Kuna mengi yaliendelea achilia nafasi ya umakamu Rais, kuna pesa za karafuu zilizomezwa na muungano na huyu mzee hilo lilimuuma na kuhoji kwanini imekuwa hivyo. Pia kuna swala za Zanzibar kuwa nchi alilisimamia kwani alitaka kuwapo na serikali tatu na hilo likawa mwiba mkali kwa Nyerere akaona jamaa ni msaliti akishirikiana na kina Seif Sharif Hamad. Pia alihoji uhusiano wa Vatican na Tanzania na hilo halikumpendeza Nyerere akaona atamuharibia uongozi pengine (Soma katika kitabu chake).
Kweli viongozi wakubwa wanapostaafu na kurudi kwao wanasaidia sana kuchochea maendeleo ya maeneo wanayotoka. Mfano baba wa taifa Mwl Nyerere baada ya kustaafu alirudi kijijini Butiama kuendelea na kilimo kama alivyoamini kuwa siasa ni kilimo.Maendeleo ya kijiji cha Butiama yasingekuwa hivi kama Nyerere asingerudi na hatimaye baada ya kufa alizikwa pale. Cleopa Msuya mmoja wa mawaziri wakuu wastaafu alirudi Usangi na kuchochea maendeleo huko. Siamsahau pia Peter Kisumo. Malecela naye yuko kwao. Nakubaliana kabisa na wewe kuwa ni vizuri viongozi wakubwa wanapostaafu warudi kwao ili kuchochea maendeleo. Wakati mwingine nadhani viongozi wasiorudi kwao huwa wanakuwa ni wale ambao hawakuwa wakithamini kwao kwa kwenda mara kwa mara na kusaidia maendeleo ya maeneo yao hivyo baada ya kustaafu wanashindwa kurudi kwakuwa hawakuweka mazingira mazuri kwao. Wengine huishia kuzikwa nje ya kwao. Vile vile kutokana na kukosa ushirikiano na watu wa maeneo ya kwao wanashindwa kurudi. Hapa ndipo najiuliza imewaje Mkapa ahamie Lushoto badala ya Masasi baada ya kustaafu. Sumaye naye yuko kwao? Mimi nawashauri viongozi wachukue changamoto ya Mwl Nyerere ya kurudi vijijini kwao baada ya kustaafu na sio kung'ang'ani Dar mpaka warudishwe wakiwa wafu. Wakihitajika kwa ushauri watafuatwa huko huko.Mdondoaji,
..hata Mzee Mwinyi naye kajibanza huku Tanganyika "analima" maembe.
..Sheikh Idiris Abdul Wakil Nombe naye alikuwa kajinafasi Ilala-Bungoni.
..Maalim Seif naye inasemekana alikuwa akiishi hotelini hapa DSM. sijui kama ni kweli.
..Hamad Rashid Mohamed naye anaishi Tanganyika akifanya biashara ya vyuma chakavu.
..Zanzibar itajengwa na nani kama watu kama hawa hawataki kwenda kuishi huko?
Inavyosemekana kosa, alilofanya Jumbe ni kuwa na dhamira ya kuanzisha mjadala wa kitaifa kwa lengo la kuanzishwa hapa nchini mfumo wa shirisho badala ya serikali mbili.
Jamani basi hata kabla ya kutoa tuhuma muwe na uhakika wa historia basi... ati Jumbe yuko kifungo cha maisha!
Miaka ya tisini nimewahi kufika kwa Jumbe na siku ona dalili za kifungo alikuwa anasafiri na kuishi huru labda sijui maana ya kizuizini. alikuwa jirani mzuri kule mji mwema na sikuona akizuiwa kwenda atakako.
Mdondoaji,
..inawezekana Mzee Aboud Jumbe hataki kushiriki shughuli zozote zile za kisiasa/kiserikali.
..niliwahi kusoma kwenye magazeti kwamba Mzee Jumbe ameacha wosia kwamba akifariki asizikwe kwa heshima za kiserikali na kijeshi kama inavyofanyika kwa viongozi wengine wakuu.[/QUOTE
Wasia wa Alhaj Aboud Jumbe
unapatikana katika makala ya AN-NUUR
gazeti la Kiislamu la kila wiki toleo na 247hulHijja1420/machi31 - april5,2000
Kuanzia hapo, madai ya Wazanzibari kutaka mabadiliko ya Katiba, huku wengine wakitaka warejeshewe Visiwa vyao (Zanzibar), kupitia mihadhara, magazeti na redio, yalipamba moto ambapo wanajeshi wa Kizanzibari nao walikuwa na malalamiko yao.
Mashambulizi yenye kashfa nzito nzito na matusi ya kisiasa yaliongozwa na redio ya ufichoni iliyopachikwa jina la Kiroboto Tapes, hadiilipogunduliwa na kuharibiwa na wanajeshi kutoka Bara. Mitafaruku yote hii ilikuwa na ridhaa ya Alhaj, Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi.
Ukizisoma hizi BOLD mbili unapata picha hii ilikuwa ni vita ya kijeshi, ambapo Jeshi la Visiwani lilishindwa vita na kusalimu amri kwa Jeshi la Bara.
Ukizisoma hizi BOLD mbili unapata picha hii ilikuwa ni vita ya kijeshi, ambapo Jeshi la Visiwani lilishindwa vita na kusalimu amri kwa Jeshi la Bara.
Lakini Nyerere aliamua kutomteua Kanali Seif Bakari kumrithi Karume kuwa Rais; Akapendekeza awe JUMBE ili kuondoa UJESHI ndani ya SIASA za ZNZ