Nimemkumbuka Ma-samaki wa TRA na tuhuma za kumiliki nyumba sijui sabini na ngapi kumbe uongo tu,mwingine sijui anaingiza milion 7 kwa dakika daah mambo ni
Watumishi wa Umma waheshimiwe.Wanasiasa lazima Waheshimu Watumishi wa UmmaHabari zenu wanabodi.
Kuna jambo niliobserve kwa muda sana na leo nimejikuta natype hapa ili kushare na wenzangu ambao wamewahi kulifikiria hili .
Miaka ya hivi karibuni husasani kipindi hiki cha awamu wa 5 na haswahaswa Sasa hivi kumekuwa na trend za tumbuatumbua na kuhoji watumishi na viongozi wengine hadharani Huku wananchi wakipiga kelele kuonesha either mtumishi huyo au kiongozi husika hafai na kama ilivyotokea leo huko nachingwea mtu alipopewa fursa ya kuongea alisema yeye anachotaka ni mtu kutumbuliwa tu.
Nimekuwa nikipitia post mbalimbali hususani pale mtu anapotumbuliwa au kushtakiwa unakuta wengi wanasema huyo ni mhujumu uchumi etc etc lakini ukija in details unakuta mtu huyo wala sio mbaya na wengi wanaocomment wala hawamjui zaidi ya kumsikia siku hiyo,ila unakuta ndo kwanza wanataka asulubishwe asulubishwe.
Najiuliza hii mob ya wapiga kelele kwenye mikutano na mitandaoni huwa haina ndugu ambao ni watumishi wa umma? Haina jamaa na marafiki huko kwenye utumishi? Kwa nini inahukumu bila ata kujua ukweli uko wapi ? Likimpata mtu ambaye mpiga kelele au watoa hukumu hao wanavinasaba naye will it be the same ?
Hiki kitu nashindwa kuelewa ni notion iliyopandikizwa kuwa kila mtu anayedhalilishwa ni mwizi kweli au ni wivu wetu tu sisi Watanzania? Ni husda au ni chuki tu na watu ambao ata hatuwafahamu muda mwingine?
Kuna muda binafsi huwa najikuta naumia na kushangaa kwa nini tunafika hapa.Naomba mawazo yenu wanabodi kuhusu hili jambo ni nini hiki kimetufanya hivi? Tunafurahia matatizo yanapompata mtu ata kama hatumjui?