Ni muda muafaka CCM ikaunda kurugenzi za kisekta, hivi wizara ya Ardhi imeshindwa kueleza Samia alivyowapa watu ardhi dhidi ya upotoshaji wa Lissu?

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,009
20,684
Nashangaa wizara ya Ardhi inaposhindwa kujibu propaganda za Lissu kwamba awamu ya sita imekuwa ikinyanganya watu ardhi. Serikali iliunda kamati ya mawaziri ambayo ilipitia migogoro ya ardhi, na watanzania kwa maelfu, waligawiwa ardhi iliyokuwa Ina mgogoro na hifadhi za taifa au taasisi za umma, sioni hili likisemwa kwa sauti kubwa.

Hapa Kuna mawili, moja wizara imeshindwa kuwasiliana na umma, japo Ina raslimali zote, ikiwamo fedha na maafisa mawasiliano, na kama hawatoshi, ipo idara ya habari maelezo. Wameshindwa kuifikishia jamii ujumbe huo, wanafanya ni ujumbe wa kupita.

Pili, kama Waziri ameshindwa pamoja na wizara yake, nadhani ni muda sahihi kwa CCM kujisemea Sasa, kwa kuunda kurugenzi za kisekta ambazo zitasemea na kufanya uchambuzi masuala ya sekta mbalimbali ikiwamo ardhi, madini,afya, TAMISEMI, na kadhalika. CCM ifanye reforms za mfumo wake kuangalia hayo.

Hapa ndipo gepu la lukuvi linaonekana, huwa anasema mapema na kwa wakati. Hata mgogoro wa mabwepande, lukuvi asingemuacha gwajima anahangaika pamoja na mkuu wa Mkoa, ungemuona tayari Yuko saiti, ana mapendekezo kwa Rais na wananchi.
 
Back
Top Bottom