Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,008
Nilikuwa na mjadala na rafiki yangu mmoja na mada husika ilikuwa inajadiliwa. Kwamba, ati mwanamke akiugua labda kwa mrefu kidogo mwanamme hawezi kutulia sana huamua kutafuta kidumu au mahali pa pembeni pa kujiliwaza. Kwamba mwanamme hana ule upendo wa kweli wa kumpenda mwenzie katika shida na raha. Hoja nyingine ilitolewa kuwa wakati mwingine ni mwanamke mgonjwa ambaye anamuencourage mumewe kwenda kutafuta wa kumliwaza kwamba hawezi/hataki "kumuona" mumewe anamuangalia tu hata hawezi kumpatia mapenzi yake bora amuache atafute mwingine!
Hoja ikawa kinyume chake hata hivyo si kweli. Kwamba, mwanamme akiugua mwanammke atajitahidi kuwa naye na anakuwa kama ameamua kutawa. Ni mara chache sana kumkuta mwanamke ambaye anampenda mtu wake kiukweli na akaugua halafu yeye akamtelekeza kwenda kwa mwanamme mwingine. Mshirika tuliyekuwa tunapiga soga akasema "labda wanawake wa enzi hizo, hawa wa dot com 'they will leave your @ss in a minute'" alisema.
Ni kweli kuwa linapokuja suala la kuugua na kuuguzana tunapenda tofauti? Kwanini?