Wazazi tunaozijua tabia mbaya za koo au makabila yetu tuwe mstari wa mbele kuwaelimisha watoto, walimu wa shuleni na dini bado wana msaada mdogo

R-K-O

JF-Expert Member
Jun 27, 2023
482
2,138
Na kama mjuavyo tumeshatoka kwenye mfumo wa kuishi kwa makabila chini ya machifu kwa sasa tupo kwenye taifa ambalo sehemu kibao tunashi pamoja kwenye miji na majiji, Tabia kadhaa zinazoweza kuvumilika na koo au kabila basi kwenye jamii iliyochanganyika inaweza kuwa kero, kuleta aibu na hata adhabu kali kwa sheria za nchi.

hakuna kipindi kizuri cha kumuelimisha mtu kama kipindi akiwa mtoto, na mzazi ndie ana nguvu zaidi ya kumpa umakini wa kumuelimisha mtoto wake, kipindi hiki bado anakuwa mbichi unaweza kumkunja mapema kabla hajakakauka,

Mamlaka na nguvu ya mzazi kumuelimisha mtoto ni kubwa sana, kuna walimu wa shuleni, msikitini, kanisani, n.k. lakoni nguvu ya mzazi katika malezi ni kubwa mno.

Kila ukoo na hata kabila huwa zipo tabia mbaya , hizi tabia zinakuwa zimezoeleka sana, wewe unaweza ukawa umezikwepa lakini mtoto wako anaweza kuja kurithi tabia kama za baba yako, babu yako, n.k. na hali huwa mbaya zaidi usipomuelimisha mapema.

Kuna koo / kabila hupenda wizi na utapeli kupata hela za haraka.

Kuna koo / kabila Mtu akipata pesa anakuwa na majigambo na kuwaona masikini si watu.

Kuna koo / kabila wanawake wakitongozwa kidogo tu hawaoni shida kutanua mapaja.

Kuna koo / kabila ni wachafu.

Kuna koo / kabila wanasifika watu wao kuwa na kiburi na jeuri kupindukia

Kuna koo / kabila hupenda kujitenga tenga.

Kuna koo / kabila Kuna koo / kabila uvivu ni tatizo kubwa, kutwa kupiga domo, hawapendi kujishughylisha,

Usiingie mtego wa kudhani tabia hizi ni nzuri kwasababu watu wa ukoo au kabila wanakinga kwamba kila kabia lina tabia hizi, kumbuka kinachofanya kitu kisifike ni kipimo chake kuzidi ukawaida uliozoeleka, mtaa A unaweza kuwa na watu wawili mwenye tabia mbaya ila mtaa B kuna watu 30 wana tabia mbaya, mitaa yote ina watu hawa lakini tabia hio itasifika zaidi ni mtaa B kwasababu imevuka ukawaida na ni kinara, tabia hii itazidi kumea na kusambazwa zaidi.

Pia tabia mbaya haina visingizio, kwenu husema mwili huhitaji mapumziko lakini jua mapumziko yakizidi na kukwepa kazi ni uvivu, kwenu watasema hatupendi dharau ila kuna mipaka ya kuingia kiburi na jeuri, watasema tunajiliwaza na magumu tuliyopitia ila zikiwa kelele huwa ni majigambo, watasema ni ujanja wa kuwa na akili na ujasiri lakini kuchukua vitu vya mtu bila ridhaa ni wizi na utapeli, n.k.

Hizo bi baadhi ya tabia ambazo ukichunguza ukoo wenu ama hata kabila unakuta zimesambaa sana, nakwambia hata kama wewe umeziruka basi tegemea mtoto wako atakuwa nazo

Sisi kama wazazi tuna jukumu kubwa sana la kuhakikisha tunapunguza ama kutokomeza kabisa tabia hizi kwa watoto wetu maana tunajua kikamilifu na kwa undani sehemu tunazotoka

Kama unajua uvivu ni tabia yenu, hakikisha unamzoesha mtoto kazi na ayajue matunda ya kazi na aipende kazi pindi akiwa mdogo itasaidia hata akiwa mtu mzima apende kazi.

Kama unajua kwenu kuna mambo ya wizi na utapeli kaa na mtoto wako uwe unampa elimu ya madhara ya wizi na utapeli, muhadithie kama uliwahi kuibiwa jinsi ulivyorudi nyuma kimaendeleo, jinsi wezi walivyofanya ukose hata pesa ya kula, mwambie kwamba wezi na matapeli watu wabaya.

Kwenu tabia ya umalaya inasifika hasa kwa wanawake, mama kaa na mwanao mwambie asijirahisishe, muhubirie sana thamani yake kama mwanamke, muelezee madhara ya kuwa malaya, aibu atayoleta kwenye family, heshima atayojishushia, magonjwa ya zinaa muonyeshe picha kabisa.

Kwenu mnasifika kwa kuishi kwa kujitenga tenga hakikisha unafunza wanao kwamba kuna watu wazuri na wabaya hii dunia na ni muhimu kujua kuishi nao, dunia hii utake usitake utahitaji msaada wa wengine, awe makini na marafiki sio kila mtu rafiki, awe makini na machawa, ahudhurie shughuli za kijamii kama misiba hasa ya majirani maana mae ni mwanajamii, n.k.

Kwenu mnasifika kwa majigambo na hata dharau basi mhusie mwanao tangu akiwa mdogo kwamba anapopata ashukuru kwamba hajakosa na asaidie wasionacho, sio kuanza kutambia wengine, kudharau wenginr, n.k.

Kwenu ushamba umetawala, mhusie mwanao kwamba usichojua usiwe mbishi wa kuonekana unakijua utadhalilika, mfundishe kuvaa kwa mpangilio, mfundishe kujishusha afundishwe pale anapokutana na mapya, mfunze kukwepa majigambo.

Kwenu watu ni wachafu, anza mapema kumfunza mtoto iwe ni lazima kuoga kila siku, iwe lazima kuvaa nguo safi kila mara na umfunze kuzifua, chumba chake kiwe safi muda wote, n.k. hata huko mbele usipomsimamia akipunguza usafi basi iwe nafuu na sio kero kwa wengine.
 
kama unataka kuoa nenda Kijijini kwao kwanza ,ukikuta wale watoto ambao hawana baba wapo kibao kwa bibi tambua huo ukoo una matatizo kabisa na kuna hasara nyingi ukiingia.

Cha kwanza ,hao madogo kazi kutegemea wajomba na ndugu ,kama ukiwa na uwezo jiandae kuwabeba moja kwa moja ila kumbuka baba zao walishawakataa hapo ndo balaa.

Cha pili,kwa wengine wanaamini mtindo wa kuzaa watoto hovyo bila ya ndoa huleta nuksi na mikosi kweny familia na koo kwa ujumla...Unawza kuingia kweny ukoo umelaaniwa kabisa ni balaa lake ni zito unakuta wanao hata shule wote wanafeli , hawaelewi mara unakuja kuzaa vibaka ,wezi na wazinzi wanakuletea watoto bila ya baba nyumbani.
 
kama unataka kuoa nenda Kijijini kwao kwanza ,ukikuta wale watoto ambao hawana baba wapo kibao kwa bibi tambua huo ukoo una matatizo kabisa na kuna hasara nyingi ukiingia.

Cha kwanza ,hao madogo kazi kutegemea wajomba na ndugu ,kama ukiwa na uwezo jiandae kuwabeba moja kwa moja ila kumbuka baba zao walishawakataa hapo ndo balaa.

Cha pili,kwa wengine wanaamini mtindo wa kuzaa watoto hovyo bila ya ndoa huleta nuksi na mikosi kweny familia na koo kwa ujumla...Unawza kuingia kweny ukoo umelaaniwa kabisa ni balaa lake ni zito unakuta wanao hata shule wote wanafeli , hawaelewi mara unakuja kuzaa vibaka ,wezi na wazinzi wanakuletea watoto bila ya baba nyumbani.
Ndio hapo sasa, hizo tabia za koo au kabila mzifanyie juhudi kuelimisha watoto wasiziendeleze, hii inaweza kusaidia kupunguza.

Baadhi ya koo shuleni ni hovyo sababu watoto wamebeba tabia ya uvivu, hapa yafaa kuwafunza wawe na bidii na kuwaonyesha matunda ya bidii
 
Back
Top Bottom