Ni kwanini bado Waarabu wanatubagua, hata Mwafrika anapokuwa Muislam wanamkatalia kumuoa binti yao?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,046
Kwa wazungu ndoa za waafrika na wazungu zipo nyingi tu, ni kawaida.

Shida inakuja kwa waarabu, yani hata uwe muislam uliekariri aya nyingi za korani na sauti nzuri ya kuzinukuu hawawezi kukupa binti yao labda kama utaweza kutumika kimaslahi aidha uwe na cheo kikubwa serikalini ama uwe na pesa nyingi sana.

Na hapa navomaanisha waafrika ni hadi wazanzibari ambao hufanana na wasomali, hali ni hivyo hivyo tu, japo wao hupenda kujiweka kundi moja na waarabu ila waarabu huwaona ni zao la watumwa
 
Kwa wazungu ndoa za waafrika na wazungu zipo nyingi tu, ni kawaida...
Kuna ndoa kibao za Weusi na waarabu, tatizo mila zetu na zenu ni tofauti. Kwetu ndoa sio matangazo ya TV kila mtu ajue.

Juzi tu Alpha Blond kaoa Mwarabu.

images (40).jpg
 
Umasikini ni kama una sumaku, ni ngumu sana masikini kutajirika, atahitaji nguvu ya ziada kuvunja mzunguko wa umasiki katika familia.

Kwa hiyo nawaelewa wanaepuka shida za umasikini. Pia ukiwa masikini kila kitakachoongelewa au kufanyika; utaanza kujishtukia kama wanakusema au kubaguliwa.

Japo sikatai kuwa ubaguzi haupo
 
Unafuatilia nini ?!!!

Hivi ukijiamini unabaguliwaje ?!!

Unaanzaje kubaguliwa??!!!

Iwe na mwarabu ,mhindi ,mzungu ama mchina?!!!

Waafrika tu wako wabaguzi dhidi ya wenzao....kikabila ,rangi ,kipato....ssmbuse watu wenye rangi nyeupe?!!!

Dunia ya sasa ya SOKO HURIA na MAARIFA mapana...vilio vya kubaguliwa havina maana....

Unakuwa wapi mpaka mtu anakubagua?!!

Mfukoni mwake ?!!!

Kwanini uwe mfukoni mwake ?!!

Why desperation?!!!

Umesema kuwa mwafrika hata awe muislam na kuwa (Qari) fundi wa kusoma Quran hawezi kuoa hao waarabu...right?!!!

Nisikilize....watu wengi hawana imani ya dini vile wanavyojionyesha ukubwa wa kuwa nayo....iwe hao waarabu ama wengineo....

Sasa unataka mwarabu asiye na IMANI kubwa ya dini akupe binti yake kwa kuwa tu wewe "una sauti " kinanda ya kusoma Quran ?!!!

Hao waarabu wengi ni wafanyabiashara....akili zao ziko katika biashara na KUPATA FEDHA eti wakuhusudu wewe MRANGI ,MDIGO ,MUHA uliyehifadhi msahafu kwa kichwa na huna kitu wakupe BINTI YAO kwa kigezo hicho tu labda zamani....sikatai..ziko familia chache ila wengi wakitaka KUZISIKIA HIZO SAUTI NZURI zikisoma QURAN(tajweed ,tartil na hukumu zake) wanawaita walimu wa madrassa wakitoa elfu 50...walimu hao wanakuja na vitoto vya madrassah na kuanza kusoma Quran tukufu ,ikifuatiwa na WASSILATU SHAFI ,Kitabu cha Maulid Barzanji ,wanapiga madufu na nari zake wakimaliza wanajipiga BIRIANI chuzi zitooo...nyumba ya mwarabu tena ,kitonga mseleleko....shughuli ikiisha wanawaaga mpaka siku nyingine...ustadh anakwenda kutamba kijiwe cha kahawa na Al Kasus....
Ya nini mwarabu "afuge mkwe" wa kirangi ,kiha ,kisambaa ,kinyaturu ,kimeru kisa tu NI FUNDI WA KUSOMA QURAN?!!!

Dunia imebadilika....fedha fedha fedha si hao waarabu si wewe Mngoni.....

#SiempreJMT
#MamaAnaupigaMwingi

#DP World ndio habari ya mjini

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Sipo kuichafua Dini yangu ila hawa Jamaa ni next level.... niliingiaga Msikiti wao kwa kweli nilipata tabu sana... kukaa Mstari mmoja na Mtu mweusi kwao hawataki na ukikaa nao utaona wanavyosegea na kuacha nafasi kubwa kati yao na wewe.... wakiingia Msikitini wote wewe ukija wakikuona kufunga Mlango si jambo la kushangaa
mbna hatariii lol
 
ila kuna kiwango chake sasa,

waarabu wamezidi sana
Uko desperate unataka upendwe na kila aliyeko mbele yako ?!!!

Uwe na chako uingie mikataba kama hii ya DP WORLD...na si kulialia tu

Hakuna mwenye kujiamini akabaguliwa....wanaanzaje?!!!

Mbona hao waarabu wakitaka kitu kwako HAWAKUBAGUI?!!!

Ni sawa tu na mswahili na mtanzania akitaka kitu kwako....atakuachia tabasamu na salamu nzuri tu....kinyume chake anaweza kukupita nje kwako bila ya salamu ilihali ni majirani hata miaka kisa tu wewe uko chini kikipato kuliko yeye....Binafsi NIMELIEXPERIENCE hilo mara kibao katika hurstling zangu tena kutoka kwa vijana wa umri wangu....ajabu siku anashoboka na salamu nyingi kumbe kuna kitu anahitaji....wabongo weusi tiii

#MamaAnaugongaMwingi

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kuna ndoa kibao za Weusi na waarabu, tatizo mila zetu na zenu ni tofauti. Kwetu ndoa sio matangazo ya TV kila mtu ajue.

Juzi tu Alpha Blond kaoa Mwarabu.
View attachment 2656004
Pesa hiyooo.....

Pesa hiyooo....

Huna kitu unalialia kuwataka "wamanga" utawapatia wapi ilihali hao WAMBULU NA WABARBAIGW na WARANGI mabaamedi hawakutaki apeche alolo huungii "Heineken"

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom