Ni mbinu gani ambazo Ethiopia inatumia kukuza pato lake la Taifa (GDP -155), na kwa nini inaonekana kuwa na mafanikio? Je, ni kwa nini tusiwaige?

covid 19

JF-Expert Member
May 9, 2014
4,904
10,699
Napenda kufahamu ethiopia wanategemea kitu gani kwenye kukuza uchumi wao pia ni sector gani kwao inayoongoza kuwaingizia pesa nyingi.

Swali kwa wachumi ni mbinu gani ambazo Ethiopia inatumia kukuza pato lake la Taifa (GDP) hadi wanaenda speed sana yaani miaka kama 3 au minne nyuma tulikuwa hatupo mbali nao ghafla sasa hivi wamepaa sana to 155.804, wakati sisi tumebaki kwenye 85.00 ni kwa nini inaonekana kuwa na mafanikio?

Je, ni kwa nini nchi zingine, kama vile yetu tanzania , tusiige njia hizo? maana sisi tunapanda taratibu!
 
napenda kufahamu ethiopia wanategemea kitu gani kwenye kukuza uchumi wao pia ni sector gani kwao inayoongoza kuwaingizia pesa nyingi

swali kwa wachumi ni mbinu gani ambazo Ethiopia inatumia kukuza pato lake la Taifa (GDP) hadi wanaenda speed sana yaani miaka kama 3 au minne nyuma tulikuwa hatupo mbali nao ghafla sahivi wamepaa sana to 155.804, wakati sisi tumebaki kwenye 85.00 ni kwa nini inaonekana kuwa na mafanikio? Je, ni kwa nini nchi zingine, kama vile yetu tanzania , tusiige njia hizo? maana sisi tunapanda taratibu!

Ndiyo wale raia wao kila leo kufa kwenye ma container safarini sauzi kwa njia za panya?
 
napenda kufahamu ethiopia wanategemea kitu gani kwenye kukuza uchumi wao pia ni sector gani kwao inayoongoza kuwaingizia pesa nyingi

swali kwa wachumi ni mbinu gani ambazo Ethiopia inatumia kukuza pato lake la Taifa (GDP) hadi wanaenda speed sana yaani miaka kama 3 au minne nyuma tulikuwa hatupo mbali nao ghafla sahivi wamepaa sana to 155.804, wakati sisi tumebaki kwenye 85.00 ni kwa nini inaonekana kuwa na mafanikio? Je, ni kwa nini nchi zingine, kama vile yetu tanzania , tusiige njia hizo? maana sisi tunapanda taratibu!
Wasingekuwa na shida za kiusalama wangefika mbali ila Sasa ni unstable county kama Nigeria.

Watu wengi lakini zero security huko countryside ndio maana wanakimbia Nchi Kila siku.
 
Hata sisi tusikate tamaa. Hawa jamaa walipigwa na njaa mpaka wanamuziki wakubwa duniani wakajumuika kukusanya pesa ya chakula. Leo, mashallah mambo sio mabaya.
Lakini pia, Ethiopia ni nchi ya kustaajabisha sana. Imepiga maendele makubwa kiuchumi, ingawa wananchi wengi, haswa vijijini, bado maskini. Pia, ni nchi ambayo haina Amani ya kudumu, kila siku wanapigana 《Tigray vs Oromo》.Ukija kwenye hali ya hewa ndio usiseme. Ukame kila mara. Internat yao ni ya kuunganisha na gundi, akini uchumi wao unaendele kukua.

Upande mwingine, Ethiopia Wana Diaspora kubwa sana, haswa kule US (takribani Ethiopians 400, 000 wanaishi huko) Pengine hii inasaidia kwenye remittance inayorudishwa, Sina uhakika. Maana Hawa jamaa ni ma- entrepreneurs by nature. Kila walipo lazima wafungue biashara.
 
Ifike wakati tuache kuambiwa uchumi wa kwenye makaratasi..., Nadhani wewe hauhitaji kuambiwa kwamba upo vizuri ni wewe mwenyewe utajua.... Ni Wahabeshi wangapi wanashikwa wakikimbia nchini kwao kwenda pastures new kutafuta maisha... ?

Point yangu tusiige mtu bali tutengeneze maisha ambayo ni inclusive..., huwezi kuangalia Uchumi Pekee bila kuangalia Social na Environmental Factors pia..., vilevile uchumi huo uwe inclusive wenye majority ya middle income wanaoweza kujitapati basic needs (kujipatia na sio kupewa kama sadaka)
 
hapo ndio shida sasa

Siyo shida bali ni wizi wa serikali Kwa watu. Hao ni kama sisi tu. Kumbuka hata kwetu na matatizo ya corona au umeme Kodi Kwa serikali zinapanda bila kujali walipa Kodi biashara zao zinakufa au la.

Serikali dhalimu hunyang'anya watu wake mali bila kujali.
 
Back
Top Bottom