AshaDii,Jasusi you genuinely believe angekua kiongozi mwingine hata kama ni CCM humo
humo ndani hali ingekua tofauti?? Na in other words huu ufisadi umeanza miaka hii mitano ya karibuni??
<br />Hii misingi yote mibovu ya kiutawala na ya kiutendaji ni matunda ya Benjamini Mkapa, ambayo kamkabidhi JK.<br />
JK na Mkapa wote ni marais wabovu walipata kutokea hapa Tanzania tumeona kwenye vipindi vyao mambo mengi ya UFISADI na uporaji wa mali za umma yamefanyika sana wakati wa vipindi vyao.<br />
Tofauti ya Mkapa na Jk, ni moja tu, Mkapa ni mkali na Jk ni mpole.
Kweli Mkapa alikwenda ikulu akijua kazi anayokwenda kuifanya.
Ya kuuza Migodi yetu kwa wazungu na kuuziana nyumba za serikali kwa bei ya kutupa, wewe unaonekana wazee wako walikuwa kwenye serikali ya Mkapa ndio maana unasifia eti maisha yalikuwa mazuri labda kwenu
Tuseme ukweli, hata wakati wa Mkapa mambo mengi yalikuwa exposed, particularly first term. Maana nakumbuka issue za akina Mbilinyi, idd Simba, Hasi Kitine and several others ambao walikuwa wakifanya ufisadi tu Mkapa hawaangalii usoni anawatimua instantly. Mkapa alikuja tu kuchanganyikiwa miaka miwili ya mwisho, but the guy real did his best. Awamu ya kwanza na ya pili mwanzoni hakufumbia macho upuuzi na alikuwa anajitahidi kuweka kila kitu wazi. Na alichokuwa anakifanya kila mtu alikuwa anaweza kukiona na kuappreciate. Ni wakati wa Mkapa ambapo serikali ilikuwa inaweza kufanya mambo mengi kwa bajeti yake yenyewe. Hata Kikwete alipoingia madarakani alikiri kwamba alikuta fedha kibao za kigeni na za ndani. Leo zimepukutika zote na kilichofanyika cha maana hakipo.Jasusi ... unazungumzia la Jairo hili la juzi... angalia ungozi mzima wa JK... mangapi yamekua exposed?? matatizo mangapi saizi yamekua as a result of that exposure?? Na umejiuliza hayo yoote yalokua exposed ni since when yalianza na mizizi yake iko tangled vipi?? JK yupo kwenye politics like forever - swali napenda nijue ni kwamba alijua yoote hayo, alifanya hivo kwa malengo gani kama hawezi ya solve??
AshaDii,
Nadhani hoja nzima ilikuwa fikra za watu wanaosema ni kheri ya Mkapa angerudi kuliko uongozi wa JK kuwa msingi wa hoja yako kuwashangaa watu hawa lakini sikutegemea kwamba hata wewe unaona bora ya JK ktk kipimo cha viongozi wawili wabovu. Binafsi siku zote humpima kiongozi sio kwa jambo moja na wala simpimi kiongozi kwa kufanikisha sheria zisiyokuja Uchumi wa nchi kwani hakuna sifa kama hiyo ktk uongozi bora kama huboreshi maisha ya wananchi..
Niliwahi kusema kwa wanaomsifia Mkapa kwamba aliweza piga hatua tatu mbele muhimu za ufanisi ktk uchumi wa Tanzania lakini akatudisha nyuma hatua saba hivyo kwa ujumla wake Mkapa aliturudisha nyuma hatua nne sawa na JK ambaye aliukuta uchumi upo hatua nne nyuma katurudisha hatua nyingine mbili zaidi na kufika hatua sita nyuma. hatua mbili nyuma hazina unafuu wowote kwa sababu gari lililokwama huwezi jaribu kuliendesha ktk tope bila kutafuta mbinu za kulikwamua kwanza.
Kwa nini wananchi wanasikia uchungu zaidi leo wakati wa JK kuliko wakati wa Mkapa au Miwnyi?..ni kwa sababu tulikuwa ktk kuporomoka tayari (hatua nne nyuma) hivyo ongezeko lolote la kuporomoka chini linakuwa na machungu zaidi kuliko tungekuwa ktk hali nzuri ya kiuchumi na tukashuka kama nchi za Ulaya leo hii.
Sasa sababu hasa ya wananchi kushindwa kufikia maamuzi mazuri na ya busara ktk mapendekezo kama haya ni kwa sababu hatujawahi kuona maendeleo ya kiuchumi zaidi ya miaka ya mwanzo ya Nyerere between 1972 na 1978 kabla ya vita ya Uganda ambapo GDP yetu ilikuwa ikipanda kwa zaidi ya asilimia 6 na hadi 10 kwa mara ya kwanza ktk historia ya nchi yetu. Lakini kwa bahati mbaya ni ktk miaka ya 80's ndio watu wengi tunayo kumbukumbu yake kwa sababu tulishuka hadi kuanza kula mtaji na kifo cha Ujamaa ndio kilitumaliza kabisa.
Ni vigumu sana kumpata mtu leo hii anayekumbuka Tanzania ya mwalimu Nyerere ambayo ilikuwa nchi ya pili duniani kwa kuproduce Chai, halafu ukitazama pamba, kahawa, korosho na katani tukiwa ktk best 10 bila kusahau Zanzibar ikiongoza duniani kwa kuzalisha Karafuu na spices nyinginezo. Leo hii ni historia ktk vitabu, hatupo hata katika picha ya wazalishaji pamoja na kuwa tumeingia ktk Ubepari - Pamoja na kwamba Ardhi bado tunayo na nguvukazi imeongezeka maradufu.. hatuna cha kujivuania zaidi ya kuhesabu madeni na mchango wa misaada ktk GDP yetu wakati hakuna mfumo bora wa kutoza na ukusanyaji kodi..
Bado mahotel yanabadilishana mikono kwa majina kila baada ya miaka mitano na Jk hawezi kuwalazimisha wenye Hotels wasiuze kwa sababu hiyo ni biashara ya mtu sio ya serikali. Biashara ikishuka hakuna sheria ya kumfunga mtu kulazimishwa abakie na biashara isiyolipa, ingawa tunajua wanatengeza faida kubwa. Hayo Madini, Wanyama pori, Viwanda na uwekezaji woote ulotanguliwa na mikataba/ubinafsishaji wa Mwinyi na Mkapa ulikuwa Mbaya sana kiasi kwamba JK hawezi kurekebisha kitu unless yeye mwenyewe achukue maamuzi magumu..Nakumbuka Jk alisema mashirika ya madini yataanza kulipa ushuru wa mapato mwaka 2010 lakini ktk bajeti sikusikia hilo likizungumziwa na limeongeza pato la taifa kwa kiasi gani..
Ni yapi hayo maamuzi magumu.. nadhani hapa ndipo napoweza kumpongeza Lowassa kwa kauli yake ingawa sina hakika kama alikuwa na maana sawa na yangu. Maamuzi magumu ni kuvunja mikataba yote mibovu, mikataba iisiyokuwa na faida kwa nchi yetu zaidi ya kuuza utu wetu kwa fedha. Kuchukua maamuzi kama ya rais Chavez wa Venezuela kwa sababu mikataba yote iliyotanguliwa na Mwinyi au Mkapa imeifunga serikali ktk gereza, hali ambayo sii rahisi kujikwamua na labda niseme kwamba serikali imekamatwa pabaya kama shirika la Tanesco ktk sekta zote za Uzalishaji...Ubinafsishaji umekuwa Ukoloni mamboleo tunalipa madeni yasiyokwisha, kuwadhalilisha wananchi zaidi badala ya kuwajenga.
Na maadam JK ameshindwa kusimama imara na kusoma alama za nyakati na kuchukua maamuzi magumu kama Lowassa alivyofanya na Citywater matokeo yake ndio maana JK anaonekana kiongozi dhaifu na asiyeweza kuongoza kutokana na urithi alochukua na kuapa kuboresha maisha ya wananchi...Kifupi JK kashindwa kuongoza, GDP inayoongezeka kwa mauzo ya mashirika ya nje hali mfuko wa Taifa haifaidiki na rasilimali/ maliasili zilizopo ni sawa na kujaribu kujaza maji ndoo iliyotoboka..Haisaidii kitu kupanda kwa GDP ikiwa hakuna kitu kinaongezeka ktk mfuko wa Taifa kulingana na mahitaji na kupanda kwa maisha..
Tatizo la nchi hii siyo kiongozi mmoja mmoja kama watu wanavyotaka kutuaminisha. Tatizo ni mfumo wa kikatiba na kisheria unaotoa mwanya wa viongozi wabovu kuzalishwa, kulelewa na hadi kushika nafasi za juu za uongozi. Kwa taarifa yako tatizo la uongozzi nchi hii limeshuka toka kwa raisi mpaka kwenye ngazi za juu na za kati za uongozi wa serikali na kwa bahati mbaya hapo ndipo maamuzi makubwa ya matumizi ya pesa za walipa kodi yanapoanzia. Hata utamaduni wa utendaji kazi wa serikali hautuwezeshi kwenda mbele kwani umesababisha wataalamu kuwa mabingwa wa kusoma matakwa ya wanasiasa na kutoa ushauri unaoendana na mambo ambayo wanasiasa wanapenda kuyasikia. Kwa ufupi tupo kwenye tope zito "quagmire"na tunaendelea kuzama.
Naona hapa "great thinkers" wako bize wanajadili nani zaidi utadhani wako kwenye kipindi cha nani zaidi kwenye muziki cha redio one. Ninavyojua "simple minded people" ndio wanaopoteza muda wao kujadili watu.
<br />Yaani una maana kwamba Tanzania tutapata rais worse than Kikwete? God forbid!