Ni mafuriko, Tabora yazizima

[h=2]Mgombea mwenza kupitia CCM, Samia amezidi kuiteka Tabora, maelfu kwa maelfu wajitokeza kumpokea mkoani Tabora.Mama Samia ameahidi serikali yake itajitahidi kuhakikisha wanatoa fursa kwa vijana kupata mikopo na kuweza kujiajiri. Serikali itaboresha miundo mbinu hususani huduma za afya na barabara.[/h]



Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni uliofayika leo kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Uyui katika jimbo la Tabora mjini.
Maelfu ya wananchi wakimshangilia mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Uyui, jimbo la Tabora mjini mkoani Tabora
Aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Nkenge lakini akashindwa katika kura za maoni, Mama Asupta Mshama, akihutubia maelfu ya wananchi katika viwanja vya Shule ya Sekondari Uyui, Jimbo la Tabora mjini mkoani Tabora
Mbunge wa jimbo la Tabora Mjini Emmanuel Mwakasaka akiomba kura katika mkutano wa kampeni wa Mama Samia, uliofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Uyui, katika jimbo hilo mkoani Tabora leo

sishangai Tabora kwani hata maendeleo yao yanaonekana ccm wameichagua wenyewe mbele kwa mbele
 
watu walienda kushangaa ndio maana alipouliza wangapi watampa pombe kula wakanyanyua mikono watu saba tu.
 
Mmmmh hata hamna mafuriko Tabora ninayoijua hapo kulikuwa hamna watu zaidi ya wanafunzi na washangaa wasanii tu
 
Acha ulingo weye...sijui hao watu kwanza mlipowatoa ni wapi. kwanza utadhani hata hakuwepo. pamoja na kuja na hao wasanii ambao sasa hivi kwa sababu ya matendo wanaitwa mobile big brother
 
mbona mmeukimbia uwanja aliifanyia mkutano Lowasa? mnampeleka mama wa watu kwenye uwanja wa mpira mita miamoja halaf mnasema mafuriko
 
Back
Top Bottom