Ni lini Watanzania hasa vijana tutaacha tabia ya kusifia viongozi ili kupata teuzi?

BALOTEL

JF-Expert Member
Jan 8, 2013
596
670
Habarini ndugu zangu wa Tanzania.

Naomba nikiri kwanza kabisa mimi sio mwandishi mzuri hivyo kama nitakua nimeenda tofauti kidogo nipo tayari kurekebishwa.

Mimi sio mwanasiasa na wala sio mwanachama wa chama chochote kile ila ni mtanzania mpenda maendeleo, naomba nitambulike hivyo.

Nimekua nikitazama mambo mengi yanayoendelea katika majukwaa yetu ya kisiasa na shughuli mbalimbali na hata humu jamii forum. Kuna jambo moja naliona kama linapata kukua kwa kasi sana katika kizazi hiki cha sasa, swala la vijana kuwa ni watu wa kusifu tu na kujifanya watiifu kwa wanasiasa wenye nyadhifa au ambao wanaonekana kwenda kupata nyadhifa.

Najiuliza hasa mara nyingi hivi ni kweli taifa letu limekua na vijana wanaojua tu kusifia sifia kinafiki hawa viongozi wetu na hakuna namna nyingine ya kuweza kuonekana na kupata hizi teuzi au ndio mfumo tuliochagua kwenda nao ili tuangamie baadae?

Kuna hatari siku moja tutapata kiongozi mkubwa asiyekuwa mzalendo na raia wa nchi hii hasa kwa staili hii ambayo tunaenda nayo.

Kuna wakati vijana waliamua kujitoa kabisa ufahamu na utu na kuamua kuwa wakatili kwa watanzania wenzao ili tu kupata vyeo.

Sitaki kuweka majina hadharani lakini kama kumbukumbu zitawaelekeza vizuri mtakumbuka wakuu wa wilaya na mikoa baadhi walivyopatikana na namna walivyoendeleza aina yao ya uongozi.

Sitaki kuamini kama vyama hivi vimekosa kabisa namna ya kuwapa elimu ya uongozi vijana wanaotarajiwa kuja kuwa viongozi siku za usoni mpaka vijana wanaamua kuwa tu watu wa kusifia na kujipendekeza ili kuonekana.

Niwaombe wenye mamlaka za uteuzi tafadhalini sana kabla ya kudanganywa na hawa vijana wa kusifu na kuomba hembu tuangalie sifa nyingine mbadala za kuwa kiongozi.

Na sisi vijana hembu tujifunze kuwa wazalendo na wakweli ,tuhoji kwa adabu na nidhamu pale panapohitajika kufanya hivyo, tuache hii tabia ya kusifu kupitiliza tunalimaliza taifa letu wenyewe.

Asalam alekhum

Saanane Jr.
 
Back
Top Bottom