Ni lini ukarabati na ujenzi wa viwanja vya kisasa vya mpira utaanza chini ya Serikali hii?

Magufuli 05

JF-Expert Member
May 7, 2023
943
1,989
Ndugu Watanzania, umekuwa ni wimbo usiokuwa na mwisho,kila siku ni maneno tu,"tutakarabati,tutajenga uwanja Dodoma wa KISASA " lakini wapi.

Wimbo huu toka mwaka 2020 Hadi sasa unaimbwa tu. Watanzania wamegeuzwa wajinga,wanabebeshwa mabango kwenye mechi za Yanga na Simba eti anaupiga mwingi, wapiii!

Masikini Watanzania wanapenda mpira hasa ligi ya ndani lakini wanaangushwa na viongozi wao.
Timu zetu zinajitahidi kuitangaza nchi kwenye maeneo mengi,mfano kutokomeza magonjwa,unyanyasaji, kutangaza utalii,lakini wapii!

Watanzania wanadanganywa na eti goli la!

Nchi hii njaa inaliangamiza taifa, uzalendo ni bidhaa adimu Sana (kwa sauti ya Mh. Tabasamu)
Hivi ni nini kinashindikana nasi tukawa na VIWANJA vizuri?

Masikini kila mkoa utakuta uwanja wa CCM tu. Umetelekezwa,halafu hapo ndiyo ligi kuu inachezwa,mechi inaonyeshwa mbashara, daaa! Nchi yangu Tanzania,nani katuroga na huku tunakila kitu?

Shida ni pesa? Au ni akili za wenye dhamana?wadau wanajitahidi Sana kina Bakhresa, kuwekeza katika soka letu, kina fountain gate, kina MO na GSM,lakini tumekosa commitment ya serikali.

Imekuwa inavizia tu wakisikia fountain gate wamechukua kombe hao kwenye mapokezi na kuwapeleka Bungeni, Yanga kaingia nusu final hao visit Tanzania.

Michezo inakuza na kutangaza siasa za ndani, lakini kwetu michezo inatumikia siasa na siasa inafaidika kupitia michezo hakuna win win situation.

Inasikitisha Sana,mwisho kabisa, Watanzania,msikubali kutumika kuwajengea watu umaarufu hewa, bali kazi yao inayoonekna kwa macho ndiyo itawapa umaarufu.

Usibebeshwe bango kwenye uwanja wa mpira kumtangaza mwanasiasa, mwache afanye kazi sisi tutaiona na kamwe hatutamsahau kwa kazi hiyo.

Mkapa alijenga uwanja tutamkumbuka na kumuenzi kwa hilo
Ahsanten
 
Back
Top Bottom