Ni kweli Waafrika hatukuwa na Historia kabla ya ujio wa Wazungu?

Historia tunayoisoma na kuifahamu kwa sasa imepotoshwa sana, kuna uwezekano mkubwa tu kuwa waafrika katika wakati fulani walikuwa superior kuliko hao wengine.

Historia haidanganyi kaka u superior ktk lipi?

Kama ndivyo why tulibaki nyuma kiteknolojia?
 
Historia yetu imefunikwa sana na hawa waliokuja kututawala, wamebadilisha mambo mengi ili tujione tu wanyonge.

Nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani, lakini suala la historia ya mwafrika liko pale pale, wao wazungu ndio waliokuja na CREATION THEORY kuwa binadamu wote tumetokana na adam na Eva, bado wakaenda mbali zaidi kusema sisi Wafrika na kizazi ambacho tulipewa laana na Nuhu, kuwa sie ni kizazi cha NUHU kwa hiyo ndio tulimchungulia Nuhu alipolala uchi na kumcheka, hivo akatupa laana. maswali ya kujiuliza katika hili, mbona hawa watu walikuwa wakiingiliana wao kwa wao ili kuongeza kizazi, hii sio laana?????? wakaa wakaona baadhi ya vipengele vya agano la kale vina utata, wakaja na Agano jipya, (yote yaliikwisha pale msalabani) Ukikaa ukiangalia vizuri utaona kuwa biblia inavipengele vingi vya kumtukuza mkubwa(boss) na kumfanya slaves kuwa wakunyenyekea tu. utakumbuka kuwa kipindi cha industrial revolution ndio kipindi ambacho biblia ilichukua nafasi kubwa ili kuwafanya watumwa wawe watulivu, biblia is just a myths.

Hawa hawa wazungu ndio waliokuja na theory ya ORGANIC EVOLUTION wao waliamini Human beings like any other organisms are subjected to a series of gradual changes in their genetic and physical constitution. sasa basi kwa hii mitazamo miwili iliyopingana ilifanya wazungu kitu cha kwanza walipokuja ni kutubadilisha imani, wao wanasema wametustarabisha, kitendo cha kutubadili imani, mtazamo, fikra kikatufanya sisi tuamini wao ni watu wa ajabu, wanafanana na mungu, wamekuja wakaua locai industries zetu na kila kitu chetu ili iwe rahisi sisi kutumia vyao. hapo ndio afrika tulipo anguka na kutokuwa na maendeleo hadi sasa, maana tulikubali kutawaliwa na kuwatumikia tukasahau kabisa yetu, ndio hadi leo tumebaki kuwa dumpo la bidhaa zao tena za hali ya chini, tunaishi kwa masharti yao nk.

cc. HOW EUROPE UNDERDEVELOP AFRICA. by Walter Rodney
 
Lugha ni ushahidi kwamba tulikuwa na maisha yetu kitambo.

Fuatilia maneno kwenye lugha za asili.
Zipo namba
yapo maneno yanayoashiria dini, hapa hakuna Allah wala Yeshua.
Zipo ngazi za kiutawala wa jamii
Yapo maneno yanayoelezea matukio maalum

Hayo maneno yanaashiria uwepo wa wa vitu na shughuli hizo. Jamii hii ilikuwepo na utaratibu na shughuli zake.

Kama iliwahi tokea ukawepo muingiliano huo kabla, lugha zingekuwa na hifadhi ya mawasiliano wakati wa muingiliano huo. Ninafikiri kama wachambuzi wa jamii, wakifuatilia kwenye lugha zetu za asili tunaweza kupata jibu.

Neno tarakishi, halikuwepo kabla ya uwepo wa kifaa hiki. Maneno hayo yanaweza yakawa yamepungua kama ni kipindi kirefu tangu mahusiano hayo yajitokeze ila uwezekano wa kupotea kabisa ni mdogo. Bahati mbaya hatukuwa na maandishi.
 
Mkuu ngoja nijaribu kukushawishi then twende pamoja.
  • Kwanza sielewi unyonge unaouzungumzia ni upi?
  • pili maendeleo ya namna gani?
back to topic:
Ushahidi wa kihistoria unaothibitisha kuwa mwafrika hakuwa mnyonge ni kuwa kwanza uelewe mwafrika alikua na mila, desturi na utamaduni wake ambao ndio ulimuongoza kwa wakati huo, sio kwamba mwafrika alikuwa stasic hapana ila tunajua kwamba jamii za afrika zilikuwa zikihama toka stage moja kwenda kwenda nyingine kimaendeleo, kwakua mwafrika alikuwa akijishisha na hunting and gathering. through this activities they obtain food. The basic tools used by early man were made from wood, bones and stones,they easily obtained from their natural surrounding, from this resources they were able to make arrows, bows used during their hunting and gathering processes.

Ifahamike kwamba hunting and gathering societies commenced since the biggining of human kind and we know Africa is the birthplace of humanity and the only continent that has evidence of the early evolution of humans. rejea: Olduvai Gorge, Laetoli,Lake Turkana, Hadar and Omo valley, etc.

sasa basi maisha ya huyu mwafrika kwa ujumla wake yalikuwa ni historia, tunaona namna jamii za wakati huo zilikuwa zikiishi kwa kuhamahama, lakini pia walivaa magome ya miti, walizungumza kwa ishara, na maisha yao yalitegemea kuwinda na kuokota matunda pori hii peke yake ni ushahidi wa kihistoria, tunaona hadi sasa zipo jamii ambazo zinaishi ivo kama Hadzabe, Tindiga, Sandawe, Bumbuti, Pygmies, Khoisan and Ju'/hoans people.

Lakini linapo kuja suala la maendeleo .
Maendeleo ni kitendo cha kutoka hatua moja kwenda nyingine, kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa, nk.
Tukirudi Afrika tunaona kuwa katika kipindi kile:
  • mwafrika kwanza alikuwa akitumia simple tools katika shughuli zake, pia aliweza kugundua chuma (Neolithic revolution) hii ilimsadia kuweza kufanya kazi kwa urahisi.
  • Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi jamii nyingi zilibadili mfumo wa maisha, mfano Tindiga, sandawe, hadzabe walianza kufuga pia
  • Pia jamii hizi zilikuwa na mifumo ya kiutawala(political organization) hii ilitokana na kuongezeka kwa watu hali iliyopelekea formation of state.
  • Jamii hizi ziliachana na kuwasiliana kwa ishara na kuanza kuzungumza kwa sauti, hii ilitokana na muingiliano na ushirikiano baina ya jamii moja na nyingine, but within Africa.

Sasa basi ni ukweli usio pingika kuwa mwafrika alikuwa na historia yake na alidevelop over time and space, Alikuwa na local industries(handcraft industries), tulikuwa na Iron smelting, Salt making etc, lakini vitu vyote hivi alikuja kuviua mzungu.
Historia ya mwafrika iliharibiwa na mzungu hasa baada ya Charles Darwin (1809-1882) na Alfred Russell Walless kuja na theory ya ORGANIC EVOLUTION hii iliwapa shida sana white people kukubali kwamba binadamu wa kwanza alitokea afrika, theory hii iliwakara sana kwanza kwa kuona inapingana na biblia kuwa binadam hakuumbwa ila alitokea Afrika in form of ape, kutokana na ubaguzi wa rangi na kuona wao ni kila kitu hapo ndio walipokazana kueneza CREATION THEORY na kumuweka mwafrika kuwa kiumbe duni.

Nimejaribu.
cc: Yericko Nyerere, mtzmweusi, hoshea, Ubwabwaz and other historians.

Upo vizuri, waje hao wa dini watuletee ushahidi wao
 
Historia haidanganyi kaka u superior ktk lipi?

Kama ndivyo why tulibaki nyuma kiteknolojia?

Mkuu unatambua kuwa 90% ya Wazungu ni Majini?

Soma makalahii, hapa chini niliyowahi kuiandika siku nyingi kidogo,

Kwakutumia historia ya binadamu kibiblia, ukichambua kila uzao na sambuli zake unaweza kubainisha wazi hilo nilisemalo, japo laweza kuwa zito kwa wengine.

Kwa wale muaminio biblia mnaweza kukubaliana na mimi kuwa sababu kuu ya Mungu kuiangamiza dunia enzi za Nuhu, ni kutokana na wanadamu kumuasi mungu, maasi yalikuwa yakufuru hasa yakihusisha mwingiliano wa majini na binadamu, wanyama na binadamu nk na baada ya angamizo hilo, manusura walikuwa ni Nuhu, wanawe, mke wake, na kila kiume kibaya na chema aliviokoa mke na mme. Mwanzo 7:1-11

Hapa tunaona kuwa na majini yaliokolewa na Nuhu, Sasa tukirejea katika masimulizi yetu tunaona sasa baada ya Nuhu kuokolewa na safina, wanae watatu wakiume ambao tayari walikuwa wameoa (enzi za gharika) mmoja wao Yafethi alikuwa kaoa jini, wakati wawili Shemu na Hamu wao biblia inasema walioa mahali ambapo si chukizo mbele za Mungu. Mwanzo 10:1-7

Uzao wa wana wa Nuhu ndio unatupatia ukweli wa nikisemacho, kwanza tunaona kuwa wana wa Yafethi alieoa jini ni, Gomeri (Ujerumani), Magogu (Cambridge UK ), Madai (Hispania), Yavana (Italia), Tubali au Yunani (Ugiriki), Mesheki (Lebano) na Tirasi (Ufaransa), Mpaka hapotumeona uzao wenye ushirika na majini wa Yafethi

Sasa tuangalie uzao Hamu unaotajwa kuwa Mungu aliupenda na kuupa baraka tele, uzao huo ni Kushi (Ethiopia), Misri (Misri), Kanaani (Israel) na Putu (Libya)

Mwanzo 10:21-23 Tunasoma yakuwa wana wa Shemu ambe ni sehemu ya kipenzi cha Mungu, ni Elamu (Saudi Arabia), Ashuru (Syria), Arfaksadi (Kuweit), Ludi (Jordan), na Aramu (Qatar)

Mpaka hapo tumepata mwangaza kuwa uzao wa Yafethi wenye tokezo la majini/uovu ndio uzao wa mataifa karibu yote ya Ulaya. nauzao wa Hamu na Shamu ndio uzao uliopewa neema na muumba hii ni kwamujibu wa maandiko ya kiroho.

Kwamaandiko hayo tunaamini kabisa kuwa Mashariki ya kati, na Afrika ndio maeneo muhimu ambayo mungu aliwabarikia watu wake.

Hata ukitumia Kuruani takatifu hayo yote yanabainisha wazi kabisa.

Kwamsaada zaidi rejea Mwanzo 4:16-24, Ufunuo 16:13-15, Ufunuo 20:7-8, Ezekieli 27:12-14, Ezekiel 38:1-9

Kwakupanua wigo wa mjadala nje ya biblia hasa wale wenzangu waaminio Freemasonry ijapokuwa watetezi wake hupinga kuwa si ushetani/ujini, watambue kuwa uzao wa asili wa freemasonry ni Magogu (Cambridge UK) japo katika historia inasema ni Scotland UK

Haya ndugu zangu nawakaribisha katika tafakuri njema
 
Ni kama vile fumbo la imani, kwa wale waamini wa kristu wataungana na mimi kuwa habari za Mungu na uumbwaji wa dunia zilikuja kuandikwa na Musa, na Musa aliziandika kama vile aliziishi ijapokuwa karma ya kiroho inasema Musa alikuwa mbeba kizazi yani kizazi cha Musa kikaishi miaka 2000, Kikaja kizazi cha Eliya Mtishibi nacho kikaishi miaka 2000, Kikaja kizazi cha Yesu nacho kimeishi miaka 2000, sasa kwamjibu wa karma ya kiroho nikuwa Mungu mwenyewe ameshuka kukiongoza kizazi hiki tunacho ishi mimi na wewe,

Vivyo hivyo kwa upande wa binadamu wa kiafrika habari zake na uumbwaji wake zimekuwa zikitoka kwa binadamu weupe wazungu, kanakwamba wao waliyaishi maisha ya mwafrika huyu.

Je, nikweli kwamba, hapo zamani za kale Waafrika hatukuwa na Historia; na kwamba Historia yetu ilianzia baada ya kuja kwa Watu Weupe wazungu

Na iwapo suala hili jawabu lake ni hapana, kuna uthibitisho wowote wa Kihistoria unaothibitisha kwamba, kuna wakati ambao Mwafrika hakuwa Mnyonge na kwamba aliwahi kuwa juu kimaendeleo dhidi ya Watu wa Jamii nyingine Duniani.?

Acha bla bla bla We tapeli mlipe bwana Oluoch
 
Last edited by a moderator:
Ukweli nikwamba hata mafarao wa misiri walikuwa wa afrika kama wewe kwahiyo tulisha wahi kuitawala dunia pia wala sio kuwa na hisitoria tuu bali kuw nahitoria kubwa kabisaa.
 
ukizungumza historia yavmwafrika

anza kumtafta nimrode
na uzao wa nuhu utakutana na watoto watatu

na mwafrika alikuwa akiitwa kushi
na huyo ndo alianza kutawala kwa mwanae nimtode na ndo alikuwa tajiri kuliko woote

nenda pia kasome historia ya misri ni dola la kwanza kuwa kubwa kabla ya rumi na ukatidayo

pia pitia habari za Ethiopia utagundua kulikuwa na malkia wa Ethiopia ambaye alienda kwa Suleiman

hiyo inamaana afrika tulikuwa superior mapema kuliko wazungu

na kwa kukazia number system ilitoka misri
 
Historia imeweza kuendelezwa na ufahamu wa kusoma na kuandika. Waingereza hawana historia kabla ya kutawaliwa na Warumi, na katika utawala wa warumi historia inaonyesha maisha yao walivyowatawala Waingereza kwasababu Warumi walijua kusoma na kuandika muda mrefu. Babu zetu wangetuachia urithi mzuri wa historia kama wangeweza kuiandika.

Una elimu ndogo ama una akili ndogo? Huwezi hata kujisogeza mbele kidogo kiudadisi hata kile ulichojaribu kukielewa? Kwanza Warumi wepi unao ongelea? hukuwai kujiuliza hao warumi maarifa wametoa wapi?
 
Historia imeweza kuendelezwa na ufahamu wa kusoma na kuandika. Waingereza hawana historia kabla ya kutawaliwa na Warumi, na katika utawala wa warumi historia inaonyesha maisha yao walivyowatawala Waingereza kwasababu Warumi walijua kusoma na kuandika muda mrefu. Babu zetu wangetuachia urithi mzuri wa historia kama wangeweza kuiandika.

Kwa taarifa yako maarifa ya warumi yalitokana na wagiriki. na wagiriki walielimishwa na babu zetu pale misri, Kush na unubia (Soudan).So kifupi maarifa na ustaarabu ulianza Afrika ukasambaa. watu walikuwa wanakuja Afrika kuja kusoma kama siku hizi watu wanavyoenda Ulays na Marekani kusoma.
 
Mkuu ngoja nijaribu kukushawishi then twende pamoja.
  • Kwanza sielewi unyonge unaouzungumzia ni upi?
  • pili maendeleo ya namna gani?
back to topic:
Ushahidi wa kihistoria unaothibitisha kuwa mwafrika hakuwa mnyonge ni kuwa kwanza uelewe mwafrika alikua na mila, desturi na utamaduni wake ambao ndio ulimuongoza kwa wakati huo, sio kwamba mwafrika alikuwa stasic hapana ila tunajua kwamba jamii za afrika zilikuwa zikihama toka stage moja kwenda kwenda nyingine kimaendeleo, kwakua mwafrika alikuwa akijishisha na hunting and gathering. through this activities they obtain food. The basic tools used by early man were made from wood, bones and stones,they easily obtained from their natural surrounding, from this resources they were able to make arrows, bows used during their hunting and gathering processes.

Ifahamike kwamba hunting and gathering societies commenced since the biggining of human kind and we know Africa is the birthplace of humanity and the only continent that has evidence of the early evolution of humans. rejea: Olduvai Gorge, Laetoli,Lake Turkana, Hadar and Omo valley, etc.

sasa basi maisha ya huyu mwafrika kwa ujumla wake yalikuwa ni historia, tunaona namna jamii za wakati huo zilikuwa zikiishi kwa kuhamahama, lakini pia walivaa magome ya miti, walizungumza kwa ishara, na maisha yao yalitegemea kuwinda na kuokota matunda pori hii peke yake ni ushahidi wa kihistoria, tunaona hadi sasa zipo jamii ambazo zinaishi ivo kama Hadzabe, Tindiga, Sandawe, Bumbuti, Pygmies, Khoisan and Ju'/hoans people.

Lakini linapo kuja suala la maendeleo .
Maendeleo ni kitendo cha kutoka hatua moja kwenda nyingine, kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa, nk.
Tukirudi Afrika tunaona kuwa katika kipindi kile:
  • mwafrika kwanza alikuwa akitumia simple tools katika shughuli zake, pia aliweza kugundua chuma (Neolithic revolution) hii ilimsadia kuweza kufanya kazi kwa urahisi.
  • Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi jamii nyingi zilibadili mfumo wa maisha, mfano Tindiga, sandawe, hadzabe walianza kufuga pia
  • Pia jamii hizi zilikuwa na mifumo ya kiutawala(political organization) hii ilitokana na kuongezeka kwa watu hali iliyopelekea formation of state.
  • Jamii hizi ziliachana na kuwasiliana kwa ishara na kuanza kuzungumza kwa sauti, hii ilitokana na muingiliano na ushirikiano baina ya jamii moja na nyingine, but within Africa.

Sasa basi ni ukweli usio pingika kuwa mwafrika alikuwa na historia yake na alidevelop over time and space, Alikuwa na local industries(handcraft industries), tulikuwa na Iron smelting, Salt making etc, lakini vitu vyote hivi alikuja kuviua mzungu.
Historia ya mwafrika iliharibiwa na mzungu hasa baada ya Charles Darwin (1809-1882) na Alfred Russell Walless kuja na theory ya ORGANIC EVOLUTION hii iliwapa shida sana white people kukubali kwamba binadamu wa kwanza alitokea afrika, theory hii iliwakara sana kwanza kwa kuona inapingana na biblia kuwa binadam hakuumbwa ila alitokea Afrika in form of ape, kutokana na ubaguzi wa rangi na kuona wao ni kila kitu hapo ndio walipokazana kueneza CREATION THEORY na kumuweka mwafrika kuwa kiumbe duni.

Nimejaribu.
cc: Yericko Nyerere, mtzmweusi, hoshea, Ubwabwaz and other historians.
safiii
 
Sam97,
Hakuna binadamu asiyekuwa na historia yake halikadhalika hakuna
watu kwa maana yoyote ile iwe kundi au taifa wasiokuwa na historia.

Hii dhana ya kuwa labda, ''hapakuwa na historia,'' chanzo chake ni
wale wasiopenda historia ya watu wengine ifahamike kwa sababu zao.

Hili tumelizungumza sana hapa jamvini.
 
Kuna mtu aliitwa Nimrod kitika Ukaridayo ya kale leo hii Iraq, huyu alikuwa mweusi na ndio aliitawala dunia na ndie aliongoza katika kipindi cha ujenzi wa mnara wa babel. Naweza kushawishika kuungana na wewe mkuu
Kama Nimrod alikuwa mweusi basi inawezekana kuwa kijakazi wake ambaye ni Terah alikuwa pia mweusi hivyo basi Abrahamu pia alikuwa mtu mweusi.
 
Historia tunayoisoma na kuifahamu kwa sasa imepotoshwa sana, kuna uwezekano mkubwa tu kuwa waafrika katika wakati fulani walikuwa superior kuliko hao wengine.
Kweli kabisa mkuu, migratory paterns za watu weusi zinadhihirisha tulitoka nchi za kaskazini mwa africa(Egypt) au kwa jina la kitambo Kemet kuhepa vita.
 
Bwana Yericko umenigusa sana na leo nimeamua kufunguka na ninaomba Mungu sana Mh Waziri wa elimu na taasisi ya ukuzaji mitaala Tanzania isome hii comment yangu! au kama kuna mwanajamvi anaweza kuwafikishia ujumbe huu nitashukuru sana, ni hivi, mimi ni mwalimu ( nina diploma ya ualimu na nimefundisha somo la historia kwa shule kadhaa za sekondari O and A level kwa miaka kadhaa na nina BA ya Mlimani na Masters ya Social Welfare ya ulaya! na ninaishi ulaya miaka kadhaa now! iko hivi huku ulaya hawasomi kuhusu historia ya Afrika kwenye level za chini ni hadi ufike University ndo unaanza kusoma habari za Afrika! kuna wazee wa kizungu ukiwaambia unatoka Tanzania wanakuuliza hiyo nchi iko wapi! ninapenda sana kuanzisha mjadala wa kufuta Topics mbili za somo la historia kwa shule za msingi na za sekondari! ninapendekeza Topics za Slave Trade na Colonialism zifutwe kwenye mtaala wa shule za msingi na sekondari Tanzania. Hizi topics ni miongoni mwa topics zinazoendeleza unyonge wa Mwafrika na kufuta historia ya Afrika , mila na desturi zetu! hizi topics zinamfanya mtoto mdogo kukua akijua wazungu na waarabu ni bora kuliko waafrika na kumfanya kutamani kila kitu cha ulaya! hizi topics zinashusha thamani ya mwafrika na kumfanya kuabudu ulaya! ni topics zinazobeba sehemu kubwa ya somo la historia na kupoteza ufundishwaji wa historia yetu kama nchi na makabila yetu na sayansi yetu na civilization ya mwafrika! ukweli ni kuwa kuna wazungu omba omba huku ulaya wengi tu, na wanaomba kila mtu anaepita njia hata mwafrika! ukweli wakati umefika sasa tunahitaji kuwafundisha watoto wadogo mashuleni mila na desturi zetu na hayo ya slave trade na colonialism wakasome University wakiwa matured! ni hayo tu! naomba kuwasilisha!
Nashukuru sana mkuu, ujumbe wako umefika
 
Back
Top Bottom