Ni kweli Waafrika hatukuwa na Historia kabla ya ujio wa Wazungu?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Ni kama vile fumbo la imani, kwa wale waamini wa kristu wataungana na mimi kuwa habari za Mungu na uumbwaji wa dunia zilikuja kuandikwa na Musa, na Musa aliziandika kama vile aliziishi ijapokuwa karma ya kiroho inasema Musa alikuwa mbeba kizazi yani kizazi cha Musa kikaishi miaka 2000, Kikaja kizazi cha Eliya Mtishibi nacho kikaishi miaka 2000, Kikaja kizazi cha Yesu nacho kimeishi miaka 2000, sasa kwamjibu wa karma ya kiroho nikuwa Mungu mwenyewe ameshuka kukiongoza kizazi hiki tunacho ishi mimi na wewe,

Vivyo hivyo kwa upande wa binadamu wa kiafrika habari zake na uumbwaji wake zimekuwa zikitoka kwa binadamu weupe wazungu, kanakwamba wao waliyaishi maisha ya mwafrika huyu.

Je, nikweli kwamba, hapo zamani za kale Waafrika hatukuwa na Historia; na kwamba Historia yetu ilianzia baada ya kuja kwa Watu Weupe wazungu

Na iwapo suala hili jawabu lake ni hapana, kuna uthibitisho wowote wa Kihistoria unaothibitisha kwamba, kuna wakati ambao Mwafrika hakuwa Mnyonge na kwamba aliwahi kuwa juu kimaendeleo dhidi ya Watu wa Jamii nyingine Duniani.?
 
Historia imeweza kuendelezwa na ufahamu wa kusoma na kuandika. Waingereza hawana historia kabla ya kutawaliwa na Warumi, na katika utawala wa warumi historia inaonyesha maisha yao walivyowatawala Waingereza kwasababu Warumi walijua kusoma na kuandika muda mrefu. Babu zetu wangetuachia urithi mzuri wa historia kama wangeweza kuiandika.
 
Historia ilikuwepo, isipokua suala la uumbaji kwakua ni imani na imani hii ilianzia huko kwao sisi tuliipokea tu. hata ukiifuatilia kwa umakini haina ushahidi wa kutosha wa kwanini kuna tofauti ya rangi ikiwa wote ni watoto wa ADAM,
 
Kuna uthibitisho wowote wa Kihistoria unaothibitisha kwamba, kuna wakati ambao Mwafrika hakuwa Mnyonge na kwamba aliwahi kuwa juu kimaendeleo dhidi ya Watu wa Jamii nyingine Duniani.?
 
Kuna uthibitisho wowote wa Kihistoria unaothibitisha kwamba, kuna wakati ambao Mwafrika hakuwa Mnyonge na kwamba aliwahi kuwa juu kimaendeleo dhidi ya Watu wa Jamii nyingine Duniani.?

Africa haikuwa na history...

Africa had no philosophy.....
 
Ni kama vile fumbo la imani, kwa wale waamini wa kristu wataungana na mimi kuwa habari za Mungu na uumbwaji wa dunia zilikuja kuandikwa na Musa, na Musa aliziandika kama vile aliziishi ijapokuwa karma ya kiroho inasema Musa alikuwa mbeba kizazi yani kizazi cha Musa kikaishi miaka 2000, Kikaja kizazi cha Eliya Mtishibi nacho kikaishi miaka 2000, Kikaja kizazi cha Yesu nacho kimeishi miaka 2000, sasa kwamjibu wa karma ya kiroho nikuwa Mungu mwenyewe ameshuka kukiongoza kizazi,

Vivyo hivyo kwa upande wa binadamu wa kiafrika habari zake na uumbwaji wake zimekuwa zikitoka kwa binadamu weupe wazungu, kanakwamba wao waliyaishi maisha ya mwafrika huyu.

Je, nikweli kwamba, hapo zamani za kale Waafrika hatukuwa na Historia; na kwamba Historia yetu ilianzia baada ya kuja kwa Watu Weupe wazungu

Na iwapo suala hili jawabu lake ni hapana, kuna uthibitisho wowote wa Kihistoria unaothibitisha kwamba, kuna wakati ambao Mwafrika hakuwa Mnyonge na kwamba aliwahi kuwa juu kimaendeleo dhidi ya Watu wa Jamii nyingine Duniani.?

Interesting. Mi naamini tulikuwa na historia. Shida ni kwamba yawezekana watu wa wakati huo hawakuwa na utaalamu wa kuandika au vile vile zimekuwa wiped out. Kitu kimoja naamini na kila siku naendelea kukiamini, mzungu ( ambao nadhani ni waanzilishi wa kuandika kwenye vitabu etc ) anakupa kile anachotaka wewe ujue. Mfano, kama anataka kufikisha ujumbe fulani, yuko tayari ku distort kwa kutoa distorted message all the time mpaka itakapogeuka na kuwa ukweli. Huo ni mtazamo wangu....
 
mwafrika ana historia ndefu kabla ya kuja mtu mweupe, mwafrika aliweza kutumia majahazi kufika pwani za south amerika kabla hata ya columbas, tafuta documentary inaitwa hiden colors utajua greece na scotland imewahi kuwa chini ya mtu mweusi, hata jeshi la warumi wamewahi kuwa na commander wao mweusi!

Kuna mtu aliitwa Nimrod kitika Ukaridayo ya kale leo hii Iraq, huyu alikuwa mweusi na ndio aliitawala dunia na ndie aliongoza katika kipindi cha ujenzi wa mnara wa babel. Naweza kushawishika kuungana na wewe mkuu
 
Africa haikuwa na history...

Africa had no philosophy.....

Msome kwanza mdau huyu hapa chini,

mwafrika ana historia ndefu kabla ya kuja mtu mweupe, mwafrika aliweza kutumia majahazi kufika pwani za south amerika kabla hata ya columbas, tafuta documentary inaitwa hiden colors utajua greece na scotland imewahi kuwa chini ya mtu mweusi, hata jeshi la warumi wamewahi kuwa na commander wao mweusi!
 
Africa is the source of all mankind and civilization.
Elites dont want that to be known, ask youself why and do the research.
If you dont know your roots you's just a stupid sheep with no direction/ idea, doing what the master commands.
 
Kuna uthibitisho wowote wa Kihistoria unaothibitisha kwamba, kuna wakati ambao Mwafrika hakuwa Mnyonge na kwamba aliwahi kuwa juu kimaendeleo dhidi ya Watu wa Jamii nyingine Duniani.?

Mkuu ngoja nijaribu kukushawishi then twende pamoja.
  • Kwanza sielewi unyonge unaouzungumzia ni upi?
  • pili maendeleo ya namna gani?
back to topic:
Ushahidi wa kihistoria unaothibitisha kuwa mwafrika hakuwa mnyonge ni kuwa kwanza uelewe mwafrika alikua na mila, desturi na utamaduni wake ambao ndio ulimuongoza kwa wakati huo, sio kwamba mwafrika alikuwa stasic hapana ila tunajua kwamba jamii za afrika zilikuwa zikihama toka stage moja kwenda kwenda nyingine kimaendeleo, kwakua mwafrika alikuwa akijishisha na hunting and gathering. through this activities they obtain food. The basic tools used by early man were made from wood, bones and stones,they easily obtained from their natural surrounding, from this resources they were able to make arrows, bows used during their hunting and gathering processes.

Ifahamike kwamba hunting and gathering societies commenced since the biggining of human kind and we know Africa is the birthplace of humanity and the only continent that has evidence of the early evolution of humans. rejea: Olduvai Gorge, Laetoli,Lake Turkana, Hadar and Omo valley, etc.

sasa basi maisha ya huyu mwafrika kwa ujumla wake yalikuwa ni historia, tunaona namna jamii za wakati huo zilikuwa zikiishi kwa kuhamahama, lakini pia walivaa magome ya miti, walizungumza kwa ishara, na maisha yao yalitegemea kuwinda na kuokota matunda pori hii peke yake ni ushahidi wa kihistoria, tunaona hadi sasa zipo jamii ambazo zinaishi ivo kama Hadzabe, Tindiga, Sandawe, Bumbuti, Pygmies, Khoisan and Ju'/hoans people.

Lakini linapo kuja suala la maendeleo .
Maendeleo ni kitendo cha kutoka hatua moja kwenda nyingine, kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa, nk.
Tukirudi Afrika tunaona kuwa katika kipindi kile:
  • mwafrika kwanza alikuwa akitumia simple tools katika shughuli zake, pia aliweza kugundua chuma (Neolithic revolution) hii ilimsadia kuweza kufanya kazi kwa urahisi.
  • Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi jamii nyingi zilibadili mfumo wa maisha, mfano Tindiga, sandawe, hadzabe walianza kufuga pia
  • Pia jamii hizi zilikuwa na mifumo ya kiutawala(political organization) hii ilitokana na kuongezeka kwa watu hali iliyopelekea formation of state.
  • Jamii hizi ziliachana na kuwasiliana kwa ishara na kuanza kuzungumza kwa sauti, hii ilitokana na muingiliano na ushirikiano baina ya jamii moja na nyingine, but within Africa.

Sasa basi ni ukweli usio pingika kuwa mwafrika alikuwa na historia yake na alidevelop over time and space, Alikuwa na local industries(handcraft industries), tulikuwa na Iron smelting, Salt making etc, lakini vitu vyote hivi alikuja kuviua mzungu.
Historia ya mwafrika iliharibiwa na mzungu hasa baada ya Charles Darwin (1809-1882) na Alfred Russell Walless kuja na theory ya ORGANIC EVOLUTION hii iliwapa shida sana white people kukubali kwamba binadamu wa kwanza alitokea afrika, theory hii iliwakara sana kwanza kwa kuona inapingana na biblia kuwa binadam hakuumbwa ila alitokea Afrika in form of ape, kutokana na ubaguzi wa rangi na kuona wao ni kila kitu hapo ndio walipokazana kueneza CREATION THEORY na kumuweka mwafrika kuwa kiumbe duni.

Nimejaribu.
cc: Yericko Nyerere, mtzmweusi, hoshea, Ubwabwaz and other historians.
 
They've made us feel inferior because we're so superior. We've to wake up now and see the real picture folks or else we'll be forever doomed.
Tatizo la afrika in the first place was u mimi mwingi, you just imagine kulikuwa na kingdoms zaidi ya 1000 kwenye hili bara, wanapigana porana ardhi and those stuff wazungu wakaja wakashirikiana na rivals wakachukua kingdoms after kingdoms, mkwawa hakuna alomsaidia tena maadui zake wa palepale iringa waliside na wajerumani, usnitch kama huo ulifanyika maeneo kibao, that was just to illustrate utengano tulokuwa nao kabla, wakafanikiwa wakachukua matawala hadi ikawa nchi moja chini ya serikali za wakoloni. Wakaleta dini zao zikatugawa kiimani wengine wakaendekeza hiyo migawanyo ya kikabila hadi sasa inafanya kazi kama sudan kenya kidogo etc. Tz sisi ukabila umekwishaga, tatizo dogo ni hii migawanyo ya kiimani huyu anataka barikiwa na God wa Israel huyu wa Saudia wengine kwingineko. Hapa kwenye suala la dini ndipo waafrica watateseka napo after ukabila if and only if hatutoshtuka. Mungu ni wewe na roho yako mazee, hii migawanyo kuna wajinga nahisi walikaa chini wakaisuka ili warule over, u know that phrase divide and rule. That's it. So wakuu inabidi tukae chini tutulie tujievaluate sana, mambo haya si kama tulivyokuzwa tukidhani, sababu hili tatizo lisipotatuliwa africa hatutaona mwanga.
 
historia zimeanza kuandikwa baada ya kuanza kugundua maandishi ambazo ndo zimetumika kutuza kumbukumbu hivyo afrika tumekuwa nyuma katika hilo ndo maana hakuna historia lakin ukweli ni kwamba afrika ina historia yake
 
Kuna uthibitisho wowote wa Kihistoria unaothibitisha kwamba, kuna wakati ambao Mwafrika hakuwa Mnyonge na kwamba aliwahi kuwa juu kimaendeleo dhidi ya Watu wa Jamii nyingine Duniani.?
Historia tunayoisoma na kuifahamu kwa sasa imepotoshwa sana, kuna uwezekano mkubwa tu kuwa waafrika katika wakati fulani walikuwa superior kuliko hao wengine.
 
Back
Top Bottom