Ni kama alivyosema Juliana Shonza, Mbowe must be disposed

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Katika Thread yake ya tarehe 24 February 2016, Ndugu Juliana Shonza aliandika Ushauri kwa Jirani: Mbowe must be disposed! akitaja sababu kadhaa za kwanini anadhani mbowe HAFAI kuwa Kiongozi si kwa chama chake tu bali popote pale Tanzania. Nilitafakari juu ya fikra zake hizo na kwa kweli baada ya Mgogoro wa TBC na CHADEMA ambao msingi wake ulikuwa kukurupuka kwa MBOWE nakubaliana kabisa na Ndugu Shonza kuwa Freeman MUST BE DISPOSED..!

Sifa moja ya Kiongozi bora ni kufanya informed decisions, maamuzi yaliyopitia tafakuru ya kutosha na kupima madhara na faida ya maamuzi hayo, katika kile ambacho kimethibitika kuwa ni kukurupuka, Mbowe aliwafukuza waandishi wa TBC wakiwa Live katika mkutano wao wa ufunguzi Mbagala, katika namna ya kudhalilisha na ambayo ingepelekea kudhuriwa kwa waandishi hao ama mali zao kuharibiwa. Leo amejitokeza hadharani bila aibu anasema alishinikizwa na kupotoshwa wakati anafanya maamuzi hayo, alisema hivi pia siku Lowasa anarudi CCM, kwa Kiongozi wa Juu kabisa wa Chama tena aliyekuwepo madarakani kwa miongo kadhaa kurudia kosa lile lile na kutoa sababu zile zile za kufanya kosa hilo ni UJUHA.

Kilichonifurahisha zaidi ni akili za wafuasi wa CHADEMA, kwa namna wanavyoiponda TBC na kwa namna walivyompongeza Mwenyekiti wao kwa kuwafukuza TBC ni ajabu kwa namna wanavyosifia na kushangilia uamuzi wa kuwaomba msamaha TBC na kuwaomba warushe matangazo yao kwa mara nyingine. Chama kile cha Freeman, kina tatizo kubwa zaidi ya nilivyokuwa nikifikiria awali.,na tatizo hilo linaanzia kwa wafuasi kabla ya Viongozi, kuwa na wafuasi wasio na mwelekeo wasiojua wanataka nini, wanageuzwa kama samaki kikaangoni., ni tatizo na kwasababu hiyo Viongozi wanajua udhaifu wa wanachama wao na wanawajua kwa dhati kabisa kuwa ni watu wasiojielewa, watu wengine wanawaita kwa lile jina baya la Manyumbu, mimi siwezi kuwaita hivyo ila hili la kushangilia matangazo ya TBC kurudishwa limenifikirisha.

Freeman amefikia mwisho wa kufikiri, hana jipya, amekosa mwelekeo, amepoteza jimboni na anapoteza Taifani, amepanic na anaona giza limetanda katika safari yake ya kisiasa. Ni Mbowe amesababisha Chama kukimbiwa na Wabunge, Ni Mbowe ameivuruga Bavicha aliwapangia safu ya uongozi na watu aliowaweka wakamkimbia, ni mbowe ameivuruga Bawacha akamuweka Mdee kwasababu zake binafsi, akagawa ubunge wa Viti maalum kwa upendeleo na matamanio ya nafsi yake, akaendesha Chama kama kijiwe cha wahuni, wale wenye fikra wakamkimbia. Chadema haikubaliki kwa wasomi, haikubaliki na Wazee, haikuwahi kukubalika na wanawake wa nchi hii, haikubaliki kwa Vijana na haikubaliki Kaskazini (hakuna Chadema Arusha, kilimanjaro wala manyara) wala Kusini , haina base Mashariki wala magharibi, Chadema ya leo ni YATIMA.

CHADEMA wamepoteza hamasa katika mikutano yao, wamepoteza mvuto kwa wananchi, wamekosa ajenda na hawana sera. Sio coverage ya TBC, ITV, Clouds TV ama media yeyote ile inaweza kuwasaidia kwasasa. Narudia tena kuwa Kampeni ni maarifa, mipango na akili, CHADEMA WAMEKOSA VYOTE....!!
 
Tumia ubongo kufikiri, hebu jiulize kwani mbowe ndiyo aliyendaa huo Mkutano wa reconciliation? Kwanini TEF na NEC wameona umuhimu wa kuwakutanisha CDM na TBC kuondoa hizo tofauti? Je hukumsikia Dr. Rioba mwenyewe akiomba radhi kwa kitendo kilichofanywa na watangazaji.

BTW, elewa kuwa kwenye kutafuta suluhu kila upande haupaswi kushupaa, bali hujishusha kuleta mardhiano

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 
Katika tukio lile inamuonesha Mbowe akipewa ujumbe wa shinikizo pasipo tafakuri nae akatekeleza, bila kujali itachukuliwa vipi na taasisi zingine pamoja na wananchi.KAKOSA SIFA MUHIMU YA UONGOZI MUST BE DISPOSED.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom