Ni kheri arudi urais Benjamin Mkapa kuliko uongozi wa Jakaya Kikwete: What does that tell us?

Me naona imefikia mahali 2kubaliane kwa pamoja kuwa serikali iliyopo madarakan imeshindwa kutekeleza majukum yake, coz inapofikia mahal ukaona ktk uongoz wako migomo ya mara kwa mara haish bac kimsingi ujue umeshindwa kutekeleza majukum yako! Leo hii mpaka watoto wa shule ya msing wanagoma wanalala barabaran eti ha2ondoki mpaka kieleweke..ths iz too much bhana, jiulize mtoto huyu lin amejua maana ya mgomo? 2mefikia pabaya rais anashidwa kutoa maamuz magum, hii nikumaanisha kuwa hafai kuwa kiongoz kwan hata kama unawapenda vp hao mafisad bt as tym goes on u hve 2 do something 4 ur nation! Kumbuka hata Mungu ali2penda sana bt ilifika mahal ilibid atoe maamuz magum kama ilivyotokea ktk kizaz cha NUHU as wel as SODOMA NA GOMORA!

Kwid;

Its true ..There come some times in our life ..where .. We must be able to do what is to be done ...and sometimes we have to do the impossible...!

I tought Jk is the person who can DARE!! and be the example of this ... But ..!!! and honestly I dont see one in CCM neither in CHADEMA ...unless one can point one for me .. I would be very much happy to see the name posted here!!!
 
Zama za Kikwete ni Kama za Nyerere, anatusaidia kudai Uhuru wetu upya. Subiri utaona, for better or worse
 
Kwidi... hio in blue hata CCM wenyewe wanatambua hilo but hawawezi tamka... thou matendo yanawasemea....
<br />
<br />
i lyk ur comments gal, logicaly it seems u ve something on ur mind..bt nahic kuna wa2 wanaweza wakawa wanakuelewa tofaut au hawakuelewi kabisa coz u based on facts na hufungaman na upande wowote kwa maslahi yoyote" binafsi hapo mwanzo nilikuwa ckuelewi sasa nakuwa kama nakuelewa unakoelekea! Bigup one luv"
 
Mkandara

Niseme kuwa Nimevutiwa zaidi na matamshi hayo niliyowekea rangi ya buluu!!

Katika nguvu mbalimbali zinazopelekea mabadiliko kutokea kwenye jamii yoyote moja ni kama hiyo uliyoeleza hapo...

Naamini kuwa wakati wa wakoloni ..mateso na ukandamizaji huo .. zilikuwa nguvu tosha kuwafanya wananchi wa wakai ule .. wafikie kikomo cha kuonewa na kudhalilishwa Utu na heshima yao. Naamini kuwa kunakiwango cha mwisho cha mkadamizo kilichofikiwa kwa Watanzania wa wakati ule ndipo ..TUKAWEZA!!

Kwa sasa bado ninaamini kiwango hicho cha kukandamizwa hakijafika kwa Watanzania wa leo. Kila mwanadamu anakiwango cha mwisho cha uvumilivu ..ambapo baada ya hapo .. lazima atachukua hatua hata kama hatua hiyo itavuka mipaka ya busara na hekima. Na pia kila jamii inakiwango cha mwisho cha kuvumilia ..na lazima woga utaondoaka na ujasiri mkuu hutokea na jambo la kufanywa huwa linafanywa. Hapa jambo hilo si rahisi kulibashiri .. kwani inategemea watu hao watagushwa vipi. Lakini Kwa kuwa umesema tuko ICU ... nafikiri BREAKING POINT ... kwa kizazi chetu haiko mbali... Na hili ni jambo la kutiliwa maanani sana kwa wale wanaolitakia Taifa letu Mema. Ni vema kufuatia mbadiliko haya na ikiwezekana kuyalea na kuyaogoza Yaishie kuwa yanafuata mikondo ya Ya Utu, hekima, ubinaadamu na upendo kwani ikiwa kinyume chake maafa yanakuwa ni makubwa bila sabau yeyote!

Lakini kabla ya tukio hilo muhimu halijafikiwa nawatakia Watanzania wenzagu .. burudani njema ... huku tukionewa na kikundi cha watu wachache na kutupeleka kwa namna wanayotaka... Sasa wasifanye hivyo ..iko wapi nguvu ya UPINZANI? iko wapi kauli na vitendo vya KUPINGA NA KUTAKA KUJIOKOA??
Mkuu wangu shukran sana na napenda kusema tusiwe na tumaini zaidi kwa kutegemea Mtume au hero kusema kweli hilo hatuna na hatuwezi kuwa na hero ambaye atatoka ndani ya chama kwa kuchaguliwa na chama kusimama. heroes ziku zote huzua fikra pevu ambazo huwavutia wananchi na wakajiunga nyuma yake..

Halafu kwa Unafiki wetu siku zote Heroes wetu wametokana na fedha - The root of all evil kina Rostam, Lowassa, Chenge na wengine ambao sitaki hata kuyataja majina yao ambao huko majimboni kwao ndio huonekana mashujaa kwa sababu tu wanamwaga Takrima kisawasawa. Na acha hawa watoto wetu wauza Unga na wezi wanaoweza kurudi nyumbani na Range Rover, wakajenga majumba ya fahari ndio rolemodel wetu hivyo kutegemea kumpata kiongozi ktk sura ya Ukombozi wa kimaandishi haiwezekani..

Mimi nasema hivi ni rahisi sana kum underestimate Dr.Slaa kwa uwezo wake kuongoza, au hata Zitto kwa sababu tumegawanyika ktk mafungu ya Unafiki kushabikia.. Lakini ukweli utabakia kwamba hawa jamaa wameweza kusimama imara zaidi ktk maswala ambayo yanatukera sote na ajabu wameyafanya haya bila woga na hata kujitoa Mhanga ktk uwakilishi wa majimbo yao kwa hoja ya Kitaifa... bado wananchi tumeshindwa kuwaamini wachache kama Dr.Slaa au Zitto kwa sababu tu Dr.Slaa/Zitto ni Mkristu/Muislaam au wote ni wana Chadema...

Hivyo tusitegemee sana kumpata mtu mmoja ambaye anaweza kukamata nafasi ya Urais na kuleta mabadiliko isipokuwa nguvu ya chama kama jumuiya kushinikiza mabadiliko hayo kwa sababu tunapigana na nafsi zetu wenyewe..Kama vile wanavyosema kulia kuna malaika mwema na kushoto kuna Shetani hivyo huu mvutano hauko nje ya nafsi zetu na ndio maana tunashindwa kukikataa chama CCM kwa sababu ni sehemu ya maisha na historia yetu badala yake tunawasema kina Mkapa na JK na hata kutafuta mashujaa na sio chama Mbadala.

I think, Chadema wapo katika nafasi nzuri zaidi ya kushinda lakini sio ktk mazingira tulokuwanayo na CCM wajanja sana utafikiri Panya wanaouma na kupuliza. Leo utawasikia kuna wanachama wa CCM wanampinga JK ili wako ktk kundi linaloshabikia upande mmoja. Ni yaleyale ya Wapiganaji 11 wa CCM ambao lengo lao kubwa ilikuwa kupambana na Ufisad wa magamba ndani ya chama, leo wamefanikiwa wengine kina Wapambanaji tunapata majibu toka upande wa pili wakielekeza mashambulizi yao kwa JK..

Sisi wananchi tunayumba, hatujui kama kundi la Wapiganaji la CCM ndilo lilikuwa imara au hili la wapambanaji wanaomtolea Uvivu JK bila kueleza wanataka JK achukue hatua gani kuboresha utawala wake. Na bado tunatamani atokee mtu ndani ya CCM ambaye atakuwa na uwezo wa kuleta mabadiliko ambayo ndani ya nafsi zetu hatuyapendi..Kaazi kweli kweli!
 
Jaman achen kulinganisha watu kila m2 ana mapungufu yake to me the president is OK. Tatizo tu ni wale wanaomzunguka wanamwangusha...hatna sababu ya kulalamika hyo ndo raisi wetu hatuna budi kumweshmu naomba sana watanzania.if ur real great thnker mlitakiwa muelewe uchaguz mwingne n 2015 hvyo 2mpe ushirikiano rais aliyepo...NAOMBA KUTOA HOJA!
<br />
<br />
2cwe wanafiki either kwa kukaa kimya au kumcfia m2 hata pale anapokosea coz 2takuwa ha2jengi bali 2nabomoa! Mapungufu yapo ha2katai bt ths iz too much bwana..ucpopata muda wa kukaa nyumban kwako wadhan utajuaje matatizo ya familia yako? We nchi ipo vitani rais yupo disco? Kweli ukiwa kama baba unaona wanao wanachafua shati lako washidwa hata kuwakemea kama c kuwaadhibu? Au wadhani ukivaa shati lenye tope watasema mwachen coz wanae ndio wamelichafua c yeye?
 
Binafsi namkumbuka Benjamin Mkapa kwa Kuwauzia wazungu Migodi yetu pamoja na UFISADI aliofanya yeye na washirika wake.
Kina Balali, Sumaye, Yona, Mramba, Mkono, Chenge, Liumba, Mahalu na wengine wengi tu, na aliowauzia nyumba za serikali
 
kumrudisha Mkapa hakutasaidia,ninashangaa watu wanasema bora kipindi cha Mkapa na kipindi cha Mkapa walikuwa wakisema bora kipindi cha Mwinyi.Hakuna madiliko makubwa yaliyoka kiuchumi.Mnataka kuniambia kipindi cha Mkapa hakukuwa na watu wakuwa wakila na njaa?watanzania walikuwa na ajira?Mikataba mingi ya ulaghai ilifanyika kipindi cha Mkapa.Tanzania tunahitaji madiliko ya chama.
 
Mkandara,

Na sipendi hata kutafakari mvutano utakao tokea pale CCM ambayo nafikiri itakuwa imefiliska kabisa kisiasa wakati huo ..Itakapokuwa inajipigania nafsi yake ... kwa hali yeyote ...kujaribu kurudi madarakani.... dhidi ya chama kingine na uwezakano mkubwa ukiwa Ni CHADEMA ..Nina amini kuwa Busara fulani itatokea na Kuepusha ..matendo yasiyo na Busara na kuepusha mivutano isiyo na tija kwa Jamii yetu.

Lakini ni nani mwenye hiyo busara na upeo wa dhati wa kuona mbali na kujitolea kuliogoza Taifa kufikia hapa ninapo elezea ..hakikia SIMUONI!!


Azimio one thing you should know ni kua CCM wakianguka… watabaki jina tu… lakini they will never be able to rise again for Watanzania ni wapole lakini sio wajinga…. Itakua kama yale ya Kenneth Kaunda na UNIP … NDIO alikomboa inchi yake and did a lot but Wanachi wa Zambia wakachoshwa na serkali yake mpaka pale Chiluba alipokuja watoa with a bang! Na kash kash nyiiingi kwa mzee na tuhuma kibao ambazo zlikua with drawn from the time of Presidency…

Kuhusu CDM na Utawala mpya… mpaka CDM wawe katika utawala na waweze kabisa kuwafikiria Wananchi itachukua mda hata kama watafanikiwa kunyakua kiti katika uchaguzi ujao… Hivo Mtanzania wa kawaida akazane tu na kupigana na maisha hoping for the best katika mipango yake na kupata serkali mpya ili walau tuone kasi yao pia…. Hata hivo CDM Matendo yao yapo so set kubishana na kutaka kukomoa wapinzani (which is not bad – but inatakiwa kufanya kwa mpangilio na malengo kama walivyo fanya Eygypt na Mubarak; Maana itakua haina maana kushtaki mafisadi huku pesa zoote ziwe zimepotea na yabaki maneno tu kortini…..
 
Zama za Kikwete ni Kama za Nyerere, anatusaidia kudai Uhuru wetu upya. Subiri utaona, for better or worse

Yaani hapa mkuu sijakupata kabisa! Kwamba JK anatusaidia kupata Uhuru... or anachangia sie kutaka Uhuru??

i lyk ur comments gal, logicaly it seems u ve something on ur mind..bt nahic kuna wa2 wanaweza wakawa wanakuelewa tofaut au hawakuelewi kabisa coz u based on facts na hufungaman na upande wowote kwa maslahi yoyote" binafsi hapo mwanzo nilikuwa ckuelewi sasa nakuwa kama nakuelewa unakoelekea! Bigup one luv"

Appreciated Mkuu... nataka zaidi wataonielewa na kujua/ku realise where i am coming from... Kwamba kua interested na Siasa sio lazima niwe tu blind na kushikilia sehemu moja in the name of upinzani wa Chama kingine... Sijaona kama tuna that Luxury ya kuona na kugenrelise kua Chama hiki is absolutely RIGHT na kingine WRONG..... Naona kua woote in most cases (CDM Vs CCM) wapo sawa tu... kinacho tofautisha this two parties ni kwamba one is in power the other is not.... Na napenda yule ambae yupo katika Chama kimoja wapo akasifia wanapo patia na kukemea wanapo kkosea it is so constructive - kuliko kufumba macho na kusifia upuuzi sababu tu ni chama chake husika kimehusika....

Kuhusu wasio nielewa... naamini kua ni wale ambao anapapasa na kusoma comments kwa kuperooz kwa uvivu wa kusoma... or ambae yupo so prejudged na hataki kabisa kubadilisha ama kuongeza pale ambapo anafikiria... it is better basi aseme wapi tatizo then waweza muelewa kuliko kujudge from afar.... haijengi....
 
Binafsi namkumbuka Benjamin Mkapa kwa Kuwauzia wazungu Migodi yetu pamoja na UFISADI aliofanya yeye na washirika wake. Kina Balali, Sumaye, Yona, Mramba, Mkono, Chenge, Liumba, Mahalu na wengine wengi tu, na aliowauzia nyumba za serikali

Hapo umenena Mkuu... niongezee na kujimilikisha mgodi ambao mpaka sasa bado hatujui hatma yake....

kumrudisha Mkapa hakutasaidia,ninashangaa watu wanasema bora kipindi cha Mkapa na kipindi cha Mkapa walikuwa wakisema bora kipindi cha Mwinyi.Hakuna madiliko makubwa yaliyoka kiuchumi.Mnataka kuniambia kipindi cha Mkapa hakukuwa na watu wakuwa wakila na njaa?watanzania walikuwa na ajira?Mikataba mingi ya ulaghai ilifanyika kipindi cha Mkapa.Tanzania tunahitaji madiliko ya chama. li

Hapo ndio nashindwa kabisa kuelewa ni kwanini Wananchi tuna Memory spun fufi kiasi hicho.... Kwamba hata waweza entertain the thought of him being a president again!!! Hii ni insult kwa Mtanzania....
 
kichekesho. Hivo Mkapa ni bora kuliko Kikwete?. Ama nyinyi muna ndoto kweli. Huyu Mkapa ni adui wa nchi hii ametuua wapemba bila huruma halafu eti ni mtu Mwema?. Labda ikiwa ni muhafidhina mwenzake.
 
huu mjadala plus alichoandika Ansbert Ngurumo jana umeniongezea tafakuri nzito! Bravo Ashadii kwa kuongoza vyema mjadala.
 
huu mjadala plus alichoandika Ansbert Ngurumo jana umeniongezea tafakuri nzito! Bravo Ashadii kwa kuongoza vyema mjadala.
<br />
<br />
ngurumo jana kaandika makala nzuri sana,uelewa wa watu ni tofauti,kama watu hawatambui mchango wa rais mstaafu pamoja na mapungufu yake basi watanzania tuna matatizo,wananchi wanamkumbuka wanajua na kutambua alikowatoa,
 
Appreciated Mkuu... nataka zaidi wataonielewa na kujua/ku realise where i am coming from... Kwamba kua interested na Siasa sio lazima niwe tu blind na kushikilia sehemu moja in the name of upinzani wa Chama kingine... Sijaona kama tuna that Luxury ya kuona na kugenrelise kua Chama hiki is absolutely RIGHT na kingine WRONG..... Naona kua woote in most cases (CDM Vs CCM) wapo sawa tu... kinacho tofautisha this two parties ni kwamba one is in power the other is not.... Na napenda yule ambae yupo katika Chama kimoja wapo akasifia wanapo patia na kukemea wanapo kkosea it is so constructive - kuliko kufumba macho na kusifia upuuzi sababu tu ni chama chake husika kimehusika....

Asha; + Mkandara;

To me what I have just coloured blue worth a thread!! Ni muhimu tena muhimu sana ... nafikiri Mkandara atakuwa na cha kusema hapa!

Inanitatiza sana kwa nini mambo yawe kama yalivyo... yaani kuna UPOFU ..tena UPOFU very siginificant ... Hivi kweli kabisa kama Mimi napingana na wewe inaweza kufikia kukataa kuita maji maji kwa sababu mimi mpinzani wako nimatangulia kujaita maji kuwa ni maji. Hivi kweli ni lazima kuyatafutia jina lingine tu simply kwa kuwa ukijaita maji utaonekana kuwa emefungamana na Mimi mpinzania wako. Hivi kweli is it wise ... Kukataa maji kuwa si maji kwa kuwa Mpinzani wangu ameona kuwa ni maji!

Nini kitatokea kama Mpinzani akaamua Kusimamia umoja na uzalendo wa Kitaifa ... Si unaona ... Mwenzake Itabidi aukane uzalendo na Utaifa... Nini kitatokea kama Chama kimoja kina sera sahihi kabisa dhidi ya jambo fulani ....lakini .... NI MWIKO chama kingine kuliunga mkono kwani inaonekana kuwa huo ni usaliti. Hivi kweli huu si upuuzi ... does it realy make sense ... Yaani makundi mawili yanajiita vyama vya siasa vinafanya michezo ..or call it MIND GAMES ...Lakini Mind game na maisha ya Watanzania wote...

Nani haona nini kinatokea pale bungeni ...sometimes totaly nonses... Unaona kabisa Mbunge wa CCM mwingine mzuri you can tell anavyojenga hoja nk ...Lakini Unaona waziwazi akifikia mahili inabidi asifie CHADEMA au Kuunga mono Hoja iliyotolewa na CHADEMA ...anapatwa na Kigugumizi.... Akidhubutu kuruka mstari na kuonyesha kama yuko upande sahihi wa hoja ya manufaa kwa jamii lakini ya CHADEMA ..anafanyiwa KIKAO na wana CCM wenzake! Na Kwa upande wa CHADEMA mambo ni the same ...hata kama wana nafuu fulani ...lakini tungetegemea wajiamini kabisa .... Kama ni issue inayojumuisha manufaaa ya kitaifa, uzalendo, Utu na heshima ya Mtanzania hata kama imetoka upanda wa CCM wao CHADEMA bila kumumnya maneno ... Inabidi waisifu na kuisimamia na kuinga mkono with full force ..full imapact ..kama it wise to do so!!

Nani haoni kuwa CCM na CHADEMA kunawakati wanaonekana kama wanatoka nchi mbili tofauti kabisa.

Hivi nani haoni kuwa Vyama vikubwa viwili vinapofikia hapo ... vinajenga MTINDIO WA KIMAENDELEO USIOPIMIKA na kumalizika kirahisi.

CCM kingekuwa chama safi , chenye maadili na muelekeo wa kusimamia na kujenga maslahi ya Watanzania ...KINGEJIAMINI NA KUSIMAMA PAMOJA NA CHADEMA ...KAMA ambavyo CHADEMA ingefanya pia ...what is a big deal in that? Vyama hivyo havitabadilika na kuwa kimoja vikionyesha Kukomaa kwa namna hiyo ambako kumesheheni ... kujiamini, Busara, Kujali, Heshima and all moral values needed by this nation so much!!

Lakini Kilango akionekana kumuunga Mkono Zito ...ohhhhh...shida ..wala sio kaunga mkono CHADEMA ...lakini Kaunga mkono hoja yake yenye mantiki na kanuni yenye kujenga Tiafa lote kwa Ujumla. Huko CHADEMA the same!!

I am sure something need to be done in this issue baada ya sisi kumaliza to compare and contrast present and past presidents!!
 
Sishangai kwani maneno hayo yote hutokea kama hali ya kukata tamaa au majuto nafsini mwa mtu au watu. Si vibaya kusema heri kufa kwa risasi kuliko kufa kwa kunyongwa japo vyote ni vifo tu. Wanaosema heri ya mkapa wako sahihi kwani unapolinganisha watu wawili lazima ataonekana mmoja bora kuliko mwingine hata katika wabovu kuna wabovu wenye ahueni. Hii haimanishi kwamba mkapa alkuwa ni kiongozi bora waliowahi kutokea tanzania bali kama ni kuwapima katika mzani mkapa ataonekana mwenye uzito mkubwa kuelekea maendeleo na jk. Kuwa na uzito mdogo kuelekea maendeleo.
 
kichekesho. Hivo Mkapa ni bora kuliko Kikwete?. Ama nyinyi muna ndoto kweli. Huyu Mkapa ni adui wa nchi hii ametuua wapemba bila huruma halafu eti ni mtu Mwema?. Labda ikiwa ni muhafidhina mwenzake.

Mkuu next time soma basi zaidi ya heading before huja comment.... ingekua
hivo ulivoelewa kweli ingekua kichekesho... But naona huajasoma the whole posts....

huu mjadala plus alichoandika Ansbert Ngurumo jana umeniongezea tafakuri nzito! Bravo Ashadii kwa kuongoza vyema mjadala.

Mtazamo... nashukuru saaana in your interest and appreciation...
Lakini hata hivo ningefurahi zaidi ungekua umegusia msimamo wako
na mtazamo pia... as much as it seems una support....


bora Makinda awe rais ili tuwahi machafuko.

OMG!!! I hope unatania.... Dah!
 
AshaDii na Azimio Jipya,

Wakuu zangu lazima mfahamu kwamba lugha mnayotumia hapa ni ya kisonmi sana na lazima mtu akafanye homework yake ili vitu vijae kichwani.. Moja kubwa ambalo nimeliona mkizungumzia ni mchanganyiko wa rangi mbili za Njano na Blue kwa ufasaha ambao msomaji lazima afahamu viwango na nini matokeo ya mchanganyiko huo..

Sasa kwa wengine wasiojua mnachozungumza, wao huona mbele yao rangi ya Kijani! na wakashangaa sana kwa nini inazungumzia mchangayiko wa rangi za njano na Blue hali kinachoonekana kwoa ni rangi ya Kijani...Kwa maana hii Wadanganyika wengi hawafahamu matokeo ya kuchanganya rangi hizo wala kwa kiwango gani hivyo hukurupuka na kuanza kupinga kwa sababu maishani mwao hawajawahi kuona rangi hizi mbili zikichanganywa na nini kitatokeo kama rangi hizi zitachanganywa..

Na ndio maana hata mimi hujaribu sana kuendelea kutetea hoja na mtazamo wangu pamoja na kwamba nafahamu fika kwamba wengi ya watu wasionielewa ni pamoja na wale ambao hawajui mchanganyiko wa rangi isipokuwa rangi (readymade) wanayoiona machoni mwao..
- PATAMU HAPO
 
Back
Top Bottom