Ni mkoa gani Tanzania kinafanyika kilimo Cha umwagiliaji?

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,678
Kama unataka Mali basi utaipata shambani, Mimi nimeamua kuunga juhudi nikashinde na kuteketea shambani huko labda tutatokea huko, nilichogundua biashara sio kwa ajili ya Kila mtu huko competition+uchawi ni mkubwa.

Mtaji wa kilimo kianzio kama million 5 upo, nataka nilime kwa kutegemea umwagiliaji na mbolea maana bongo hapa ulisema utegemee mvua ni kubahatisha tu, unaweza teketeza hata million 10 hivi hivi.

Niko Mwanza kwa Sasa, je mkoa gani Unafaa kwa kilimo Cha umwagiliaji? Nilifikiria niende SINGIDA nikalime vitunguu Lakini pote huko ni pakame sidhani kama Kuna bonde la maji.

Natanguliza shukrani.
 
Kilimo cha umwagiliaji kinahitaji usimamizi sana wa karibu nina uzoefu nayo wa mda mrefu na inalipa.maeneo yapo mengi cha muhimu masoko na ulipo na unafanyia wapi na ww unafanya nn
Funguka zaidi mkuu, singida,babati au kondoa (dodoma inawezekana?)..maana nipo karibu zaidi na Maeneo hayo
 
Dodoma inawezekana maeneo kama Hombolo, Mpwapwa Kuna bonde moja hivi watu wanalima sana Mahindi na kilimo Cha horticulture, Kondoa vijijini kuanzia Kolo mpaka kule Galapo wenyewe wanapaita mbugani unapanda mpaka babati kuna watu wanalima kilimo Cha umwagiliaji wanamiliki visima vyao.

Moshi wilaya ya Moshi vijijini maeneo kama ya Chekereni, Kahe, Mwanga kule Kuna mifereji ya maji yanatiririka tu watu wanalima sana Nyanya, hoho na Vitunguu.

Sina uzoefu sana ila nina interest na mambo hayo pia, tuendelee kuangalia kwa wajuvi wengine wa mambo.
 
Asante sana ndugu.
 
Kama unataka Mali basi utaipata shambani, Mimi nimeamua kuunga juhudi nikashinde na kuteketea shambani huko labda tutatokea huko, nilichogundua biashara sio kwa ajili ya Kila mtu huko competition+uchawi ni mkubwa.

Mtaji wa kilimo kianzio kama million 5 upo, nataka nilime kwa kutegemea umwagiliaji na mbolea maana bongo hapa ulisema utegemee mvua ni kubahatisha tu, unaweza teketeza hata million 10 hivi hivi.

Niko Mwanza kwa Sasa, je mkoa gani Unafaa kwa kilimo Cha umwagiliaji? Nilifikiria niende SINGIDA nikalime vitunguu Lakini pote huko ni pakame sidhani kama Kuna bonde la maji.

Natanguliza shukrani.
Sikumbuki jina la kijiji, lakini ni maeneo ya Sengerema jirani na Ziwa Victoria. Miaka ya nyuma, kulikuwa na mtu alikuwa anafanya kilimo cha tikiti maji pande hizo. Labda ungejaribu kufuatilia na huko pia
 
Kikubwa maji yawepo mkuu na mazao yanayo kula maji ya kutosha yanakuwa super sokoni.
Nilienda kwa ndugu yangu mmoja mlandizi nilikuta kaendelea sana hadi gari analo na stock ipo ya mpunga wa kutosha almost gunia 100 na ushee

Toka ameanza irrigation system mafanikio yapo kikubwa ni kuwa karbu tu.

Uliza pia na morogoro mana sijafika huko kuhus kulima mpunga kwa umwagiliaji.
 
Tabora-Igunga,,Mwanzugi panakilimo Cha mpunga na maji ya uhakika,sijawahi fika kwenye mradi huo isipokua Afisa kilimo wa wilaya ya Iramba ananihadithiaga sijamtilia maanani.
 
Back
Top Bottom