Ni kipi cha thamani kwa mwanamke kati ya kitanda na mwili wa mwanaume?

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
19,254
42,873
Tunapoelekea mwisho wa mwaka, nikaona nijaribu kuleta kwenu hii hoja ambayo imekua ikiibuka Mara nyingi hasa Kwa wanandoa wanaume.

Hapa naongelea Mme ameoa, anaamua kuchepuka anasema hawezifanya hicho kitendo na mwanamke mwingine kwenye Kitanda anacholalia na Mke wake.

Sasa kama unamheshimu mkeo kiasi Cha kuthamini Kitanda unacholalia nae, mwili wako si ndio unatamani zaidi ya Kitanda? Kwanini umpe mwili wako mchepuko na kuhangaika kufanyia eneo lingine kisa heshima Kwa Mke wako?

Ukishaamua kusaliti, hua hapo hakuna Tena suala la heshima haijalishi utafanyia kwenye mti, vichakani, hoteli ya nyota 5 au ufukweni. Tuache kujifariji.

Niwatakie heri, afya njema na mafanikio wanajukwaa wote wa JF tunapoingia mwaka 2023.
 
Kuna mahali haupo sawa..au sija kuelewa.kwaio tusichepuke au?
Kwa nilivyo muelewa…anauliza kwanini kitanda kionekane kuwa kinathamani(mke au mume kupiga game kwenye kitanda chao na sio mwili wa mhusika?)

Yani yuko tayari akachepuke kwenye kitanda cha nje ya nyumbani kwao lakini amesahau kuwa mwili unathamani zaidi ya kitanda.

The Monk nirekebishe
 
Kuna mahali haupo sawa..au sija kuelewa.kwaio tusichepuke au?

Ukiamua kuchepuka, achana na mambo ya kusema unamheshimu mkeo Kwa kuogopa kuchepuka kwenye Kitanda unalalia na mkeo.

Mwili wako ni WA Thamani kuliko Kitanda, ukishafikia hayo maamuzi, ni dhahiri suala la heshima Kwa Mke usilitaje sana hasa Kwa kuogopa Kitanda wakati unautoa mwili wako Kwa mchepuko.

Suala la kuchepuka au kutokuchepuka ni muamala tofauti japo unahusiana na hii hoja
 
Kwa nilivyo muelewa…anauliza kwanini kitanda kionekane kuwa kinathamani(mke au mume kupiga game kwenye kitanda chao na sio mwili wa mhusika?)

Yani yuko tayari akachepuke kwenye kitanda cha nje ya nyumbani kwao lakini amesahau kuwa mwili unathamani zaidi ya kitanda.

The Monk nirekebishe

Agiza mirinda nyeusi hapo Kwa Mangi utume na lipa namba mambo yasiwe mengi.
 
Ni kama mtu anaingia lodge halafu eti anavua Pete ya ndoa anaihifadhi pembeni kuwa anaiheshimu ndoa yake,
Screenshot_20221205-163219.jpg
 
Kwa nilivyo muelewa…anauliza kwanini kitanda kionekane kuwa kinathamani(mke au mume kupiga game kwenye kitanda chao na sio mwili wa mhusika?)

Yani yuko tayari akachepuke kwenye kitanda cha nje ya nyumbani kwao lakini amesahau kuwa mwili unathamani zaidi ya kitanda.

The Monk nirekebishe
kwamba ukichepuka una uharibu huo mwili au! kwasababu unasamani..labda kama mtu uchepuke nawenye magonjwa
 
Swala ni heshima tu,
Heshima ni positive feeling tunaonyesha kwa mtu wetu wa karibu au tunayedhani ni mtu anayetakiwa kulindiwa hadhi au tumempa hadhi ya juu sana. Kutochepuka mbele yake, watu wanachepuka miaka kumi na wapo kwenye ndoa zao zenye furaha, wapo wamezaa kabisa. HESHIMA. Regards kwa yule hufanyi mbele yake inatosha.
Ndio maana utamtukana rafiki yako tusi kubwa wakati wa stru na si baba yako.
Kuchepuka nje ya kitanda cha wewe na mkeo, nikuonyesha ni jinsi gani unamuheshimu. Hata kuvua pete wakati wa kuchepuka, as well as , swala si tu kitanda , kwahyo unadhani mtu mwenye nyumba vyumba vitatu anaweza kuja na mchepuko akachukua chumba kingine na kulala nae?.
HESHIMA IS ALL I HAVE TO SAY.
 
Ukiamua kuchepuka chepuka usigunduliwe iwe kitandani kwenu au bafuni, ukijulikana ni dharau sana na huonyesha dhairi umpendi mkeo, chepuka usigundulike wala kutiliwa shaka,
 
Back
Top Bottom