Ni jibu hapa hapa tafadhali!

Bakulutu

JF-Expert Member
Nov 30, 2011
2,544
1,760
Naomba kujua ni kiasi gani cha mbegu {mahindi} kina hitajika kwa heka 1 ya mahindi?
KILIMO KWANZA...MAPINDUZI YA KIJANI.
 
Inawezekana hakuna wakulima humu. Ni vizuri ukaulizie kwenye maduka yanayouza mbegu za kilimo kama za mahindi unaweza kupata msaada.
 
Naomba kujua ni kiasi gani cha mbegu {mahindi} kina hitajika kwa heka 1 ya mahindi?
KILIMO KWANZA...MAPINDUZI YA KIJANI.

Kama wapo watu wa mambo ya kilimo hapa JF watakusaidia. Mkuu hiyo slogan ya: KILIMO KWANZA hivi kweli italeta matunda kwa wakulima hapa nchini ikiwa serikali yako imeshindwa kuelimisha mtu kama wewe? Tumebaki kuimba tu, mara: siasa ni kilimo, kilimo cha kufa na kupona, kilimo ni uti wa mgongo, kilimo kwanza. Ifikapo 2015 utasikia tena : SIASA NI KILIMO!
 
Kutoka moyoni:
Ni msemo tuu watu tunajifaraji kama vile..jembe halimtupi mkulima, lakin hii kauli mbiu haina tija yeyote,ni janja na sehemu ya waleee kujitengenezea posho kwa matreta mabovu, pembekeo feki...!
Mtaji wa masikini ni nguvu zako mwenyewe!
 
Umenikumbusha, JF Wamesahau kuweka jukwaa la wakulima humu. Hawa jamaa nao ni muhimu sana katika jamii yetu. Hebu wekeni jukwaa lao ili nao tupate maoni na michango yao. JUKWAA LA WAKULIMA
 
Back
Top Bottom