Ni kweli Waafrika hatukuwa na Historia kabla ya ujio wa Wazungu?

Kwamba Waafrika hatukuwa na historia yetu kabla ya ujio wa Wazungu ni uzushi mkongwe. Uzushi huu ulianza karne ya 19 na kushamiri hadi karne ya 20. Hiki lilikuwa ni kipindi cha ubepari mkongwe au ubeberu (imperialism) ambapo mabepari wa Ulaya walieneza na kuupa nguvu uvumi huu ili kuwadunisha Waafrika na kuwafanya watawalike kirahisi.

Kigezo kikubwa kilichotumika katika madai haya ni kuwa historia huhifadhiwa katika maandishi (written documents) na Waafrika hawakuwa wameandika kuhusu historia yao. Maandishi katika Africa yameletwa na mtu mweupe wakati wa ukoloni.

Ukweli ni kwamba kila jamii ina namna yake ya kuhifadhi historia na kumbukumbu nyingine muhimu. Kwa hiyo kiasi kikubwa cha historia ya Waafrika kilihifadhiwa katika masimulizi ya mdomo (oral traditions). Pia tafiti nyingi za akiolojia (archaeological studies) zimeonyesha kwamba Waafrika wanayo historia kuongea. Imethibitika pasipo shaka yoyote, kwa mfano, kwamba ajili ya binadamu ni Afrika. Imethibitika pia kuwa ni Waafrika ndio walioanza kujenga waliojenga Mawe Zimbambwe? Au kuhusu ajili ya ufaidi chumba katika Africa?
 
Upo sahihi, kwa mfano hai mimi binafsi nimesoma historia ya kabila langu lakini mwandidhi wa kitabu karibu historia yote muhimu amecopy maandishi ya wazungu wa kwanza kufika katika eneo letu ambapo maandishi hayo yamehifadhiwa kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa, hawa wazungu walikuwa wakisimuliwa na babu zetu na wao wakawa wanahifadhi kimaandishi, utata je waliandika kweli tupu? Tumeshapigwa bao na wazungu.

Cha msingi ni sisi waafrika kuipekuwa historia ya kweli ya wazungu na sivyo walivyotuandika sisi je waliwezaje kutuzidi akili?
 
Jielimishe. Hata mwanafunzi wa historia wa darasa la nne anafahamu vema
 
Ni kama vile fumbo la imani, kwa wale waamini wa kristu wataungana na mimi kuwa habari za Mungu na uumbwaji wa dunia zilikuja kuandikwa na Musa, na Musa aliziandika kama vile aliziishi ijapokuwa karma ya kiroho inasema Musa alikuwa mbeba kizazi yani kizazi cha Musa kikaishi miaka 2000, Kikaja kizazi cha Eliya Mtishibi nacho kikaishi miaka 2000, Kikaja kizazi cha Yesu nacho kimeishi miaka 2000, sasa kwamjibu wa karma ya kiroho nikuwa Mungu mwenyewe ameshuka kukiongoza kizazi hiki tunacho ishi mimi na wewe,

Vivyo hivyo kwa upande wa binadamu wa kiafrika habari zake na uumbwaji wake zimekuwa zikitoka kwa binadamu weupe wazungu, kanakwamba wao waliyaishi maisha ya mwafrika huyu.

Je, nikweli kwamba, hapo zamani za kale Waafrika hatukuwa na Historia; na kwamba Historia yetu ilianzia baada ya kuja kwa Watu Weupe wazungu

Na iwapo suala hili jawabu lake ni hapana, kuna uthibitisho wowote wa Kihistoria unaothibitisha kwamba, kuna wakati ambao Mwafrika hakuwa Mnyonge na kwamba aliwahi kuwa juu kimaendeleo dhidi ya Watu wa Jamii nyingine Duniani.?
Hii ni mada nzuri sana, Afrika ilikua na historia na hii ipo dhahiri. Licha ya kwamba elimu yetu inaonesha kwamba historia huandikwa lakini tunasahaulishwa vyanzo vingine vya historia.
Historia ni mtindo wa maisha na hudhihirishwa kupitia mtindo wa maisha kisiasa, uchumi na jamii vilevile sayansi na teknolojia. Uthibitishe wa kuwepo kwa historia upo kupitia mambo kadhaa ambayo yalipenya misukosuko ya wageni, utunwa na kutawaliwa.
Tukiabgalia imani za asili, kazi za sanaa, mitindo ya ujenzi, utawala, matibabu na mengine mengi ni uthibitisho wa historia ya Afrika kabla ya kuingiliwa. Ningeeleza zaidi ila nipo kazini hapa!
 
Haya tunayathibitishaje?
Historia iliikuwepo ila haikuandiikwa, hao wazungu walipokuja Afrika walikuta ardhi tupu bila watu, na kama waliwakuta watu pia waliwakuta watu wazima ambao ambao tayari walikua wamefanya meengi, kwako wewe mkuu historia nini?
 
They've made us feel inferior because we're so superior. We've to wake up now and see the real picture folks or else we'll be forever doomed.
Tatizo la afrika in the first place was u mimi mwingi, you just imagine kulikuwa na kingdoms zaidi ya 1000 kwenye hili bara, wanapigana porana ardhi and those stuff wazungu wakaja wakashirikiana na rivals wakachukua kingdoms after kingdoms, mkwawa hakuna alomsaidia tena maadui zake wa palepale iringa waliside na wajerumani, usnitch kama huo ulifanyika maeneo kibao, that was just to illustrate utengano tulokuwa nao kabla, wakafanikiwa wakachukua matawala hadi ikawa nchi moja chini ya serikali za wakoloni. Wakaleta dini zao zikatugawa kiimani wengine wakaendekeza hiyo migawanyo ya kikabila hadi sasa inafanya kazi kama sudan kenya kidogo etc. Tz sisi ukabila umekwishaga, tatizo dogo ni hii migawanyo ya kiimani huyu anataka barikiwa na God wa Israel huyu wa Saudia wengine kwingineko. Hapa kwenye suala la dini ndipo waafrica watateseka napo after ukabila if and only if hatutoshtuka. Mungu ni wewe na roho yako mazee, hii migawanyo kuna wajinga nahisi walikaa chini wakaisuka ili warule over, u know that phrase divide and rule. That's it. So wakuu inabidi tukae chini tutulie tujievaluate sana, mambo haya si kama tulivyokuzwa tukidhani, sababu hili tatizo lisipotatuliwa africa hatutaona mwanga.
 
Waafrika wana historia na falsafa tatizo ni matokeo ya utumwa yalifuta kila kitu kilichokuwa ni utambulisho wa muafrika. Kwa utafiti naoendelea kuufanya unathibitisha waafrika walikuwepo tena kabla ya adam na hawa, nitaiwasilisha ripoti kamili itapokamilika ila tambua Afrika was mother of civilization
 
Vivyo hivyo kwa upande wa binadamu wa kiafrika habari zake na uumbwaji wake zimekuwa zikitoka kwa binadamu weupe wazungu, kanakwamba wao waliyaishi maisha ya mwafrika huyu.

Je, nikweli kwamba, hapo zamani za kale Waafrika hatukuwa na Historia; na kwamba Historia yetu ilianzia baada ya kuja kwa Watu Weupe wazungu

Na iwapo suala hili jawabu lake ni hapana, kuna uthibitisho wowote wa Kihistoria unaothibitisha kwamba, kuna wakati ambao Mwafrika hakuwa Mnyonge na kwamba aliwahi kuwa juu kimaendeleo dhidi ya Watu wa Jamii nyingine Duniani.?

Fufu la Binadamu wa kwanza karne hii wapi inapatikana?. Kama kweli Biandamu wa kwanza kaanzia Tz kwanini tuko nyuma kiasi hiki hata Afrika?.

Olduvai Gorge - Wikipedia, kamusi elezo huru
UrlAdvisorGoodImage.png

Kwa kuwa watu wanadhaniwa kutokana nao, eneo hilo pengine limeitwa kwa Kiingereza Cradle of Mankind, kitovu cha binadamu, ambao wameishi katika eneo hilo kwa walau miaka 17,000 mfululizo.
 
Back
Top Bottom