sasa hakuna.

Mwezi Oktoba alipita mhifadhi kwenye vijiji na kutangaza kuwa GN 754 ndio inayofanya kazi na ni marufuku kufanya shughuli za kibinadamu katika mipaka mipya. Ikumbukwe kuwa mipaka mipya iliwekwa katika upanuzi wa hifadhi lakini inaanza kufanya kazi huku wananchi wakiwa hawajalipwa fidia na hawajahamishwa. Yaani watu wanaishi kwenye maeneo hayo kusubiri fidia bila kufanya chochote yaani hakuna kufuga Wala kulima wapo tu.

Mwezi Novemba mbunge alitembelea vijiji vilivyoathirika. Hakusema Kama fidia wananchi watalipwa lini na Kama watalima maeneo hayo kwani ni msimu wa pili Sasa way wapo tu hawajui hatma Yao.

Ni muda Sasa Kwa serikali kuja na kauli ya kuongoza wananchi Hawa. Wajue wataruhusiwa kulima maeneo hayo wakati wakisubiri tathimini na fidia au walipwe fidia. Kwa upande wa fidia ni changamoto maana mpaka Sasa tathimini haijafanyika na mvua zimeanza hivyo ni ngumu kupima mashamba na viwanja lakini ni Bora waseme Neno na roho zetu zitapona.
 
Back
Top Bottom